Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Nenda lodge
 
sio kwamba hawana cha kutosha,ndani kuna mchele,maharage,mkaa,unga nk,sema wao wamezoea kula kidogo,hivyo hufikiri kila mtu anakuwa hivyo,niliishi mwanza,faza hausi,alikuwa anasonga ugali wa kula watu 6,anapiga peke yake,sisi tukisonga wetu alikuwa anasema tunatania hatuli chakula,ugali wenyewe udaga...
Usione vingi, si vya kula siku moja. Hakuna anayezoea kula kidogo, ni njaa tu.
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Kama jina lako
 
sio kwamba hawana cha kutosha,ndani kuna mchele,maharage,mkaa,unga nk,sema wao wamezoea kula kidogo,hivyo hufikiri kila mtu anakuwa hivyo,niliishi mwanza,faza hausi,alikuwa anasonga ugali wa kula watu 6,anapiga peke yake,sisi tukisonga wetu alikuwa anasema tunatania hatuli chakula,ugali wenyewe udaga...
Nimeipenda hii, safi sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Tafuta kwako kijana

Acha kuhemea
 
Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja

Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha

Ngoja nicheke kidogo[emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji1787] kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue

Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku

Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani

Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali

Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi
Duuu! Hukutaka masihala jamaa, [emoji23][emoji23][emoji23] ulitisha kabisaaaaa
 
Nyumba yenye furaha ni yenye chakula cha kusaza. Sasa unakuta watu wanapika wali kwenye sufuria za kuchemshia chai! Kweli!!? Unakula hata ukienda toi unatoa kama mbuzi au mtoto!! Nyumba isiyo na chakula cha kutosha haina furaha hata kidogo.
Msipende kula hovyo kwa watu
 
Mtalaumu watu bure...
Sasa hivi maisha magumu tu! Vitu vimepanda bei pesa hakuna, si mijini wala vijijini. Labda kwa wale wenye fweza zao. Japo kwa wengine maisha yao yote wapo hivyo, hula kidogo.
Vijijini watu wanaishi kwashida
 
Back
Top Bottom