Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Sijawahi ona hiyo ya chakula kinatolewa kwa uchache kiasi hicho
Imagine mtu anaenda kununua nyanya mbili, kitunguu kimoja, mafuta ya jero, hoho moja, karoti moja, dagaa wa buku na unga nusu na robo.

Unadhani kuna nini hapo? Hongera mkuu kama hujawahi ona au kuishi namna hiyo.
 
Aisee hii iliwahi kunikuta kota za maafisa wa polisi Nyamkazi Bukoba ile familia ilikuwa inapika chakula kidogo sana nakula sishibi alafu ukimaliza kula unapewa maji ya bariiiidi sasa njaayake usipime ,jicho linanitoka kila nkitaka kutoroka nkale mgahawani watoto wa pale wananifata naishia kuzunguka nao na kurudi,,,nilivyorudi nyumbani nikaulizwa unaumwa nikasema hapana,,ila nikawa nakula kuliko kawaida mzee akasema huyu alikuwa na njaa ikabidi nisimulie,,,maisha ya mjini ni ya kipumbavu mno unakuwa jehanamu kabla hujafa!!
 
Chief mimi naona Uliishiwa mbinu ya kuwatoroka hao watoto
Au uchumi haukua vzuri
 
Kila mtu kakomaa mjini bajeti mjini bajeti.

Huo ni mji gani wa kuishi kama huwezi mudu chakula?
Shida mzee watu wanaforce kuishi mjini ebu fikirikia mtu mzima na akili zake anakunywa juisi ya u-fresh ya sh 100 au 200 wakati anaweza kupata juice nzuri kwa sh 500.
 
Shida mzee watu wanaforce kuishi mjini ebu fikirikia mtu mzima na akili zake anakunywa juisi ya u-fresh ya sh 100 au 200 wakati anaweza kupata juice nzuri kwa sh 500.
Nilivyofika mwanza mjini kwa mara ya kwanza nilishangaa kwenye vtuo vingi vya daladala wanauza maji ya kunywa shilingi100 tena yanakua ya baridi kwelii
 
Halaf sio kwamba wao wanakula kidogo hapana huko wanapotoka makazini kwao wanakula wanashiba wakifika home wanajazilizia kidogo
Watu wa hivyo siku wakija kwenu wapikie chakula kingi na kizurii wale sana
Solution ni kuacha kufikia kwa watu. Kwanza kufikia kwa watu unabadili utaratibu wao wa maisha. Ni heri upange ratiba zako ufikie lodge ufante yako usepe
 
Dah poleni sana,sijui kwanini watu wanachuki namna hii inatisha sana

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Nampenda sana mtu, muwazi, mfano hapo ulipokuwa unaishi, mko watu 4, hapo unamwambia shemeji yako!!!

Shem !! Ongeza kipimo, mm mchoma mkaa napiga msosi!! kesho shem , ntakuonesha utaalamu wangu.

kisha Mtonye mshikaji, kesho naingia jikoni mwenyewe nitoe NGUNA ya wachimba mkaa maana binafsi sishibi.

Mchana rudi mapema ukiwa na vifaa JIKO, Usitegemee unga wao, mboga yao na viungo vyao. Ikiwezekana leta vya kutosha.

Siku moja, shemeji yangu alinifurahisha sana, tulikuwa tupo wawili nyumbani, yy akaniambia leo tupike UGALI, nikamwambia poa.

Sasa mm si najua utakuwa ni mdogo tu wa kishkaji !! Akaniambia shem sufuria iko wapi?
Nikamuonesha ,akasema hiyo ndogo shem mm NIMEZOEA kula mara 3, hii haitoshi .

Nilicheka kwa furaha sana kwa ule UKWELI wake, maana mm ni mvivu wa kula na haswa nikiwa peke yangu. Hivyo Angeleta WOGA na kufuata tabia zangu Angekuwa anaumia na njaa BUREEEE.

HAO jamaa zako , yawezekana mfumo wao ni kila mtu anapojihangaikia anakula kabisa jioni ni pashapasha wakati Mwenzangu unajua nyumbani ndo kila kitu.
 
Si ungeenda tu kula na watoto mkuu[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Ila kuna familia zina wanawake wana roho ambayo haielezeki
Kuna mpangaji mwenzangu nilisikia anaongea na simu analalamika kuna huyo mwanamke ameolewa na ndugu yao kila wakienda kumsalimia anawapikia dagaa tena zile dagaa zenye mchuziii pipaa
Wanasema yani mara zote kila wakienda ilhali baba mwenye nyumba huwa ananunua nyama zikae kwenye friji na friji limejaa na nje wanafuga kuku wa nyama wengiii
...nilitamani nimpige zoezi la water therapy (unamshika kichwa unamuingiza kwenye beseni lenye maji mengi )😅😅

Sema huwa sina mazoea nae ningemuuliza Unaenda kwa ndugu kula au kusalimia
 
Hapana, hakuna anakula TOFAUT na home , hakuna migahawa kbsa ,
Sema wamezoea tu kula kdg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…