Hata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.
Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.
Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.
Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.