Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Safi braza.... Dawa ya mjinga ni kuumia tu.

Aliyepotea mpoteze zaid asirudi teena.

Unatoa sadaka 75 unakuja kuomba ushauri... Akamuombe askofu wa jimbo anayempa ulaji.
Kwani ameandika kwamba hiyo sadaka anapeleka kanisani???
 
Daaahh, na mimi nimechoma 156,900/= kuanzia tarehe 1/6/2019 hadi 8/6/2019.

Kucontrol matumizi huku ukiminimize inahitaji umakini sana
Oa mkuu tena uoe mwanamke mkuda ambae hana matumizi makubwa ya pesa akusaidie kucontrol matumizi ya pesa...... Naona wewe mwenyewe umeshindwa
 
Mmmmmh unamshauri ale bora liende
 
Ongeza sadaka, ratio ya sadaka na take home yako ni ndogo mnoo

Msisitizo usiache kutoa katika vile ulivojaaliwa hata kama ni kidogo Mungu nae mpe fungu lake ndani ya kile alichokuruzuku

Hayo mengine chukua ushauri wa baadhi ya wachangiaji mengine changanya na yako
 
Sadaka:-
25, 000 ndo nimetoa direct
50,000 ni kwa watu wenye shida zaidi ya mimi
 
. Nilipoviona nilihisi kama budget itakua kubwa vile lakn kwa haraka haraka ni kama 160,000 . hii nikiwa na familia ntaifanyia kazi. Kwa sasa itakua nafanya uharibifu
 
Mkuu kwenye hiyo hela ya ndugu unatoa kila wiki au una kituo cha kulelea yatima?

Dah! ila kiukweli tunatofautiana kwenye hiyo bajeti yako ya wiki, ongeza elfu 50 mwenzio ndio bajeti ya Mwezi na nna mke na mtoto 1.
 
Umerogwa na huyo mchungaji, yaani unampelekea 75,000/= bure.
 
Jumla?.. au tuanze kujumlisha?
 
hiyo bajeti haina uhalisia kama haina maji inamaana wiki nzima hukunywa maji? vifurushi vya cm n.k, sijaona hata umehonga wala pombe haipo
 
hiyo bajeti haina uhalisia kama haina maji inamaana wiki nzima hukunywa maji? vifurushi vya cm n.k, sijaona hata umehonga wala pombe haipo
mkuu hii bajeti ni wiki moja kma nilivyo specify , cm bando hua naunga la mwez, maji na umeme vipo ndo maana.

Sinywi pombe ,sivuti sigara na nimesema kua nipo single ( sina demu)
 
Mkuu kwenye hiyo hela ya ndugu unatoa kila wiki au una kituo cha kulelea yatima?
Dah! ila kiukweli tunatofautiana kwenye hiyo bajeti yako ya wiki, ongeza elfu 50 mwenzio ndio bajeti ya Mwezi na nna mke na mtoto 1.
ndo mana nikaona nijitafakari, ahsante mkuu
 
Hiyo bajeti ni kubwa mno unaweza ukaishi kwa bajeti ndogo tu na wewe ukawa na maisha mazuri tu poromoa hiyo bajetibyote ukija hapa isizidi laki moja kwa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…