sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni kweli Jamii forum bado inaweza kuonekana ya kawaida katika level za dunia lakini nathubutu kusema kwamba katika level zetu za hapa Africa, huu ndio mtando wenye wafuasi wengi na uliopangilika zaidi,
Najua wanaijeria wana forum yao inaitwa Nairaland.com, ni kongwe zaidi na ina members wengi lakini miundombinu yake ni hohe hahe!! huwezi hata kutafuta post kirahisi kwa title, huwezi kupandisha video, muziki, pdf, n.k.
Kenya Talk wamejitahidi kwenye mpangilio, kuna vitu vichache wakiongeza watakuwa sawa na jf mfano night mode, filters, n.k. Shida inakuja kwamba Kenya Talk bado members ni wachache na inapelekea michango iwe michache, kawaida sana kukuta post ina wachangiaji wasiozidi hata 10, nadhani hii ni sababu ya ugeni wake ilianzishwa mwaka 2014 wakati ambao tayari wakenya wameshazoea facebook, Ni tofauti na Jamii forums ilianza zamani miaka ya 2006
Nchi za subsaharan Africa ni hizi zetu nje ya mataifa yaliyojaa waarabu wa huko kaskazini kama Misri, Moroco, Algeria, n.k