EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 10,576
- 16,644
Nilikuja kuuguza wiki 3 nzima nilikuwa kwao unaweza kukaa gesti wiki 3 mzee?,kingine ilikuwa inanibidi niwahi kurudi saa 1 niwe nimerudi nilikuwa najistukia ila siku nyingine nilikuwa naishi maisha yangu halisi narudi saa 4 au 5 nakuta wameshalala chakula wamenitengea mezaniNdo siku nyingine uende guest au hotel
[emoji3][emoji3][emoji3] ungerudi kwako model mkeo angekushangaa nakuuliza Mme wangu umetoka jela?Kama kawa. Hakika ningejifanya mstaarabu na kuiga ulaji wao ningekonda walahi maana tulikuwa nao Kwa miezi mitatu. [emoji23]
Mama ana Roho ya utakatifu kabisa. Naambieni wazazi Wetu, bibi na Babu wa ZETU ni watakatifu maana walikuwa na ukarimu mkubwa sana. Walitunza misitu, wakapata Mvua nyingi na kulima mazao Kwa wingi hivyo kuwa na chakula Cha kutosha. Ila sikuhizi tunaiga uzungu kuliko kawaida, tumekata misitu, Mvua tabu, mazoa Kidogo. Sasa chakula tunakula Kwa kujilamba tu. [emoji120][emoji120][emoji120]
Asee hii Kali, we mwanang sikuwezDah mimi nimeshakataa kukaa nyumba ya mtu ugenini,unateseka msosi hushibi nilishawahi dakwa jikoni nadokoa chakula asubuhi asubuhi njaa kali[emoji3][emoji3][emoji3],yaani jamaa hawali kabisa,ka ugali kadogo
Nikaona hapa nateseka nikawa naenda kula mtaani khaaa.
Kukaa kwa watu ni taabu
acha kabisa tena na msimu huu wa mahindi na maboga ni mwendo wa kukandamiza kijijiniBora wewe umekata nusu,ningekua mimi ningekula wote,wao si ndio wenyeji wangeenda jikoni kupika tena,sio kula kama unaonja,kwanza huku kijijini kabla ya chakula tunaanza na karanga mara maziwa na manumbu mpka chakula kinakuja mtu ushaanza kushiba,
umenikumbusha mbali kidogo wakati Niko ugenini halafu nakula mpepe a. k. a bangi nilitandika chupa ndogo ya chai na chapati sita kumbe ndo kifungua kinywa cha familia yote [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
aisee acha tu kipindi nasoma chuo nilikaa kwa mpare moja nilijutaYaan ni kweli kabisa ,kuna familia watu ni wachoyo mnatafuta pesa za nin mnakula hata hamshibi [emoji23][emoji23] raha ya chakula kiliwe kibaki ukiona watu wanakula chakula kinaisha hakibaki ujue watu hawashibi
Huu ugeni jamani,
Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.
Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.
Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.
Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.
Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!
Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Chief zunguka zunguka huwezi kukosa chimbo la misosiNashukuru Wadau kwa michango yenu
Ila nipo mtwara ndani ndani , kwanza ni kijijin hakuna gest kbsa,Cha pili migahawa imefungwa maana wengi hapa wamefunga si mnajua huu mwezi wa Ramadhani,
Pale sokon Kuna watu jion wanauza uji na ftali ,
Ila apo wanapo uza Kuna duka la dawa la huyu dada nilipofikia na anauza mdogo wake , Jana nimeenda nikaona nikinywa uji dogo atakuja kuchoma nikala chungwa moja,
Daah yan
SawaTumeiga uzungu gani acha kuwa mjinga
Uliona mzungu anaishi sehem isiyo na msitu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3] ungerudi kwako model mkeo angekushangaa nakuuliza Mme wangu umetoka jela?
Sent using Jamii Forums mobile app
We ni mhaya tabia zenu tunazijua hasa linapokuja suala la msosi.Kula kutokana na Kazi yako sio upo tu nyumbani hautoki unataka kula nusu ya Ugali mtu mmoja ni hatari kwa Afya binafsi Mimi sioni Kama chakula ni kidogo isipokuwa naona unataka kuforce kula Sana Kama mtu anayebeba zege .
Sio kweli MkuuWe ni mhaya tabia zenu tunazijua hasa linapokuja suala la msosi.
Au jioni ile muda wa futari unaagiza vikombe viwili vya uji cha kwako na cha dada wa dukani...Pole, kumbe Bado upo ugenini Hadi sasa. Kwa mazingira hayo vumilia tu. Ila kama utakaa kitambo Kidogo tafuta rafiki fasta ili uwenae matembezi mida Fulani hivi, kwa strategy hii atakuonyesha kijiwe poa tu.
R.i.pHata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.
Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.
Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.
Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.
Nia gan walikua nayo hao aseeHii familia ya mang'ati? Pia inawezekana upo single mkuu alafu ulipoenda Kuna mabinti single [emoji23][emoji23][emoji23]. Maana hii iliwahi nikuta Mimi miaka ya 2007/2008, nilipanga mahali alafu nipo single na kunabinti pale mtoto wa mwenyenyumba asee wakichinja kuku, nusu nzima nakula Mimi. Baadae wakaniamishia chumba kubwa kwenye Nyumba Yao ya familia alooo! Nilifaidi sana na Nia Yao niliing'amua lakini nikatulia tu na kuendelea kula misosi.