Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

hivi tango sio tunda !???

Anyway, ongezea na maji ya kunywa 97,000 na juice 89,000 , pia kuweka bajeti ya nguo bila viatu sio poa, vuta hata sneaker moja ya 73,000
Hahahahahaha huna nia njema na mwenzio
 
Hayo matumizi mbona yapo juu sana mkuu, unataka ununue vitu vyote kama unaishi na demu babu.

Deile nunua visamaki vya buku vile au misumari (dagaa), nyanya. Monthly nunua kitunguu, mafuta na unga wa ugali tu. Hivyo ndio masela tunavyoishi!

Sasa we unataka ununue hadi hoho,binzari, letuce,gilgilani magetoni!? Utakwama tu!!!
Huyu jamaa kanishangaza kweli yani
 
Anataka apike "Ratatouille"
Hayo matumizi mbona yapo juu sana mkuu, unataka ununue vitu vyote kama unaishi na demu babu.

Deile nunua visamaki vya buku vile au misumari (dagaa), nyanya. Monthly nunua kitunguu, mafuta na unga wa ugali tu. Hivyo ndio masela tunavyoishi!

Sasa we unataka ununue hadi hoho,binzari, letuce,gilgilani magetoni!? Utakwama tu!!!
 
Harafu jamaa wali hali na maji hana mpango nayo, maharage hapendi kabisaa,
 
hunywi pombe, huvuti sigara, huna demu. ww ni mtoto wa Yesu hakika
nilikua nae mkuu akanitenda vibaya sana,

Nikawa kila nikikaa nikikumbuka alichonifanyia nacheka ata mbele za watu, kuna uzi niliandika.

Alinidanganya sana. Tangu apo sijataka nitena shida, nashukuru Mungu now nimemsahau. Bwana ananipigania na niko na furaha
 
Aisee bro;
Umeme 40000 kwa mwezi
Maji 30000 kwa mwezi
Mikate 40000 kwa mwezi
Sukari 56000(25kgs)
Cooking oil 30000 (sunflower 10lts)
Blue band 8000 (2kgs)
Sabuni ya unga 14000 (3.5kgs)
Sabuni ya mche 29000
Nishati mkaa 60000
Nishati gas 54000
Chumvi 2000
Mboga za majani mix 15000
Matunda mix 30000
Kingamuzi/cable 15000
Sadaka Mimi 20000
Sadaka wife 20000
Sadaka watoto 5 25000
Sadaka dada 6000
Nguo za watoto 1000000 mwaka
Viatu 600000 mwaka
Mavazi mke 500000 mwaka
Mavazi mimi 200000 mwaka
Matibabu mtoto 1 tu 50400 bimabinafsi wengine bima ya kazini
Karo mtoto kwanza 1900000
Karo mtoto pili 1115000
Karo mtoto tatu 800000
Karo mtoto nne 800000
Mtoto tano 000000
Fuel 200000 (kwa mwezi
Mshahara wa Dada 50000
Tunamhudumia Dada kila kitu Matibabu,nauli zake, sadaka,Pads na nguo
HIYO BRO NDO BUDGET YANGU Tena kwa uchache sana kumbuka mimi ni muumini mzuri wa castle lager kwa wastani 5beers kwa siku mambo ya kidinda Konyagi ya Kati 8000 inanuhusu au kale kadogo 4000
Pia kutimoto mara moja moja kwa familia ni lazima,siku ya kutoka out mara kwa mara jumapili hasa sehemu zenye michezo ya watoto
Nb:mke ni mjasiliamali mdogomdogo pia nina nyumba mbili za ziada napangisha 8000000 zote pamoja kwa mwaka tuna kitexie angalau kinalaza 20000 kwa siku. Mshahara baada ya makato 1.5 but bado kuna extra allowances.
Mkuu hii ni heavyweight kabisa. More than 15M per year si mchezo kabisa anyway kama inapatikana pesa kwanini isitumike? If you earn spend!
 
Asante bro nami uwa najiuliza sijui ingekuwaje kama ningelioa kabla sijajenga anyway uwa nafurahi kuwaona wanangu wakiwa na furaha siku zote ila siku ukiwa na familia jifunze kununua mazagazaga ya home kwako kwa whole sales make hivi vitu vya rejareja sijui kilo mbili za mchele nk zinaumiza sana japo pia inategemea na aina ya mke ulienae na binti wa kazi make kuna wanawake ambao kadri unavununua vitu kwa jumla ndivo pia wanavokuwa na matumizi ya vyakula hovyo,siku ukianza kuona mbwa koko kwenye jalala lako home chukua hatua jua wameanza uharabifu wa chakula.
Raha ya kununua kwa wholesale unapata hata angalau ka muda ka kunywa castle baridi bila mawazo.
But sukari au mkate umeisha castle utakuwa unaubaka moyo wako kwa mawazo
kwa maisha ya kitanzania wewe ni mtu mwenye uwezo 😊😊😊
 
Hata vitu vingine nimesahau
Mchele kutokana na ukubwa wa familia yangu uwa najitahidi kuweka magunia 6 mpunga ndani kila mwaka wa msimu wa mpunga ambapo gunia moja halizidi 40000
Pia naweka gunia moja la mahindi
Maharage gunia moja
Dagaa hata nusu debe kwa mwezi.
So nyama tunatumia 1kg siku ikisukumwa na mboga za majani na dagaa
Samaki ni mlo mbadala wa nyama samaki 40000 wanatutosha kwa mwezi.
Bro bado hapa kuna kusaidia ndugu na marafiki.

Nb hakuna nililofake katika matumizi haya ila kuna vitu vingi nitakuwa nimesahau.
Naomba pia ushauri japo mie naona sina namna ya kukwepa majukumu haya kwa familia yangu pendwa
Nachokiona mkuu ni kwamba bajet yako ungeweza kuminimize katika baadhi ya Mambo

Mfano mafuta ya gari 200k kwa mwezi hii kubwa(km aina ya gari unotumia haili sana wese) punguza ruti za ziada kwa gari zaidi ya kazini.

Sadaka pia naona kubwa 69,000 (ingawa hapa sijaelewa ni kwa mwezi au kwa wiki) lkn fanya kuminimize kdg walau iwe ½yake

Ges 56,000 hii pia inachanganya kdg. Ni mtungi upi mdg au mkubwa? Nakushauri tafuta ges mtungi wa kati ule ukishajaza tu miezi 2-3 ndo unaisha

NB:- Ingawa wakt mwingine kupunguza bajet siyo soln bali kuongeza kipato ndy best soln.
 
Yeah,true ndo maana uwa sipendagi kupiga hesabu ya hizi vitu kwani unaweza kukufuru na kuiona familia imekunyima utajiri kwa muda mrefu kumbe ni haki yao kuwahudumia mpk wajitegemee,sijawahi kuijutia hali hii kwani ni katka kuwajibu wa kwanini uliwaleta kwa dunia halafu uwatese kisa unataka kumiliki magorofa/ma lodges.
Halafu cha ajabu ukiamua kusave pesa kwa kujinyima na kuipunja familia hiyo pesa haikusanyiki maisha [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Mkuu hii ni heavyweight kabisa. More than 15M per year si mchezo kabisa anyway kama inapatikana pesa kwanini isitumike? If you earn spend!
 
Back
Top Bottom