Nipo njia panda wajasiriamali nisaidieni natamani kurudia tena uwekezaji huu wa kuku ila nasita

Brother, kwanza pole na hongera. Nakupa hongera kwa kuwa naamini kuna kitu umejifunza kwa hayo matatizo. "Kuomba ushauri". Katika biashara yoyote ile kabla hujaingia unatakiwa kuuliza wahenga, wakupe hatua zote na nini cha kufanya. Sitakwambia ni biashara hani ufanye lakini yafuatayo yatakusaidia.

- Moja; wekeza kwene kitu unachokijuwa. Kuna mwandishi mmoja anaitwa Brayan Rich, ameandika kitabu kimoja cha The secret of Rich people. Amesema " rich people invest in what they know". Inakuwa ni rahisi sana kutatua matatizo yanapojitokeza"

-pili; kuna kitabu kimoja kinaitwa " The Inteligent investor" kimeandikwa na Benjamini Graham ( Huyu jamaa ni role model wa Warren Buffert ). Kuna kitu kimoja alikiongelea " Worning of Santayana" - It says Those who do not remember the past are condemned to repeat it. Sasa hapo cha kujifunza ni kuwa sio kwamba tunatakiwa kukumbuka yaliyopita ili yatuimarishe na kujifunza tulipokosea ili tusiyarudie

- Tatu; Soma sana Vitabu na majarida mbalimbali. Hii inakusaidia kuongeza ujuzi zaid na umahiri katika biashara yako. Nikisema soma sana vitabu sina maana ya kuwa usome sana vitabu kuhusu biashara yako tu ( mf. Kuku) , soma vitabu mbalimbali vitakavyokujenga ila usisahau pia kusoma vinavyohusu biashara yako. Unaweza ukapata mbinu ya kutatua jambo la biashara yako kutoka kwene idea ya mwandishi aliyeandika kitabu ambacho hakihusiani ya biashaya yako. Pia vinakuimarisha usikate tamaa .

[emoji122] [emoji122] All the Best
 
Sory hapo kwene ushauri wa PILI, nimechanganya maelezo. Ni hivi ....siyo kwamba tunatakiwa kukumbuka yaliyopita ili yatutie woga na wasiwasi na kukata tamaa , Bali tunayakumbuka ili tujifunze tulipokosea na kutuimarisha zaidi tusiyarudie makosa hayo.....
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…