Nipo njiapanda sana

Nipo njiapanda sana

EL ELYON

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
1,565
Reaction score
1,918
Hii Ni story ya kweli ya jamaa yangu na jirani yangu huku nilipo.

Anasema mwaka 2019 alipewa taarifa na ndugu yake kwamba Kuna mradi unaanza wakati wowote na atalipwa pesa nzuri Sana.

Jamaa anasema alikuwa mkoa tofauti na huyo ndugu yake akaambiwa aandae vitu vifuatavyo Kama sehemu ya kazi hiyo passport ya kusafiria ya muda mrefu, chanjo ya manjano nk maana aliambiwa Kuna safari za nje ya nchi.

Jamaa akajipigapiga kuhusu kupata hivyo vitu maana ilitakiwa avitume haraka akaamua kukopa vicoba ili apambane kupata hivyo vitu kwa haraka sana.

Maana alishaambiwa kazi inaanza muda wowote na ajiandae kwa safari. Jamaa alikuwa anafanya kazi kampuni moja mkataba nao ulikuwa huko ukingoni kwahiyo hakuongeza akijua kwamba wakati wowote stakuwa nje ya mji.

Alipokamilisha hivyo vitu akavituma Sasa na wakati huo mkataba kule kazin kwake ulikuwa umeisha Kama mwezi mmoja hivi hapo ashapanga vitu vyake na vingine ameuza akijua safari Ni wakati wowote.

Eeeh anadai alipewa taarifa mwezi wa 6 Mara mwaka ukaisha huo 2019 ukaingia 2020 nao ukafika mwezi wa 9 hakuna kuitwa zaidi akiuliza kwa nduguye anamjibu Kuna Mambo wanayakamilisha kwani mradi Ni mkubwa unajumuisha uchimbaji wa madini na shughuli za kijamii pamoja na kiwanda na upo mikoa zaidi ya 15 ya Tanzania.

Jamaa anadai ilibidi 2021 atoke huko alikokuwa aje mwanza ambako ndipo mradi au ofisi za mradi zilipo alipofika alikutana na watu wengi Sana pale ofisini kila anayemuuliza anamjibu Mambo hayaeleweki hapa kwani huo mradi tokea 2017 Ni hivyohivyo na taarifa rasmi anazo mkurugenzi tu staff walioko pale hawana taarifa za kueleweja na mradi haujulikani utaanza lini.

Kilichokuwa kinamshangaza pale ofisini Kuna vitengo watu walishapangiwa na ukipita mda Fulani wanabadilishwa kingine Kuna pesa huwa wanasaini eti zinaitwa pesa za makabiziano kweli Ni pesa nyingi kwani jamaa anasema alisaini million 26 ajabu hizo pesa zinatofautiana kwani Kuna wengine wanasaini million 100.

Jamaa anadai huo mchezo wa kusaini pesa hizo umekuwa Ni wa kila Mara ukipita muda Fulani watu mnaitwa kusaini pesa zilezile.

Anadai Kuna siku alipewa taarifa ghafla mchana kwamba watu wanatakiwa wakasaini pesa hizo ambazo ndo umekuwa mchezo wa pale siku hiyo zoezi alikuwa analisimamia mkurugenzi mwenyewe huku akisema hakuna kumsainia mtu hapa asiyesaini na lake halipo na hayo majina anayatuma siku hiyohiyo sa sjui aliuwa anayatuma kwa akina Nani.

Hiyo ilikuwa mwaka Jana mwezi wa 2 jamaa akajipa matumaini kwamba Mambo yanaenda kuwa ok. Ikapita miezi Kama miwili hivi kuko kimya alishangaa anapigiwa simu kwamba kesho asubuh anatakiwa awe ofisini haraka sana huo ulikuwa mwezi wa 6 mwaka Jana jamaa anadai alikuwa amesafiri kidogo Yuko nje ya Mwanza alikuwa Tabora huko ikabdi apambane asafiri usiki kwa usiku mradi afike Mwanza kesho yake asubuhi anadai alipofika ofisini anakutana na zoezi la siku zote la kusaini pesa za makabiziano ambazo miezi kama miwili nyuma walisaini na mkurugenzi akawa anadai anatuma majina hayo sijui wapi

Baada ya kusaini akaambiwa arudu nyumbani kwani aliitiwa hicho tu na watu wengi Sana walikuwepo nao walikuwa wanasaini.

Sasa Ni 2022 nao unaisha hakuna Cha maana zaidi ya Mambo hayo ukikaribia mwisho wa mwezi wanaibua Jambo Fulani kuonyesha mradi unaaza ili wanaochangia ofisi wachangishwe pango la ofisi na posho ya wale staff walioko pale baada ya hapo kimya ukiuliza unajibiwa Kuna mvurugano ulitokea kwahiyo ndo umechelewesha Mambo.

Sasa jamaa Hali Ni mbaya kiuchumi japo anapambana Ni Kama ameanza maisha upya mkoa mwingine pasipo kupenda.

Huo mradi anadai ofisi zipo eneo la mecco mwanza ukishuka hapo kwenye hicho kituo unaingia ndani ndani kidogo huko na upo kisirisiri Sana japo wao wanadai serikali unaujua na Ni mradi mkubwa ambao unakuja nchi hii.

Sasa anaomba kujua kwenu wajuvi wa Mambo je Ni kweli Kuna kitu Kama hicho maana humu Kuna watu wengi uwenda yupo muhanga wa mradi huo humu anajua abc zake.
Asanteni.
 
YANIA ANASAINI TU NA HELA HAPEWI?? au me mgumu kuelewaa.... 😀 😀 😀 unasaini pesa ambazo hujawahi pewa hata 100 siku ukishtakiwa mahakamani sijui utajibu nini jamaa aachane na huo upuuzi afanye mambo mengine.
 
YANIA ANASAINI TU NA HELA HAPEWI?? au me mgumu kuelewaa.... 😀 😀 😀 unasaini pesa ambazo hujawahi pewa hata 100 siku ukishtakiwa mahakamani sijui utajibu nini jamaa aachane na huo upuuzi afanye mambo mengine.
😃😃😃😃😃 Aisee bongoland hii
 
Kapigwa huyo. Mfumbue akili anapotezwa mda yaani mradi wa mamilioni ofisi 15 nchi nzima ukapange ofisi huko mecco uchochoroni. Huyo anasubiria bata atage dhahabu ndipo atajirike. Mwambie atafute Kazi ingine ya kufanya.
 
Aulizie kama pana wanigeria hapo. Kama wapo mwambie akimbie bila kugeuka nyuma atauziwa kesi.
 
Back
Top Bottom