Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Na mm nimeishi na mtu ugali wa mtu mmoja Basi atapika mle Kama watatu HV
Huyu bwana namuonaga lege lege HV

Mtu unatakiwa upige heavy weight
 
Hahahahahhaaaaa nimecheka Sana wakati mwingine sio vzuri kutwambia Habari za nguruwe tafadhari lakini
 
Hata na mimi nashukuru nilizaliwa familiya ilokuwa na uwezo wa kilisha mtaa mzima so ishu ya vyakula nyumbani ni tangu tukiwa wadogo.
Nakumbuka tukiwa wadogo baba akiwa hai, kwanza akitoka safari anachinja ng'ombe kijiji kizima wakija kumsalimia wanakula na nyama wanabeba.
Akitoka safari chakula kinapikwa kuanzia asubuhi hadi jioni yaani kila anekuja kumsalimia baba lazima ale.
Maisha ya mama baba akiwa hai ni full time jikoni na wafanyakazi wawili
Nyumbani wageni ni full time na wengine wanalala mpaka baba akisafiri tena ndo mama anapumzika.
wabibi, baba akifika kila jion wanafata mafuta ya taa na sukali hao wote lazima waondoke wamekula, chakula kikiisha lazima mama apike kingine hata kama ni usiku.

Nyumba yenye chakula cha kutosha haikosi wageni na wafanyakazi wa kutosha. Kwetu kulikuwa kama sherehe most of the times.

Siku baba yangu amefariki watu wazee kwa vijana walilia sana. Msiba ulimaliza zaidi ya mwezi na zilichinjwa ngombe zaidi ya 10 sikumbuki idadi maana tulikwa nazo kama 300 hivi.
Kama una uwezo lisha watu washibe ili ukifa tupate na machozi ya kukulilia.

Msibani kwa baba watu walikuwa wanalia hivi:,
Wazuri hawadumu, tulikula bure, nyama tulipewa bure, sukari bure mafuta bureee, wewe mtoto nini kimekupata? Wanapiga geneza wamama, amkaaaaa sisi tunakula wapi? Amkaaa watoto wetu wanalipiwa na ada na nani? fulani amkaaaaaaa. Loh nimekumbuka mbali.
...hivi ndivyo maisha ya binadamu yalitakiwa yawe ili kumtofautisha na mnyama pia maisha huwa ni ya Furaha zaidi na Amani unapoishi kwa kusaidia watu.!Mzee azidi kupumzika kwa Amani kwa matendo yake.
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo
Wewe tumefanana alfu unakuta hyo familia ya Ina roho mbaya sna majirani hawaele wani nao
 
Ndio maana wasukuma wakienda mijini wanateseka sana..ugenini wewe jilie zako nje ukija homu unagusa tonge moja tu ya kuzugia.
Sipendi kulala kwa mtu sana
ERoni
Haha, mkuu familia nyingi za Dar watu hawali sana, nahisi matumbo yetu yamekuwa madogo au shida nini sijui.

Binafsi wakija wageni wanaume natoa tahadhari mapema, japo maza house anajua sana kupima share ila sipendi aibu za kijinga.
 
Iliwahi kunikuta nikawa natoka kuongezea kwa mama ntilie!!
 
Wala hawamfukuzi tatizo mazoea,mm mwenyew alishakujaga mdogo wangu kutoka kijijini,asubuhi ilivyofika nikaenda kuchukua mkate,basi yule ndugu yangu alimishangaa Sana mkate tule wawili.

Ikabidi ule mkate nimwachie nikanunue maandaz kwa ajiri yangu,aisee alinifutia wote[emoji3][emoji2]
Mkuu mm nimekulia mjini ni mwembamba sana ila ninakula sana, mkate mzima nafuta, chapati nakula NNE kwa kujibana sana, Kuna mgahawa Fulani nakulaga mchana chakula ni expensive ila wananifahamu nauziwa plate mbili za wali au pilau kwa bei ya plate moja ugali nakula plate mbili ndo nishibe, wanaiita msukuma, nameza dawa za minyoo kila mwezi lakini kula kupo palepale, cha ajabu sinenepi hata kidogo nazidi kukonda mpaka najiuliza chakula ninachokula kinaendaga wapi?, mwaka 2012 nilihudhuria semina flan ya mambo HIV njombe wakati wa msosi niliweka mlima wa wali na viazi ndizi Kuna wazungu wakawa wanabishana kama nitamaliza nikasema moyoni hawa hawanijui, nilifuta plate nikanyanyuka nikaongeza plate ya pili nikafuta nikala matunda na maji juu, hahahaha
 
UMENIKUMBUSHA KIPINDI CHA NYUMA WAKATI NAISHI NA EX WANGU KUNA KIPINDI RAFIKI YANGU ALIKUWA AKITUTEMBELEA AKIKARIBISHWA KULA HATAKI KABISA ANADAI AMESHIBA KWANI ALIPOTOKA ALIKUWA TAYARI YUPO FULL, IKAWA TUKIWA WAWILI ALINIAMBIA KWAMBA HUWA HATAKI KULA KWA SABABU ANAHISI HATUTASHIBA KWAAJILI YAKE KWA KUWA UGALI ULIKUWA MDOGO SANA, WAKATI ANAONGEA HAYO ME NIKAWA NIKIVUTA VICHA NI JINSI GANI HUWA TUNAMWAGA CHAKULA KINAPOBAKI KILA WAKATI... MIMI NA EX WANGU TULIKUWA HATUMALIZI UGALI MARA NYINGI NA NILIKUWA NAHISI KAMA ANAPIKA UGALI MKUBWA SANA HIVYO NIKAWA NAMSEMA KILA MARA.

BAADA YA KUJA KUACHANA NAE NA MIMI NIKAANZA KUISHI SINGLE SASA NAWEZA KISEMA YULE BEST'ANGU SASA HANIZIDI KUPIGA MSOSI YAANI NAKULA KINOMA, SUFURIA ALIYOKUWA ANATUMIA EX SASA NAIONA NDOGO KUPIKIA UGALI WANGU MWENYEWE.

SO MY POINT HERE IS, WAKATI MWINGINE SIO KUBANA BAJETI ILA MAZOEA YA WATU YANAWEZA KUWAFANYA WAKAWA WANAONA MAYBE KITU KINATOSHA KUTOKANA NA AINA YA MAISHA WANAYOISHI ILA KWA MACHO YA WENGINE IKAWA SIVYO.

KINGINE NI KWAMBA KWA UCHUNGUZI WANGU MTU ANAEISHI SINGLE ANAKULA ZAIDI KULIKO ANAEILALIA NA KUIAMKIA.
Ni vizuri kupiga msosi nawakubali sna wazee was heavyweight kula nusu nzima ya ugali
 
Mbona mkija vijijin mnakula sanaa
Huwa vijijini wanatushangaa tunavyokula kidogo, binafsi nikienda kijijini kweli ninachokula wananshangaa, ila nikikaa zaidi ya wiki naanza kuzoea mazingira na kula kunaongezeka taratibu.
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Hao Wana asili ya uchoyo.
 
Alichokitaka huyo shemeji yako ni utake kuondoka. Kwa kifupi alikufukuza kijanja kama ulivyotamania. Ni hesabu wanazozitumia sana wanawake mijini wakitembelea na ndugu toka mikoani, hasa ndugu wa upande wa 2. Kama huamini ondoka, siku ingine uje ghafla muda wa msosi, utupie jicho mezani uone shehena huta amini macho yako.
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Je wewe ni msukuma umeenda mjini? Vumilia tu utarudi shamba.
 
Ishu za misosi mara nyingi ukiwa ugenini inabidi ujinyime flani hivi.

Apo inabidi uwe na mpango wa kando unakula mgahawan uko ukija ukirudi Hapo unajaziajazia fresh siku inaenda.

Hakuna kitu kigumu Kama uwe ugenini alafu ukute Aina yao ya maisha hujazoea Kabisa Aisee!!

Kama hakuna ishu ya muhimu ya kukuweka Hapo ni Bora uage usepe walau ukakae lodge Hadi umalize Mambo yako.
Wazee walisema " ..... UGENI SI KITU CHEMA!!!"
 
[emoji23][emoji23][emoji23] familia ikiwa kubwa hizo ndio mbizu za cuba, ajabu sasa hao wenye mji asubuhi anapita sehemu anapiga mchemsho wake, mchana anaoita shishi food anapiga makange yake ya kuku, mda wa kurudii nyumbani anapitia chips nyama anapitiliza chumbani, wanakuja yeye na mkewe wanashiba vizurii Sana, badae wanatoka chumbani wanakuja sitting room kujumuika na nyie wageni ndugu na jamaa mliokimbilia mjini kwa mjomba kudadeki kilo moja ya wali mnakula watu kumi na nyama nusu[emoji23][emoji23][emoji23]

Yani jumba zuri, magari nk wenye afya nzuri ni baba na mama Ila kuanzia watoto wamekonda balaa kumbe ni lishe duni
Mkuu hivyo vitambi ni vya bia tuu hamna kitu hapo ndani....... Nashangaa siku flani tumetoka na mwenyeji wangu kupiga gambe kidogo......., Kwa sababu ni mwanaume na kitambi chake ikabidi nimshawishi tupige b&w moja ili apunguze mafuta......

Weee nashangaa mtu nusu glass tuuu anaongea kipare mixture kikurya mwisho akalala......., Yaani mwili hauna nguvu kabisa ya kuhimili pombe kidogo ila mtambi huo duuh....., ikabid nibebe mzigo wangu hivyohivyo pakiza kwenye chuma yake peleka nyumbani huko.........

Ila jamani kuleniii acheni mambo ya ajabu... mko wanne pika wali kilo moja angalau ili mtu ashibe sio maswala ya kuonjeshana......,
 
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
Dah mimi nimeshakataa kukaa nyumba ya mtu ugenini,unateseka msosi hushibi nilishawahi dakwa jikoni nadokoa chakula asubuhi asubuhi njaa kali😀😀😀,yaani jamaa hawali kabisa,ka ugali kadogo

Nikaona hapa nateseka nikawa naenda kula mtaani khaaa.
Kukaa kwa watu ni taabu
 
Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]

Unajaza wanga usio na faida. Ugali Sahani mbili zote za nini?! Au unalima heka tatu kwa siku
 
Wewe tumefanana alfu unakuta hyo familia ya Ina roho mbaya sna majirani hawaele wani nao
Hapana hawana shida na mtu wako vizuri hata mimi walikuwa wananitreat vizuri mno ila linapokuja suala la ibada zao hapo ndipo nilipokuwa naona miyeyusho ni wasabato jumamosi moja walinibeba kkwenda nao sabato
 
Mwambie mwenyeji wako. Funguka atakuelewa. Utapigiwa na kupakuliwa kiasi cha kutosha kwako.....
 
Back
Top Bottom