Duh mzee wako alikua mtu wa watu
Sent from my SM-A115F using
JamiiForums mobile app
Alikufa at age of 30 yrs can you imegine.
Si unajua mtu akifa gafla maneno mengi lazima yatoke nani kasababisha?
Ilikuwa 1993 baba alikuwa akimsomesha sekondari bint wa bibi mmoja.
Siku mbili kabla ya kifo chake huyo bibi alikuja nyumbani akakuta baba yuko holi akaanza kulia nini kimempata mtoto wangu?
Huyo bibi alivyotoka analia akasikia umbea kuwa fulani wenda kafanya kitu.
Huyo bibi wakati huo alikuwa mmama wa makamo, mimi nilikuwa mdogo ila hiyo kumbukumbu ninayo.
Bibi huyo niliona kavua ndala kakimbia peku akielekea kwa huyo mtu walokuwa wakimsema wenda kafanya jambo baya kwa baba.
Alivyofika kwa huyo mtu nasikia alitembea na magoti akimuomba kama kafanya chochote basi asemè anataka nini. Nasikia huyo mtu akajibiwa bora akipelekwa hospital arudi jeneza na wengine tuwe na maisha mazuri.
Bibi huyo alirudi nyumbani analia akasema kama kuna mkono wa binadamu kwa mwanangu huyo mtu nishuhudie akimfata mwanangu. Nadhani huyo bibi alijuwa lazima baba afe.
Baba akapelekwa hospital j2.
Haya yote yanatokea mama alikuwa kaenda kujifungua......
Baba alikuwa amemsomesha kaka fulani hivi ana exposure ya kwenda hata sehem x, mbali kweliii alivyoona hali inakuwa mbaya ikabidi aandike barua amtume huyo kaka amwambie mama awahi. Usafiri zamani ulikuwa wa shida sana.
Huyo kaka alivyofika akakuta mama kajifungua mtoto wa kiume, akarudisha taarifa kuwa mama kajifungua atakuja alihamisi.
Juma nne huyo kaka akarudisha majibu kuwa mama kajifungua mtoto wa kiume atakuja alhamisi.
Baba akasema neno la mwisho " nimekufa bila kumuona mwanangu wa kifume" na dk hiyo akafariki.
Kweli mama anafika siku hiyo ya alhamisi analeta mtoto hajui habari za msiba wamesubiri wapi anakuta tunazika. Iliuma vibaya mno. Naikimbuka hiyo siku ila nilikuwa mdogo sikujua kuwa hatorudi.
Mtuhumiwa mauti nae yamemkuta mwaka jana baada ya miaka 29 ila yeye amedumu. Ameona wajukuu zake baba yangu hakuona kitu.
Mtuhumiwa siku alipo kufa, yule bibi aliyeenda kumuoma kama kafanya kitu arudishe moyo baba apone, bibi alivyosikia kifo cha mtuhumiwa wa kifo cha baba, alilia akasema fulani uliniulia mwanangu ukijua Mungu hakuoni? hayo ni malipo yako.
Maskini huyo bibi hata hamzai baba yangu sema tu alimsomeshea binti yake na huyo binti kwa sasa ni mwalimu mkuu.
Fatilia hata kwenu, watu wema wanaosaidia jamii hawawezi ishi muda mrefu. Akiishi sana miaka 50.