Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]
Noma sana.
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Hio nyumba naijua
 
umenikumbusha mbali kidogo wakati Niko ugenini halafu nakula mpepe a. k. a bangi nilitandika chupa ndogo ya chai na chapati sita kumbe ndo kifungua kinywa cha familia yote [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Yani ni mimi kabisa hili jambo lilinikuta

Niliungana nao tu alafu sijui kuomba ikabidi niwe nachezesha mdomo tu 🤣🤣
 
Kuna mahala nipo mimi ni mgeni, unakaangiwa nusu kuku na hapo wanataka ule na supu.Ukikaa kidogo wanakukaangia ndizi na perege kwa kweli nimekula.Pasaka wakataka kuniua wakanipikia machalari na minyama mikubwa kama ngumi ya mandonga.
Sijakaa vizuri wakaniletea chipsi na nyama za mbuzi za kuchoma.Hamadi wakaleta pilau mbuzi na vipande vya tikiti sijui na saladi.Nikala mpaka nikakasirika kwa furaha.Walivyo kiboko wakaniletea na supu.Mara paap bia hizi nkasema mi sinnywi bia wakaniletea soda tatu, ya mchana, ya asubuhi na ya jioni wakati wa kulala.Ratiba ya kuzinywa nilipanga mimi.
Yaani wakuu nilikuwa na uhakika wa kula nusu kuku kila siku.saa nyingine asubuhi kidari mchana Firigisi, jioni kipaja asubuhi namalizia kidari wakati mwingine.Nimekaa siku kumi na nne.Kuna kazi nilienda kuifanya kwao wameniambia nirudi tena kufanya ingine.NAONA KUCHELEWA.
SHIKAMOO WALE WATU WALIJUA KUNINYOOSHA KWA KWELI.ila mkuu pole hao watu ni wachoyo.jaiwezekani chakula ambacho hata panya hamalizi mle watu wanne.HAO NI WACHOYO.
 
Najiuliza why me siwez kula chakula kingi hata nizilazimishe vip?

Kuna kipindi nilienda kijijini kwa bibi ( Tukuyu), Sasa mi nilikotoka nimezoea kula kidogo (Asubuhi chai andazi 2, mchana kaugali kadogo usiku vile vile).

Kule nikakutana na shoo za matoki na lukama, mara maparachichi asubuhi tu, ukimaliza hapo mara kuna karanga za kutafuna, mara miwa mnatafuna au mananasi, mara mihogo imechomwa au kuchemshwa, mara magimbi na maziwa, hadi menyu ya mchana umeshiba kinoma. kutokana na nilivozoea huko nilikotoka nikawa siwezi kupiga yale mazaga yote. kumbe kila kitu mazoea binamu zangu wakawa wanasema "akamanya ukulya"

Baada ya muda ile hali nikaizoea ikawa ni kutitia tu, mpaka narudi town nikawa nimenenepa kinoma. mijini watu wamejicondition kula kidogo.
 
Hiyo imenikutaga aisee, nilienda kwa jamaa alikomalia kweli nistay kwao kipindi nafuatilia mambo flani hv mkoa ule, sasa chakula daah ani inabidi nile taratibu ili tuondoke wote mezani, na pia ni kiduchu yani kale kaugali daaah!![emoji29] nilikua nakaza moyo sana[emoji28]

Sasa ajabu zaidi ikitokea nimetoka misere na mwana tukiingia mahali kula alikua analalamika kwann nisile kutosha home na wakati kinachotengwa ni kidogo sana pale mezani

Aisee alipokuja mkoani kwangu, nyumbani alijishtukia mwenyewe[emoji28] maana ile msosi najipigilia mezani ni ya kufa mtu, akaanza kusema daah inawezekana kule ulikua hushibi kaka, nisamehe bure, nikawa namvungia tu namwambia amna nimeanza speed ya kula karibuni tu, ila kiuhalisia nilikua nasongolewa na njaa mpaka nakula mgahawani

Mimi nafikiri mgeni akija hebu chakula kipikwe cha kutosha siku za mwanzoni then angalia speed yake ya kula unamkadiria kama ni mlaji unaenda nae sawa na kama sio mlaji unapunguza kipimo cha diko ili kuepuka uharibifu ila ni vizuri kumkarimu mtu chakula afurahie aisee....
 
Tushazoea kuvunja ugali bamia, tusamaki twa kukaanga machainizi na kauyoga baada ya hapo ndizi za kuiva afu niende sehemu kama hizo sitakaa lazima niage [emoji16][emoji16]
 
Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja

Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha

Ngoja nicheke kidogo[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji1787] kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue

Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku

Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani

Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali

Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi
Huo sio ustaarabu kwa mgeni. Kwa kawaida sisi unapomkaribisha mgeni kula unaenda nae mezani unamfunulia mahotpot ikiwezekana unamuonesha na maji ya kunawa tena unaanza kupakua mwenyeji, hiyo inampa confidence mgeni ajikadirie yeye kulingana na mwenendo wa mwenyeji wake.

Sasa wao wakakuacha ukafanya makamuzi mwisho lazima ujihisi fedheha
 
Watanzania tunapenda kula sana tena hovyo angalieni mtapata magonjwa.
 
We jamaa inaonekana unamuogopa mkeo iv unashindwa kumwambia kma ushibi wakati ni mkeo?

Halafu mi mke wangu hananijua tabia zangu nini napenda nini cpendi hanajua hata ratiba yangu ya kwenda chooni kunya uwa nakunya saa 12asubuhi mpaka ucku

Hanajua cpendi kuoga mara kwa mara pia na tukiwa ugenini kma kwao bac lazima apambane kuweka mambo sawa!
 
Kuna mahala nipo mimi ni mgeni, unakaangiwa nusu kuku na hapo wanataka ule na supu.Ukikaa kidogo wanakukaangia ndizi na perege kwa kweli nimekula.Pasaka wakataka kuniua wakanipikia machalari na minyama mikubwa kama ngumi ya mandonga.
Sijakaa vizuri wakaniletea chipsi na nyama za mbuzi za kuchoma.Hamadi wakaleta pilau mbuzi na vipande vya tikiti sijui na saladi.Nikala mpaka nikakasirika kwa furaha.Walivyo kiboko wakaniletea na supu.Mara paap bia hizi nkasema mi sinnywi bia wakaniletea soda tatu, ya mchana, ya asubuhi na ya jioni wakati wa kulala.Ratiba ya kuzinywa nilipanga mimi.
Yaani wakuu nilikuwa na uhakika wa kula nusu kuku kila siku.saa nyingine asubuhi kidari mchana Firigisi, jioni kipaja asubuhi namalizia kidari wakati mwingine.Nimekaa siku kumi na nne.Kuna kazi nilienda kuifanya kwao wameniambia nirudi tena kufanya ingine.NAONA KUCHELEWA.
SHIKAMOO WALE WATU WALIJUA KUNINYOOSHA KWA KWELI.ila mkuu pole hao watu ni wachoyo.jaiwezekani chakula ambacho hata panya hamalizi mle watu wanne.HAO NI WACHOYO.
Beautiful- ukarimu...... Ni mbaya sana kumnyima mtu chakula au maji ya kunywa.
Wakati mwingine uchoyo ni namna mtu alivyolelewa au pengine umelelewa vizuri tu bila choyo ila unakuta ni hulka ya mtu yaani choyo ipo ndani yake mtu na hawezi kubadilika.
 
😂😂😂 familia ikiwa kubwa hizo ndio mbizu za cuba, ajabu sasa hao wenye mji asubuhi anapita sehemu anapiga mchemsho wake, mchana anaoita shishi food anapiga makange yake ya kuku, mda wa kurudii nyumbani anapitia chips nyama anapitiliza chumbani, wanakuja yeye na mkewe wanashiba vizurii Sana, badae wanatoka chumbani wanakuja sitting room kujumuika na nyie wageni ndugu na jamaa mliokimbilia mjini kwa mjomba kudadeki kilo moja ya wali mnakula watu kumi na nyama nusu😂😂😂

Yani jumba zuri, magari nk wenye afya nzuri ni baba na mama Ila kuanzia watoto wamekonda balaa kumbe ni lishe duni
 
Aseee! Hiyo kawaida kabisa, hutokea watu wengi sana. Sisi watu wa kusini tumezoea kujaza sahani maana misosi yakutosha, hao wa Dar Wana budget Kali sana. Ila kama unamishe zako si vema sana kufikia Kwa ndugu ama jamaa, panga budget yako vema ili ufikie lodge ya Bei unayoimudu.
Kusini gan yenye misosi maan npo huku 5years chakula ni shda familia zinakula milo mi2 had mmoja baada ya msimu wa korosho

30% wanalima mahind na wakulima wachache sana wenye uwezo wa kuvuna magunia ya mahindi 7+

Huku n njaaa
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Walio gundua hotel/lodge sio wapuuzi. Kwa nini ufike nyumbani kwa mtu? Wakubwa wa nakutana baa bwana mdogo.
 
Back
Top Bottom