Nipo Dar, biashara ipi inalipa kati ya kukaanga miguu ya kuku na kukaanga mihogo?

Nipo Dar, biashara ipi inalipa kati ya kukaanga miguu ya kuku na kukaanga mihogo?

Sasa mkuu wewe ndo hujaielewa mada yangu
Mada yangu ina Option ya biashara mbili mihongo na kuku
Sasa wewe mkuu umeenda mbali sana et nijifunze kushona? Hujawaza ada ya kujifunza kushona inatoka wapi?
Hujawaza wakati najifunza kushona ntakuwa na afford vipi basic needs kipindi chote hicho!
Alafu ukishajifunza kushona utafute pesa ya kununulia mashine, ukodishe ofisi au usubirie mtu akuajiri
 
Hongera sana Mkuu kwa kuwa mbunifu, kujiongeza badala ya kuketi na kulalamika. Anzia ulipo, anza ulivyo, Nia ya dhati itakufikisha kwenye Mafanikio yako! Naomba ni'tag' siku utakayoanza Biashara. Nitafurahi kukutembelea na kukuongezea Mtaji zaidi kama motisha ya kukuza Biashara yako. 👏👏👏👏👏
 
Nina laki MBILI
Kwa7b unaanza basi anza kigumu gumu huku ukizidi kuangalia upepo wa biz…

Biashara ya kukaanga mihogo :-

Nunua ndoo (deli) 10,000.
Ndoo ya maj, sio lazma kununua.
Ucnunue jiko, tumia mafiga na kuni.
Kuni za elf 2.
Azima meza ndogo ila sio lazima.
Kod ya eneo 10,000 inategemea ulipo.
Kalai 20,000. Ila ww anza na sufuria.
Upau elf3. We tumia spoku ya baiskel.
Chumvi kubwa 400.
Vifungashio 1,500.
Chachandu 2,000.
Benchi la wateja elf 10 azima pia.
Sahani za elf 10 ila w tumia za hom.
Usianze kwa kujumua kiroba kizima ila ww anza na mihigo ya elfu 5 kutegemea na uhitaji wa wateja wako.

Mpaka hapo utakuwa umebana matumizi kwa kiasi kikubwa mno.

Kufika hapa biz yako ipo tayari kuianza.

Bila kusahau pga maombi mengi kwa Mungu Baba ili akupe wepesi ktk hili.

Ukifanya biashara hii ndani ya mwezi m1 utakuwa ushaanza kuwa na wateja wa uhakika.

Kumbuka : Biashara yoyote ile kikubwa ni usafi.

Hivyo inahitaji uwe na lugha nzuri, muonekano mzuri uwapo kazn, usafi wa hali ya juu ktk iyo biashara.
 
ASante mkuu nimekuelewa sana
 
Mihogo kaangaa asubuhi halafu piga na hy ya viungo vya kuku mchana/jioni, ikiwa mtaani itakuwa unyama.
Hii ni idea kubwa sana. Cha kuongezea tafuta na shamba pembezoni mwa daa lima hio mihogo mwezi disemba. Unga unga kodi hata heka 2. Baadae ya miezi 6 utauza/ choma hio mihogo kutoka shambani kwako. Usisahau na ndugu yake viazi vitamu.
Una akili sana, baada ya mwaka utakuwa mbali. Ukifanikiwa ututag usipotee.
Kumbuka mwanzo mgumu.
 
Back
Top Bottom