changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Wakuu nipo kwenye bus naelekea Morogoro na nimefika maili moja kwasasa, bus nililopanda ni 2 by 2 na pembeni yangu kuna msichana ananitia mashaka mno namuhisia ni mtu wa tofauti nikimaanisha sio jamii yetu (binadamu).
Mashaka yangu yanaanzia wapi?
Huyu msichana ni mrembo halafu anaonekana mjanja fulani hivi lakini cha kunishangaza konda kamuomba jina na namba yake ya simu ili amuandikie tiketi kwa njia ya online lakini akasema namba hajaishika kichwani. Ikabdi konda achukue namba yangu ili aandike tiketi kwa niaba yake kisha mimi ndio nijue namfowadia vipi tiketi yake.
La pili simu yake hachati wala hapigiwi na wala nini, kaibwaga tu kwenye kikoba. Kwa mtoto wa kike kwa mida kama hii kusafiri lazima uulizwe ulizwe na ndugu au mchumba wako au mumeo kuwa umefika wapi kwasababu ni safari ya usiku sana lakini kwa huyu ni kimya kimya.
Ukimuuliza swali lolote anajibu kwa haraka sana halafu lazima aulize swali hilo hilo kwangu kwamba na wewe je. Morogoro tutaingia usiku sana kwanzia saa nane sasa kama ni kweli sio jamii ya binadamu nitamkacha vipi? Maana kama hana nia nzuri basi hata nikichukua pikipiki itakuwa bado sio salama kwangu.