Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Kuna mwaka nilisafiri na treni kutoka Mwanza-Dar. Kufika sehemu kuna jamaa alipakia magunia ya karanga akayaweka kwenye korido ya kwenda chooni. Tukafika ktk kituo kimoja mjamaa alinunua mihogo ya kuchemsha aisee ilikuwa mihogo mingi sana na kachumbali juu, nikawa najuiliza huyu jamaa ataimaliza kweli hiyo mihogo. Aisee nilishangaa sana na nikaamini kuna watu wanakula sana yaani ni ngumu kuamini
Dah[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru Wadau kwa michango yenu

Ila nipo mtwara ndani ndani , kwanza ni kijijin hakuna gest kbsa,Cha pili migahawa imefungwa maana wengi hapa wamefunga si mnajua huu mwezi wa Ramadhani,
Pale sokon Kuna watu jion wanauza uji na ftali ,
Ila apo wanapo uza Kuna duka la dawa la huyu dada nilipofikia na anauza mdogo wake , Jana nimeenda nikaona nikinywa uji dogo atakuja kuchoma nikala chungwa moja,
Daah yan
Umeyakanyaga mzee[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo imenikutaga aisee, nilienda kwa jamaa alikomalia kweli nistay kwao kipindi nafuatilia mambo flani hv mkoa ule, sasa chakula daah ani inabidi nile taratibu ili tuondoke wote mezani, na pia ni kiduchu yani kale kaugali daaah!![emoji29] nilikua nakaza moyo sana[emoji28]

Sasa ajabu zaidi ikitokea nimetoka misere na mwana tukiingia mahali kula alikua analalamika kwann nisile kutosha home na wakati kinachotengwa ni kidogo sana pale mezani

Aisee alipokuja mkoani kwangu, nyumbani alijishtukia mwenyewe[emoji28] maana ile msosi najipigilia mezani ni ya kufa mtu, akaanza kusema daah inawezekana kule ulikua hushibi kaka, nisamehe bure, nikawa namvungia tu namwambia amna nimeanza speed ya kula karibuni tu, ila kiuhalisia nilikua nasongolewa na njaa mpaka nakula mgahawani

Mimi nafikiri mgeni akija hebu chakula kipikwe cha kutosha siku za mwanzoni then angalia speed yake ya kula unamkadiria kama ni mlaji unaenda nae sawa na kama sio mlaji unapunguza kipimo cha diko ili kuepuka uharibifu ila ni vizuri kumkarimu mtu chakula afurahie aisee....

Naam kaka
Umenifundisha kitu
Ahsante
 
Beautiful- ukarimu...... Ni mbaya sana kumnyima mtu chakula au maji ya kunywa.
Wakati mwingine uchoyo ni namna mtu alivyolelewa au pengine umelelewa vizuri tu bila choyo ila unakuta ni hulka ya mtu yaani choyo ipo ndani yake mtu na hawezi kubadilika.
Sawa sawa nimelishwa mpaka nimeongezeka uzito.
 
Luckyline umekulia familia ambazo chakula kingi na ni kitu cha kawaida so huwezi kuwa mchoyo, wachoyo wengi wamekulia familia ambazo chakula ni kidogo na kikipikwa watoto ni kugombania kula huku manung'uniko ya Huyu anakomba yanasikika. Wasukuma wakipika chakula mgeni akala akashiba ndio furahayake, hata kama ni mpita njia utakula kwanza then ndo mtaanza kufahamiana, ugali unatengwa kwenye sufuria wa moto balaa nilishindwa kula nikawa napuliza tonge basi hadi vitoto vinanishangaa eti naungua, ugali haujaisha unaletwa mwingine aise wasukuma wanakula balaa.
Wasukuma sio wachoyo unakula na kushindwa mwenyewe uko sahihi
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.

Dar kuna shida mno aisee!
Wanapika chakula kidogo mno,chakula cha kula mtu mmoja Kyela hapo Dar wanakula family wa watu wazima wanne.
Nn shida?
 
mbaya zaidi kinatengwa mezani kwa stail ya self service, mgeni unakaribishwa 'karibu uendelee hapa kila mtu anakula kwa muda wake'. Ukisogea mezani ukafungua hotpot unakutana na ugali kama ngumi.
 
Mwaka jana kuna project nilienda kufanya mkoa fulani hivi ya kama wik mbili nilipofika nikapokelewa na mwenyeji wangu. Basi baada ya stori mbili tatu nikamwambia anipeleke Lodge nzuri. Jamaa akaniambia Lodge ya nini wakati home kwake kuna chumba cha wageni. Nikakataa lkn jamaa akasisitiza niende nikaona isiwe case. Nikajiongeza tukapitia kwa mangi nikafungasha haswa vitu vya ndani mamichele,unga wa ngano mafuta,tambi na mazaga zaga kibao nikamuuliza kama ana frigi akasema anayo tukapitia na buchani kununua nyama na masoseji. Basi tukafika home tukapokelewa na mke wake na watoto wake wanne wawili wa kike wawili wa kiume. Kesho yake nikaanza mishe. Yaani wale watu ni wakarimu ajabu. Shemeji kila asubuhi baada ya heavy breakfast kabla sijaondoka ananiuliza nikirudi nitapendelea kula nini,wale watoto wa kike asubuhi wananiambia niwatolee nguo chafu wafue. Mi ni Mkristo na wao ni Waislamu safi lkn awajawahi kunistrict kupiga mambo yetu yale. Tukienda bar na yule jamaa mi nakamatia vitu yeye anacharaza zake Redbull tukiondoka tunachukua nyama ya mbuzi kilo tunarudi home tunakula na familia yake fresh tuu. Siku ya kuondoka ilivyofika hakuna aliyekuwa anataka niondoke na walihuzunika sana hadi kulia. Mpaka leo ni kama ndugu zangu kabisa wananitembelea na familia yangu huwa tunafunga safari kwenda kuwatembelea. Sorry kwa uandishi mbovu.
Nice

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Hata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.

Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.

Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.

Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.
Duh mzee wako alikua mtu wa watu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Note. kabla ya kuanza kula kunywa maji kiasi.., katikati ya msosi piga maji kiasi.... mwisho piga maji ya kunywa kiasi. furahia kushiba kwako.
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Kwani vyuo na shule hamja. Fungua?
AU UME RUDISHWA ADA HUNA,
 
Eee we kiboko [emoji23][emoji23][emoji23] sasa ukienda ugenin unafanyaje?unaigiza au unakula share za watu watatu huo uroho sasa
Naogopa sana kumuongezea mtu bajeti, hivyo napendaga kufikia hotel au lodge na nikienda kusalimia ndugu ni ile mida ya SAA Tisa hadi 11 naondoka so tutapata vinywaji tu ambavyo pia nitagharamia kwa kisingizio cha kuwanunulia watoto na watu wengine ninaowakuta hapo.nilianza kujitegemea toka nikiwa darasa la sita so siwezi kuishi kwa mtu hata ssiku moja, mahali ninapokua comfortable ni kwa bi mkubwa tu ambaye anajua nature yangu ya ulaji yy hupenda kuniita simbilisi ni wanyama Fulani hv wakiingia shambani ni hatari.
 
😂😂😂😂 na hunenepi ajabu sana
 
Back
Top Bottom