Biashara kati ya Tanzania na Kenya mbona ipo miaka mingi mkuu, ninachohofia ni hizi moves zinazoharakishwa ambazo zitaipa kenya advantages zaidi za kiuwekezaji nchini kwao huku wakifaidika kwa kutengeneza ajira zaidi na kuifanya Tanzania kuwa soko tu la bidhaa zao jambao ambalo litaendelea kuua ajira za watu wetu.
Kenyatta anaposema watanzania wanaruhusiwa kufanya kazi na biashara kenya bila zuio lolote kuna mtego mkubwa ndani yake, ndo maana wengine tunatahadharisha kwamba haya mahusiano yaendelee kwa kasi iliyokuwepo au iliyozoeleka, maana kuna watu wanataka twende kwa kasi ya 5G kwenye integration na kenya, jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa mustakabali wa nchi na watu wetu.