Noma sana.Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]
A wap,Kwani hawakukwambia ujisikie upo nyumbani??
Hio nyumba naijuaHuu ugeni jamani,
Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.
Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.
Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.
Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.
Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!
Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]umenikumbusha mbali kidogo wakati Niko ugenini halafu nakula mpepe a. k. a bangi nilitandika chupa ndogo ya chai na chapati sita kumbe ndo kifungua kinywa cha familia yote [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yani ni mimi kabisa hili jambo lilinikutaIla ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Niko Mbeya wala hujakoseaH
Hiyo itakuwa mbeya bila shaka
Najiuliza why me siwez kula chakula kingi hata nizilazimishe vip?
Huo sio ustaarabu kwa mgeni. Kwa kawaida sisi unapomkaribisha mgeni kula unaenda nae mezani unamfunulia mahotpot ikiwezekana unamuonesha na maji ya kunawa tena unaanza kupakua mwenyeji, hiyo inampa confidence mgeni ajikadirie yeye kulingana na mwenendo wa mwenyeji wake.Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja
Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha
Ngoja nicheke kidogo[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji1787] kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue
Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku
Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani
Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali
Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi
Inategemeana na kazi, wachana mbao, wachimbaji nkWatanzania tunapenda kula sana tena hovyo angalieni mtapata magonjwa.
Beautiful- ukarimu...... Ni mbaya sana kumnyima mtu chakula au maji ya kunywa.Kuna mahala nipo mimi ni mgeni, unakaangiwa nusu kuku na hapo wanataka ule na supu.Ukikaa kidogo wanakukaangia ndizi na perege kwa kweli nimekula.Pasaka wakataka kuniua wakanipikia machalari na minyama mikubwa kama ngumi ya mandonga.
Sijakaa vizuri wakaniletea chipsi na nyama za mbuzi za kuchoma.Hamadi wakaleta pilau mbuzi na vipande vya tikiti sijui na saladi.Nikala mpaka nikakasirika kwa furaha.Walivyo kiboko wakaniletea na supu.Mara paap bia hizi nkasema mi sinnywi bia wakaniletea soda tatu, ya mchana, ya asubuhi na ya jioni wakati wa kulala.Ratiba ya kuzinywa nilipanga mimi.
Yaani wakuu nilikuwa na uhakika wa kula nusu kuku kila siku.saa nyingine asubuhi kidari mchana Firigisi, jioni kipaja asubuhi namalizia kidari wakati mwingine.Nimekaa siku kumi na nne.Kuna kazi nilienda kuifanya kwao wameniambia nirudi tena kufanya ingine.NAONA KUCHELEWA.
SHIKAMOO WALE WATU WALIJUA KUNINYOOSHA KWA KWELI.ila mkuu pole hao watu ni wachoyo.jaiwezekani chakula ambacho hata panya hamalizi mle watu wanne.HAO NI WACHOYO.
Kusini gan yenye misosi maan npo huku 5years chakula ni shda familia zinakula milo mi2 had mmoja baada ya msimu wa koroshoAseee! Hiyo kawaida kabisa, hutokea watu wengi sana. Sisi watu wa kusini tumezoea kujaza sahani maana misosi yakutosha, hao wa Dar Wana budget Kali sana. Ila kama unamishe zako si vema sana kufikia Kwa ndugu ama jamaa, panga budget yako vema ili ufikie lodge ya Bei unayoimudu.
Walio gundua hotel/lodge sio wapuuzi. Kwa nini ufike nyumbani kwa mtu? Wakubwa wa nakutana baa bwana mdogo.Huu ugeni jamani,
Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.
Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.
Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.
Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.
Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!
Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Ni mtwara vijijini hakuna gest kbsa,Walio hotel/lodge sio wapuuzi. Kwa nini ufike nyumbani kwa mtu? Wakubwa wa nakutana baa bwana mdogo.