Nipo kwenye process ya kufungua restaurant na nimekwama kwenye suala la lighting

Nipo kwenye process ya kufungua restaurant na nimekwama kwenye suala la lighting

BLACK_

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2020
Posts
1,885
Reaction score
4,193
Nipo kwenye process ya kufungua restaurant yangu, na kwa sasa nipo kwenye hatua za interior setup na ambience ya sehemu. Kadri ninavyoendelea kupanga vitu, nimegundua lighting inaweza kubadilisha kabisa experience ya mteja na muonekano wa chakula

Swali ni hili

Ungependa kula restaurant yenye mwanga gani?
A. Bulb nyeupe (bright, clean, modern vibe)

Lights.jpeg


B. Bulb za manjano (warm, cozy, relaxing vibe)

39e91486-1c9f-4562-83a3-29e5a41104cf.jpeg


Naomba pia mtoe sababu:

÷Ni mwanga gani unafanya chakula kionekane vizuri zaidi?

÷Ni upi unafanya ujisikie comfortable kukaa muda mrefu?

÷Kama ni date night au family dinner, ungechagua upi?

Kwa wenye restaurants au business experience:
Ni lighting gani imeonekana kuwafanya wateja wakae zaidi au wa-order zaidi?
Maoni yenu yanaweza kunisaidia kufanya decision sahihi kabla ya opening

Maoni yenu ni muhimu kwenye jambo langu,naomba kuwasilisha🙏
 
Kazi utapata,kwanini B naomba uongezee nyama kidogo shef wangu tena uwege na garlic kwa mbaali.👌
Taa za manjano zinafanya mgahawa uwe na mazingira ya warm na relaxing Wateja wanajisikia comfortable zaidi, chakula kinaonekana kitamu na sehemu inavutia hasa usiku
Yaani hata ukipiga picha inavutia kuliko taa nyeupe pee ambazo mala nyingi zipo nyumbani mteja anatakiwa aone tofauti
 
Warm light imekaa kinyamwezi. Hii ukipiga picha inatoka vizuri pia Kuna comfort flan ivi mtu anapata maana mwanga unakuwa sio mkali sana. Nipo kwenye tasnia ya stage light so najua ninacho sema kuhusu light
 
Kweli kiongozi unipikie kande halina ladha useme kuwa light italifanya liwe tamu. Nije kula ugali huko kwako haujaiva useme light itauivisha mkuu kweli. Wazo lako la kuweka light coloured huko sio baya lakini usiseme litachange mwonekano wa chakula. Nyama hata kwa mwanga wa moon n nyama tu nothin will change. Ila weka tu kila aina ya rangi ka una uwezo nunua hata zile taa za kuchange rangi coz sio wote wanapenda blue au red no wewe weka rangi zote na mteja atakua anachagua pakwenda kukaa kutokana rangi aipendayo. Cku ukifungua unipe location nije kuangusha nyago kadhaa hapo kwako bora tu iwe east africa ntakuja
 
Ukishamaliza kutengeneza niambie nikupe location nyingine ya kwenda kufungua restaurant & lounge, matajiri wa huku wazembe wanakazi ya kujaza tu lodge
 
Unafungua biashara, unaleta hoja ..... tena tuijibu na tutoe sababu sio?

Bongo nyoso
 
Back
Top Bottom