Nipo kwenye dalalada naangalia nauli nimedondosha Naombeni msaada wa haraka

Nipo kwenye dalalada naangalia nauli nimedondosha Naombeni msaada wa haraka

Jamani nipo kwenye dalalada natokea posta naenda gongolamboto mda huu, nimeangalia mifuko yote nilikuwa na buku lakini siioni sijui nilidondoshea wapi na konda mda huu ndoanasanya nauli afu ana uso mzito wa hasira ya kupanda kwa bei ya wese. Jamani Naombeni ushauri wa haraka nitumie technic gani nijinusuru na hii fedheha.
Jifanye kichaa! yaani chizi kichizi..!!
 
Umenikumbusha wimbo wa Noorah,Ila bro. Hapo mwambie konda ntakulipa mwisho wa gari halafu piga simu kwa mshikaji akurushie then unmlipa kwa muhamala,Hapo umelinda status kinyume na hapo Unaolewaa!
 
Mwambie konda nimeangusha siioni naamini Kuna wasamaria wema watakupiga tafu au waeleze majirani .acha woga na aibu kijana...Incase konda atakushusha nadhani atakuwa amekusogeza hata tazara ...hapo na Tazara si mbali fanya mazoezi tu piga mwendo Hadi gongolamboto...
 
Sema Kwa sauti Bwana Yesu asifiwe Sana.

Igiza kama mtumishi wa Mungu unatoa neno la uzima wa milele.
Nauli hutolipa na mwisho sadaka pia utapewa.
Vipi umefanyaje mpaka umefika home mbona hujatulisha
 
Jamani nipo kwenye dalalada natokea posta naenda gongolamboto mda huu, nimeangalia mifuko yote nilikuwa na buku lakini siioni sijui nilidondoshea wapi na konda mda huu ndoanasanya nauli afu ana uso mzito wa hasira ya kupanda kwa bei ya wese. Jamani Naombeni ushauri wa haraka nitumie technic gani nijinusuru na hii fedheha.
Jifanye kama umezimia "jizimishe"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani nipo kwenye dalalada natokea posta naenda gongolamboto mda huu, nimeangalia mifuko yote nilikuwa na buku lakini siioni sijui nilidondoshea wapi na konda mda huu ndoanasanya nauli afu ana uso mzito wa hasira ya kupanda kwa bei ya wese.

Jamani Naombeni ushauri wa haraka nitumie technic gani nijinusuru na hii fedheha.
Omba mkopo songesha au mitandao mingine halafu utatoa utatoa ukifika ulipe.Kama unadaiwa mchek jamaa Ako akurushie
 
Huo ndo muda muafaka wa kupandisha Mashetani!
 
Back
Top Bottom