Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Kusema kweli mjini hasa Dar watu wanakula share ndogo sana. Chakula kinapikwa hadi unajiwazia kweli hiki watu wanashiba? Ila ndio life la town!!
Hela ngumu.wengine nk kukosa ukalimu.

Duniani kote mtu hukaribishwa moyo wa ukarimu unaanzia kwenye msosi kwanza. Mengine yanafata
 
Ishu za misosi mara nyingi ukiwa ugenini inabidi ujinyime flani hivi.

Apo inabidi uwe na mpango wa kando unakula mgahawan uko ukija ukirudi Hapo unajaziajazia fresh siku inaenda.

Hakuna kitu kigumu Kama uwe ugenini alafu ukute Aina yao ya maisha hujazoea Kabisa Aisee!!

Kama hakuna ishu ya muhimu ya kukuweka Hapo ni Bora uage usepe walau ukakae lodge Hadi umalize Mambo yako.
Ndio maama hata unapokaribisha mgeni hakikisha kama una uwezo andaa chakula cha kutosha kama akishimndwa kula iwe juu yake.

Kula bila kushiba ni mateso aisee.

Shikaji akikaa hapo wiki mbili tu atakonda
 
Kuna mwaka nilisafiri na treni kutoka Mwanza-Dar. Kufika sehemu kuna jamaa alipakia magunia ya karanga akayaweka kwenye korido ya kwenda chooni. Tukafika ktk kituo kimoja mjamaa alinunua mihogo ya kuchemsha aisee ilikuwa mihogo mingi sana na kachumbali juu, nikawa najuiliza huyu jamaa ataimaliza kweli hiyo mihogo. Aisee nilishangaa sana na nikaamini kuna watu wanakula sana yaani ni ngumu kuamini

Pigia salute kwa mwamba🫡 so unashangaa!!, hata mi kwangu sipendagi marafki urojo urojo yan mtu tonge mbiri ananawa hua siwaelewi kabisa, mtu unagonga ugari robo(minimam) mlo mmoja, pembeni upaja wa kuku na hips zake, supu bakuri la pembeni af mboga za majani pale unamalizia na juice af unamwita wife aje akunawishe, unawasha fen unangalia taarifa ya habari, sasa mwizi aje ajikatize usiku namyonga na[emoji123] sihami MBEYA🫶
 
Pigia salute kwa mwamba🫡 so unashangaa!!, hata mi kwangu sipendagi marafki urojo urojo yan mtu tonge mbiri ananawa hua siwaelewi kabisa, mtu unagonga ugari robo(minimam) mlo mmoja, pembeni upaja wa kuku na hips zake, supu bakuri la pembeni af mboga za majani pale unamalizia na juice af unamwita wife aje akunawishe, unawasha fen unangalia taarifa ya habari, sasa mwizi aje ajikatize usiku namyonga na[emoji123] sihami MBEYA🫶
😅😅😅
 
Kuna mwaka nilisafiri na treni kutoka Mwanza-Dar. Kufika sehemu kuna jamaa alipakia magunia ya karanga akayaweka kwenye korido ya kwenda chooni. Tukafika ktk kituo kimoja mjamaa alinunua mihogo ya kuchemsha aisee ilikuwa mihogo mingi sana na kachumbali juu, nikawa najuiliza huyu jamaa ataimaliza kweli hiyo mihogo. Aisee nilishangaa sana na nikaamini kuna watu wanakula sana yaani ni ngumu kuamini
Na wala sio menene
 
Ishu za misosi mara nyingi ukiwa ugenini inabidi ujinyime flani hivi.

Apo inabidi uwe na mpango wa kando unakula mgahawan uko ukija ukirudi Hapo unajaziajazia fresh siku inaenda.

Hakuna kitu kigumu Kama uwe ugenini alafu ukute Aina yao ya maisha hujazoea Kabisa Aisee!!

Kama hakuna ishu ya muhimu ya kukuweka Hapo ni Bora uage usepe walau ukakae lodge Hadi umalize Mambo yako.
ukitaka uwe una shiba....siku nunua unga kilo 5 ,utumbo kilo 3 , maharage kilo 4...pika vyote weka mezani waachiw waanze kupakua..then wewe malizia ....waambie hivi ndiyo inavyopaswa kuwa
 
Mimi mbona siwezi? Yani watu watakula kama kawaida..sasa kama sisi tumeshazoea kula kujigaragaza mgeni aje ndo tule kama mijusi..au hao ndo wamezoea hivyo ila sidhani itakua ni uchoyo tuu..ukute hatq huyo mume hashibi
 
Alikufa at age of 30 yrs can you imegine.
Si unajua mtu akifa gafla maneno mengi lazima yatoke nani kasababisha?
Ilikuwa 1993 baba alikuwa akimsomesha sekondari bint wa bibi mmoja.
Siku mbili kabla ya kifo chake huyo bibi alikuja nyumbani akakuta baba yuko holi akaanza kulia nini kimempata mtoto wangu?
Huyo bibi alivyotoka analia akasikia umbea kuwa fulani wenda kafanya kitu.

Huyo bibi wakati huo alikuwa mmama wa makamo, mimi nilikuwa mdogo ila hiyo kumbukumbu ninayo.

Bibi huyo niliona kavua ndala kakimbia peku akielekea kwa huyo mtu walokuwa wakimsema wenda kafanya jambo baya kwa baba.

Alivyofika kwa huyo mtu nasikia alitembea na magoti akimuomba kama kafanya chochote basi asemè anataka nini. Nasikia huyo mtu akajibiwa bora akipelekwa hospital arudi jeneza na wengine tuwe na maisha mazuri.

Bibi huyo alirudi nyumbani analia akasema kama kuna mkono wa binadamu kwa mwanangu huyo mtu nishuhudie akimfata mwanangu. Nadhani huyo bibi alijuwa lazima baba afe.
Baba akapelekwa hospital j2.
Haya yote yanatokea mama alikuwa kaenda kujifungua......
Baba alikuwa amemsomesha kaka fulani hivi ana exposure ya kwenda hata sehem x, mbali kweliii alivyoona hali inakuwa mbaya ikabidi aandike barua amtume huyo kaka amwambie mama awahi. Usafiri zamani ulikuwa wa shida sana.
Huyo kaka alivyofika akakuta mama kajifungua mtoto wa kiume, akarudisha taarifa kuwa mama kajifungua atakuja alihamisi.
Juma nne huyo kaka akarudisha majibu kuwa mama kajifungua mtoto wa kiume atakuja alhamisi.

Baba akasema neno la mwisho " nimekufa bila kumuona mwanangu wa kifume" na dk hiyo akafariki.

Kweli mama anafika siku hiyo ya alhamisi analeta mtoto hajui habari za msiba wamesubiri wapi anakuta tunazika. Iliuma vibaya mno. Naikimbuka hiyo siku ila nilikuwa mdogo sikujua kuwa hatorudi.

Mtuhumiwa mauti nae yamemkuta mwaka jana baada ya miaka 29 ila yeye amedumu. Ameona wajukuu zake baba yangu hakuona kitu.

Mtuhumiwa siku alipo kufa, yule bibi aliyeenda kumuoma kama kafanya kitu arudishe moyo baba apone, bibi alivyosikia kifo cha mtuhumiwa wa kifo cha baba, alilia akasema fulani uliniulia mwanangu ukijua Mungu hakuoni? hayo ni malipo yako.

Maskini huyo bibi hata hamzai baba yangu sema tu alimsomeshea binti yake na huyo binti kwa sasa ni mwalimu mkuu.

Fatilia hata kwenu, watu wema wanaosaidia jamii hawawezi ishi muda mrefu. Akiishi sana miaka 50.
Nakubaliana na wee [emoji817]
 
Mi hata nikiwa mkoa wenye mamangu mdogo sijui mjombangu.
Nafikia hotel, nitaenda kuwasalimia narudi kulala na kula ninakokujua!
Nitakaribishwa chakula nitakula kwa kuojnja sana ili niisharibu bajeti za watu!

Mambo ya kulala chumba cha kina juniya, woooi!
 
Ila ugenini kunaweza kukufanya usiwe na raha kuna sehemu nilifikia kabla ya kulala usiku wanaka ibada wanakusanyika sebuleni wakiamka ahsubuhi saa 12 kaibada nami sijazoea hiyo michongo

Jwanza haya mambo ya mtu mzima kufikia kwa watu sijuwi yanakuwaje Tanzania. Kwanini usifikie hotel ukawa huru?

Dunia ya leo si ya kufikia kwa watu, mahoteli yamejaa kila sehemu.

Kula kwa mtu ni kwa kualikwa tu.
Ni kweli lkn vipi kama kaja mjini kutafuta maisha watakaa lodge mpaka lini na istoshe hata hela lodge hana,muda mwingine tunabebana tu hivo hivo japo kuwa kuna baadhi ya wageni hawanaga shukran anataka ustarabu wake alikuja nao ndo ufatwe na wanakuaga na maneno ya kuwachafua wenyej wao hao. Hawafai
 
First appointment tangu nilipangiwa Pwani, kutokana na bajeti finyu niliyokuwa nayo sikula chochote njia nzima mpaka nafika
Miaka hiyo hakukuwa na bodaboda hivyo kushuka stendi nikaelekezwa tu kwa mwenyeji wangu. Alikuwa mzee maarufu sana hiyo mitaa, nikatembea mwendo wa dakika kumi nikafika. Ilikuwa kwenye saa nane hivi
Nikakuta wako mesi wanagonga wali maharagwe na samaki, nikakaribishwa kwa bashasha sana lakini nikazuga nimeshiba sana maana njiani gari ilisimama mahali tukala ( najuta kufanya vile)

Ningekuwa nafahamu taratibu za watu ningekubali kula siku ile, lakini bila kujua nilijipa moyo kwamba jioni nitakula nishibe maana nilikotoka nilikuwa nimekunywa chai rangi na andazi moja tu asubuhi

Yule mzee alikuwa mkarimu na mtu wa story sana kwahiyo mchana wote tulishinda hapo kwake upenuni mpaka jioni alipoenda msikitini
Sasa mimi njaa inauma mida inasogea kigiza kinaingia ila sioni harakati zozote za maandalizi ya dinner ( ilikuwa familia ya watu watano baba, mama, mabinti wawili na kijana wa kiume)

Nikajipa moyo kwamba pengine kilipikwa na cha jioni ule mchana.. Kufika saa mbili usiku mzee akarudi na mkate! Kwa mawazo yangu ulikuwa kwa ajili ya kesho asubuhi
Dakika chache baada ya mzee kurudi nikaitwa ndani kwa ajili ya dinner..! Lahaula rasuli! Dinner ilikuwa kikombe cha chai ya rangi na silesi mbili za mkate[emoji23]
Kwanza nilidhani tunapasha matumbo joto halafu mahanjumati yaja.. Pengine misamaki tasi, kolekole, pweza wa kubanikwa chapati na mkate wa kumimina ama kiporo cha mchana! Naona kila anayemaliza ananyanyuka mezani.. Nilikuwa wa mwisho

Hakuna kitu kinatesa kama njaa ya ugenini..!!!
Nimekumbuka mbali kuna familia moja nliwahi fikia dar ubwabwa unapikwa ijumaa unaliwa jumamosi hadi jumapili chai,nyama inaliwa mchemsho tena namboga za majani chukwu chuckwu(hii nliipenda )japo sharti nyama ni moja moja kipande cha mshkaki duh. Kweli dar maisha magumu japo wengine na ka uchoyo kapo ndani yao...nyie ila nlikuwa na wakati mgumu wkend yote kugalagala na kiporo cha wali ..
 
Kuna mahala nipo mimi ni mgeni, unakaangiwa nusu kuku na hapo wanataka ule na supu.Ukikaa kidogo wanakukaangia ndizi na perege kwa kweli nimekula.Pasaka wakataka kuniua wakanipikia machalari na minyama mikubwa kama ngumi ya mandonga.
Sijakaa vizuri wakaniletea chipsi na nyama za mbuzi za kuchoma.Hamadi wakaleta pilau mbuzi na vipande vya tikiti sijui na saladi.Nikala mpaka nikakasirika kwa furaha.Walivyo kiboko wakaniletea na supu.Mara paap bia hizi nkasema mi sinnywi bia wakaniletea soda tatu, ya mchana, ya asubuhi na ya jioni wakati wa kulala.Ratiba ya kuzinywa nilipanga mimi.
Yaani wakuu nilikuwa na uhakika wa kula nusu kuku kila siku.saa nyingine asubuhi kidari mchana Firigisi, jioni kipaja asubuhi namalizia kidari wakati mwingine.Nimekaa siku kumi na nne.Kuna kazi nilienda kuifanya kwao wameniambia nirudi tena kufanya ingine.NAONA KUCHELEWA.
SHIKAMOO WALE WATU WALIJUA KUNINYOOSHA KWA KWELI.ila mkuu pole hao watu ni wachoyo.jaiwezekani chakula ambacho hata panya hamalizi mle watu wanne.HAO NI WACHOYO.
We au ulikuwa mbinguni mwenzetu hujui
 
Back
Top Bottom