Habarini Za wakati Huu Mabibi na Mabwana.
Takribani miezi mitatu sasa nimekuwa na mahusiano na binti flani, nimekuwa nje ya mahusiano kwa muda wa miaka minne, wakati huo nikiwa najiweka sawa kwenye mambo mengine. Hivyo nilibahatika Kumpata Binti miezi mitatu iliyopita na mahusiano yetu kiujumla yalionesha Upendo uliopo si kwangu na hata na kwake pia.
Takribani mwezi Umepita kuna Tabia ilitokea kwa huyu Binti ndani ya muda wa Siku Kama tatu nilikuwa natimiza majukumu yangu katika mahusiano kama kumjulia khali Asubuhi na pia kumtakia Usiku Mwema na kujua ni Siku yake imeishaje lakini ndani ya siku kama tatu niliyatimiza haya ila hakunijibu Simu zangu. Siku Ya nne nilimpigia simu nikaongea nae akadai kwamba alikua anaumwa, nikamweleza angenipa taarifa ila kutokujibu wala Kupokea simu zangu si jambo jema. Tuliongea hayo yakaisha.
Tatizo lingine limejitokeza leo ni Takribani siku ya nne Nimejaribu kumpigia simu hapokei, namtumia sms anazipata lakini hajibu na whatsap pia namtumia na anazisoma na anaweka mpaka sTatus ila hanijibu.
Hivyo nilikua naomba Ushauri, nichukue hatua gani katika hili Suala.