Jamani nipo njia ya panda.Kuna full sponsoreship kwenda kusoma masters Japan, course: Nucleur Enginering, mmi nime graduate pale udsm, Electro-mechanical engineering, NILIMALIZA MWAKA JANA, nafanya kazi nalipwa 600,000/= kwa mwezi. nahisi kwenda huko ni kupoteza muda kulingana na hali harisi ya tanzania kwenye sector ya nucleur, naomba michango yenu. Program inaanza mwakani october.mchakato wa kuwa enrolled mwisho ni december 10, 2010.Wasiwasi wangu ni kwenye ajira. Nifungueni macho jamani kama yamefumba
Kwa Upande wa taaluma hiyo, Japan ipo vizuri. Kuhusu application ya hiyo taaluma TZ ona mfano huu, hapa South Japan wapo wa- TZ wengi tu wanasoma mambo mbalimbali kuhusu Molecular Biology katika levels za Masters and PhD, nimehudhuria majumuiko mbalimbali ya kitaaluma juu ya aina ya tafiti na maendeleo ktk fani hiyo, ukilinganisha na nyumbani TZ application kwa sasa unawezakuona hakuna. Lakini kumbuka dunia yabadilika kwa kasi sana kiteknolojia na TZ sio kisiwa, hasa ukizingatia rasilimali zilizopo zinazoweza kuhusika na nuclear. Kusomea fani hiyo itakuwa ni investment nzuri kwa Human resourse ya TZ (kufikiri kizalendo). Tena iwapo ufadhili wako ni kupitia wizara ya elimu ya Japan (Mombukagusho) mara nyingi huwa ni toka Masters mpaka PhD japo mwaka huu masharti yamebadilika kidogo sana, japo yategemea iwapo wewe mwenyewe utakuwa tayari kuendelea na PhD.
Kuhusu kazi: Ni kweli ni vema kuwa na mahali pa kujishikiza, lakini kumbuka kuwa muda mfupi tu uliopita kwa mfano katika serikali watu wenye taaluma ndogo waliweza kufanya kazi serikalini. Sera utumishi zabadilika na sasa qualifications sio za kuajiriwa tu bali hata za kupanda cheo zinategemea hasa kiwango cha elimu/taaluma pamoja na mambo mengine. Kwa uzoefu nilionao, first degree haina nafasi kwa miaka michache ijayo, unless unakubali kubaki kada ya chini ya utumishi. Naomba unielewe vema hapa, bado nchi nahitaji wataalamu wengi kujitosheleza hata at diploma level, but their performance will be limited kutegemeana na viwango vya elimu na taaluma. Soon with a first degree you can not compete with others, in addition to that, if you are interested to become a good performer, you need tools;taaluma. Kwa uzoefu wangu wa miaka 19 kazini, jambo hili limesababisha vijana wengi walio katika ajira kuwahi masomoni kungali mapema, Thank God you have full Scholarship (very rare for majorities).
Mimi nakushauri ukasome, but mwamuzi wa mwiso ni wewe. Pima mambo vizuri, anagalia malengo yako, Some questions: unaelekea wapi, utafikaje unakoenda, Kuna faida gani na hasara gani kwa uamuzi utakaofanya leo, fanya Cost/benefit analysis ya choices zote mbili while taking into consideration the Total Opportunity Cost of the foregone choice, nikimaanisha kwa sasa na kwa future, then
angalia amani ya moyo wako.
Ukipenda naweza kukueleza roughly the basic living costs kwa mwanafunzi foreigner hapa Japan, ambazo estimates zake ni zinaendana sana na viwango vya scholarships za Mombukagusho kwa Masters na kwa PhD. You can comapre and may be it may add to your inputs to make decisions. If U` R` interested unaweza kunitumia PM.