Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Hapo wanakufukuza kijanja.. Hawataki kukuona na inawezekana unalala sebuleni au nawatoto..
Wala hawamfukuzi tatizo mazoea,mm mwenyew alishakujaga mdogo wangu kutoka kijijini,asubuhi ilivyofika nikaenda kuchukua mkate,basi yule ndugu yangu alimishangaa Sana mkate tule wawili.

Ikabidi ule mkate nimwachie nikanunue maandaz kwa ajiri yangu,aisee alinifutia wote[emoji3][emoji2]
 
Sio b



Kula kidogo haiusiani na budget Sio budget Matumbo ya watu wa mjini yameshazoea portion ndogo Nyie wa mikoani ugali kilo moja unataka ule peko yako ni tumbo la kibinadamu ni pipa

Mbona mkija vijijin mnakula sanaa
 
Sio uchoyo kwa mtu anayejitambua huwezi enda ishi kwa mtu labda muwe ndugu wa damu

Ndugu hao ndio
Kuna familia unaenda unajua kabisa ni hawana uwezo unanunua mboga na vitu vingine unawapelekea na ukifika wanapika kilichopo na ulicholeta wanatenga mezani au kwenye mkeka na hawabanii sasa unakuta watu wana uwezo lakin wachoyoo
 
Hao chakula ni cha shida na wana roho za kimasikini
 
Ndugu hao ndio
Kuna familia unaenda unajua kabisa ni hawana uwezo unanunua mboga na vitu vingine unawapelekea na ukifika wanapika kilichopo na ulicholeta wanatenga mezani au kwenye mkeka na hawabanii sasa unakuta watu wana uwezo lakin wachoyoo
Mi naenda kwa watu kuanzia saa 9 mchana, maana nina hakika washakula, naondoka kabla ya 12
 
Napigia mstari HAO NI WACHOYO.
 
Hata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.

Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.

Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.

Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.
 
Mimi nikienda ugenini popote pale iwe mkoani au mjini kwa ndugu lazima ninunue kiloba cha unga, au dumu Zima Lita 5 za mafuta ya kula na mchele kilo 20, nitakaa kidogo then naondoka...

Pia uwa ninatabia ya kutembeatembea kupata chochote kitu migahawani ili nisiwakele wenyeji wangu kwenye kuongeza ongeza msosi.
 
duh kweli.sisi hatuna uchoyo sababu ya mama katufunza kuishi na watu
 
Pole sana binti kwa kukumbukia nyakati hizo za maisha. Mshukuru Mungu aliruhusu hilo litokee kwa wakati wake. Kamwe usiache mafundisho hayo ng'wanike
 
Naona mme-base kwenye chakula tu.. Hamsemi issue ya choo pa kuweka n'nyaaa.

Me nilienda kwa sister angu wa hiari tu aliinita, nilikaa kama wiki hivi, tatizo unakula vizuri chakula cha kutosha kitamu.. Issue choo???

Sasa choo cha kukaa, ukishusha mzigo uflash maji hayatoki basi shida tupu inabidi uende na ndoo kubwa ya maji ili ukimaliza uflash mzigo uendee, Na ubaya mdada wa kazi anajua issue nzima hasemi kama kuna shida, mwenzangu haja anamalizia chooni cha boss wake.

Nakumbuka siku niliyoondoka nilijikaza mpaka kufika home saa 2 Usiku nilipitiliza chooni maana unabana n'nyaaa mpaka unajutraaaa..
 
Luckyline umekulia familia ambazo chakula kingi na ni kitu cha kawaida so huwezi kuwa mchoyo, wachoyo wengi wamekulia familia ambazo chakula ni kidogo na kikipikwa watoto ni kugombania kula huku manung'uniko ya Huyu anakomba yanasikika. Wasukuma wakipika chakula mgeni akala akashiba ndio furahayake, hata kama ni mpita njia utakula kwanza then ndo mtaanza kufahamiana, ugali unatengwa kwenye sufuria wa moto balaa nilishindwa kula nikawa napuliza tonge basi hadi vitoto vinanishangaa eti naungua, ugali haujaisha unaletwa mwingine aise wasukuma wanakula balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…