Nipeni ushauri nisome kozi gani Certificate niweze kuwa Afisa Mtendaji wa Kata

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
1,885
Reaction score
3,227
Mm ni mwanafunzi wa chuo X kada ya ualimu mwaka wa pili (degree) lakini pia nazitamani sana hizi kazi za uafisa utendaji wa kata ikitokea ajira katika ualimu ikiwa ni changamoto kupata.

Sasa nataka kujiendeleza kielimu nikiwa hapahapa chuo kuna kozi nyingi tu zinatolewa sasa naomba mrejesho ni kozi gani itanipa sifa ya kulamba asali ya uafisa utendaji kwa ngazi ya certificate au lazima diploma.

 
Samahani kama nitakukwaza, Ila afisa mtendaji chuo Chao kipo hombolo dodoma, wao wanapewa Sana kipaumbele Cha kazi za utendaji, hata mzumbe hiyo kozi hipo, Ila hombolo ndio penyewe kwa hiyo kada.
 
Hii picha umeiweka kwa ajili ya kupambia tu mada yako?

Hiyo kazi ya uafisa mtendaji kata kama huna connection, kuipata ni majaliwa.
 
Hongera na shule Kiongozi.

Unaweza kusoma fani za Public Administration, Law, Rural Development and Policy n.k

Ingawaje kuna watu waliajiriwa hizo nafasi kwa fani za Accounts then baada ya Mwaka Mmoja niliwakuta wako Idara ya Fedha 🙌

Kwasasa Connection ni muhimu kuwa nayo
 
Unawaza kuwa mtumwa. Ajira Ni utumwa.

Unaajiriiwa na mtu halafu yeye anakaa pale nyie mnapambania ndoto zake.
 
Kwahyo nisome diploma au certificate hapo ndo nitameet required qualification
 
Sheria, maendeleo ya Jamii, utawala, uongozi. Ila unapaswa kujua mishahara yao ni midogo sana, ukilinganisha na ualimu.
 
Certificate ni kwa level ya mtaa/kijiji tu
Na soon wataanza kuchukua wa diploma.
Kata walukuwa wanachukua wa diploma ila upepo ushapinduka sasa wameanza na degree holder.
Ungetaka hizo kazi ungeachana na education mapema ili uokoe wakati.
Mambo yanabadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…