Mama aboreshe uhusiano na Majirani zetu wote
Kisha tuwasainishe kuwa hakutakuwa ma agression baina ya Nchi zetu...
Kupunguza jeshi si sahihi na kusainish si garantii kuwa hawatageuka. Tumewasainisha mengi na wamegeuka kwenye mengi...usipokua mwaminifu kwa kidogo hata kikubwa huwezi kuwa mwaminifu.
Mama anapaswa kutafuta njia bora za kiuchumi yaani kuongeza mapato...huwezi kukaa na jirani wanaokwaruzana daily harafu ulinzi wako ukawa wa mashaka.
Yeye aamue kuingia katika bahari na kukodisha kwa wawekezaji vitabu vya bahari.kuu wavue walipe pesa tuachana na JMT kuwekeza kwenye uvivu wa bahari kuu.
Hakuna namna atakayofanikiwa pasipo kuwajali wataalam wake wanapawa maslah mazur ikiwemo mazingira mazuri na wanafanya kazi kwa bidii.
Akaboreshe miundo mbinu ya utalii,reli,anga na Barbara ili kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa zao kutoka kwenye uzalishaji kwenda kwa mlaji na viwandani.
Waangalie namna bora ya kuongeza thamani km uchakataji wa bidhaa..ndo namna pekee tunaweza kujihakikishia usalama wa chakula na bidhaa zingine na kujipatia hifadhi kubwa ya fedha za kigezo.
Akasimamie vema sekta ya madini iwe kuwa faraja badala ya kadhaa baina ya wawekezaji na wananchi na wananchi na serikali yao angalau ifikie uwezo wa kushinda na utalii lol pato is taifa.
Akashawishi wawekezaji wenye pesa waje kuwekeza kwa ubia na watanzania ili kuongeza ajira na kuwapa exposure vijana wetu.
Akaanza utaratibu wa kukodisha wataalam nchi zingine zinazohitaji wataalam hasa za SADc ambapo serikali itapata kodi kwa mtaalam kwenda kutumia nje kwa utaratibu rasmi.
Kupunguza matumizi ya mashirika hasa kwa njia sahihi na bora zaidi mfano kuongeza matumizi ya umeme wa gesi na maji badala ya umeme wa mafuta.
Kuomba kurejea mkataba ya madini na mambo mengine ili kuona namna bora ya kuongeza mapato. Kuboresha mitaala ya elimu iendane na mahitaji ya wakati pamoja na kumshawishi wabunge wamekubali wapunguze maslah yao ili pesa ziende kwenye huduma za jamii.
Kukodisha vitalu vya uvivu kwenye maziwa makuu kwa wawekezaji ili waweze kuzalisha na kusindika minofu nchini. Kuboresha sayansi ikiwemo uwekezaji wa utalii wa kiafya,kufufua tafiti za kisayansi kwenye mashirika na taasisi za kimkakakti km shirika la nyumbu,vyuo vikuu,vituo vya utafiti kwa kushirikiana na wabia.
Kwa leo ni hayo
Alisikikia mkubwa mmoja kwenye kikao cha kijiji