Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Nipo single, haya ni Matumizi yangu ya wiki moja - nipe ushauri

Hiyo sadaka unaitoa kanisani au kuhonga?
 
Eti tango sio Tunda teh teh , ongeza sadaka mkuu
 
Hayo matumizi mbona yapo juu sana mkuu, unataka ununue vitu vyote kama unaishi na demu babu.

Deile nunua visamaki vya buku vile au misumari (dagaa), nyanya. Monthly nunua kitunguu, mafuta na unga wa ugali tu. Hivyo ndio masela tunavyoishi!

Sasa we unataka ununue hadi hoho,binzari, letuce,gilgilani magetoni!? Utakwama tu!!!
Mfundishe maisha huyo dogo...
 
Kwa matumizi hayo We jamaa unaonyesha utakua Tukunyema/Bongenyanya sana Maana swala la kula huna Utani nalo.

Ila hayo matumizi ni ya jamaa anae ishi na ka slay queen Geto,kama unaishi peke ako na una hayo matumizi IKO SHIDA PAHALA.

Sema nini mkuu kwa matumizi ya 200k+ kwa wiki halafu huna hata Boda boda huo ni ungurunyeee...Matumizi hayo mkuu Shkamoo

Fukuza hiyo slay queen hapo geto inaenda kukuharibia channel trust me,na uhakika hauko peke ako arif.

SEMA WADADA MUNGU ANAWAONA...haya matumizi lazima kuna kapaka make up nyuma yake sio bure.
 
Hata vitu vingine nimesahau
Mchele kutokana na ukubwa wa familia yangu uwa najitahidi kuweka magunia 6 mpunga ndani kila mwaka wa msimu wa mpunga ambapo gunia moja halizidi 40000
Pia naweka gunia moja la mahindi
Maharage gunia moja
Dagaa hata nusu debe kwa mwezi.
So nyama tunatumia 1kg siku ikisukumwa na mboga za majani na dagaa
Samaki ni mlo mbadala wa nyama samaki 40000 wanatutosha kwa mwezi.
Bro bado hapa kuna kusaidia ndugu na marafiki.

Nb hakuna nililofake katika matumizi haya ila kuna vitu vingi nitakuwa nimesahau.
Naomba pia ushauri japo mie naona sina namna ya kukwepa majukumu haya kwa familia yangu pendwa
Sikuona akiba mkuu
 
Nachokiona mkuu ni kwamba bajet yako ungeweza kuminimize katika baadhi ya Mambo

Mfano mafuta ya gari 200k kwa mwezi hii kubwa(km aina ya gari unotumia haili sana wese) punguza ruti za ziada kwa gari zaidi ya kazini.

Sadaka pia naona kubwa 69,000 (ingawa hapa sijaelewa ni kwa mwezi au kwa wiki) lkn fanya kuminimize kdg walau iwe ½yake

Ges 56,000 hii pia inachanganya kdg. Ni mtungi upi mdg au mkubwa? Nakushauri tafuta ges mtungi wa kati ule ukishajaza tu miezi 2-3 ndo unaisha

NB:- Ingawa wakt mwingine kupunguza bajet siyo soln bali kuongeza kipato ndy best soln.

Nashukuru kwa ushauri wa gari nadhan cc ya inanitesa juu ya ulaji gari ni 6cyclinder na ina cc 2194 route zake ni kazini asubuhi na kurudi home jioni wakati huo asubuhi nampitisha wife kijiweni kwake na jioni ananisubiri tunarudi wote home so mafuta ni Yale Yale,pia tunaitumia kwenda kanisani tu sinaga mizungunguko tofauti na hilo labda kwa nadra sana km hospital, mtoto kuchelewa gari la shule na kuwapeleka watoto Jumapili out kidogo sehemu za michezo.so gari inakula karibu fuel ya 10000 kila siku.
Kuhusu gas ni 15kg ambao sisi tunaujaza kwa 54000 kuna kipindi unaweza kusukuma mwezi 1.5 na itategemea na matumizi ya mkaa,means mkaa ukutumika sana gas haitumiki sana.
Yaani kwenye sadaka mimi natoa 5000 kila jumapili ×4 =20000 + wife 20000=40000
Watoto 1000@1×5=5000×4=20000.
Kumbuka hiyo 5000 inakuwa imegawanywa km 3/4 kimatoleo mimi ni KKKT Kuna sadaka ya Ahadi
Kuna sadaka ya Jengo
Kuna sadaka Utumishi
Kuna sadaka ya shukran ya wiki
Kuna sadaka ya 1/10 hii inategemea na unavoousikia moyo wako kutoa
Pia kumbuka hizo sadaka za mwanzo zina bahasha maalum na kumbukumku utunzwa,so unaona elfu 5000 ninavoigawa ha pa kupunguza hakuna
Anyway asante kwa ushauri make hapa tunashare experience.
Note;Mimi sio muumin wa michango ya harusi na ukinikaribisha hata kwa bure siji labda tuwe tumeshibana sana
Note:Sinywagi pombe za magroup wewe ukikuta bar nakunywa ukanizungushia sitakurudishia kusudi time husiangaike nami.Nikitoka home na ten ya kunywa hiyo inanitosha nikiona siku nina hamu ya kuchangamka nitajiLusekelo siku hiyo.
Note:Sinaga tabia ya kuhonga wanawake mimi ni binadamu mambo yakiwa hapa nitamtafuta rafiki roho inataka nitakunywa nae kama ni mnywaji na chakula kizuri tutakula na nitajitahid kufanya performance nzuri kwa bed km rafiki but kamwe hasitegemee hata mia kutoka kwangu,wanatokaga kwangu wamenuna but baada ya muda wananitafuta tena urafiki unaendelea.
Mara nyingi uwa nawatafuta waelewa ambae leo akinywa yako kesho nakunywa yako tofauti na hapo sinaga haraka na hawa malaika hasa wasiojitambua
×××hizo ndizo kasoro zangu km binadamu wa kiume×××
Halafu siamin ktk kukopeshana ukija kwangu unataka 100000 ya mkopo ujue nitakupa 30000 ya bure na sitakwambia ni ya bure kusudi ukinidhulumu roho isiniume pia sitaki kumpoteza mdeni wangu, so ni nimpe kidogo kusudi akae na kihoro yeye wakati mimi nina amani
 
Hahahaha,man akiba ni muhimu sana ukisha kuwa na hawa raia wa Mungu husifanye kosa la kutokuwa akiba na bank na nyumbani kwa dharula ni makini man na hilo zamani kidogo kuna dogo alizingua usiku akameza coin ikakaba koo usiku na sikuwa na mia ndani,gari mafuta yalikuwa kiduchu sana sitarudia kufanya makosa km kamwe,akiba ni muhimu ila naomba niache kapuni.
Pia nina uzoefu wa kucheza na hisa!Please nakushauri km unaweza penda kucheza/kuwezekeza kwenye hisa,nina hisa kidogo CRDB but gawio kila mwaka si haba ndugu yangu na rahisi kucheza.
But Angalia makampuni yaliyosimama fresh mf TBL,CRDB,TWIGA CEMENT nk fatilia na fanya utanikumbuka ni zaidi ya kujenga nyumba za kupanga but inategemea na uelewa wa mtu na kuchangamkia fursa, karibu sana
Sikuona akiba mkuu
 
Hakuna kitu kinaniumaga kama kwenda kujikamua kwa demu aliekula pesa yangu kwa kweli sipendi kuhonga uwa namtafuta mwelewa ambae yeye anajielewa ni heri anywe na ale kwa tani yake but hasiniombe pesa ya kupanda kifuani,ikiwa hivi napoteza mzuka nabaki kujinywea,ndivo nilivo
We mbona sioni yakuhonga hapo?week nzima huja honga?
 
Back
Top Bottom