Nipo upande wa Manara 100% wenye akili watamuunga mkono

Nipo upande wa Manara 100% wenye akili watamuunga mkono

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Nawasalimuni nyote wanamichezo. Kwanza kabisa mimi ni shabiki wa Simba kabisa ila kuna kitu hakiko sawa.

Sitaki kuongelea mambo yooote sababu hayataisha ila nalenga chanzo tu. Kumekuwa na hoja nyingi sana kuhusu Manara kuwa anafanyaje kazi simba huku akitangaza bidhaa za Azam, hilo lipo sahihi kabisa, ndio yupo sahihi, kwani nani kamwajili Manara? Ni Simba au Mohamed enterprises? Msije kuchanganya hapo Manara anafanya kazi Simba utamlazimishaje atangaze bidhaa za bosi wake wakati ni vitengo viwili tofauti?

Kwa mfano Umeajiriwa kazi ya kuuza dukani na mmekubaliana mshahara ni 60,000, utajisikiaje boss aliekuajiri akikulazimisha jioni baada ya kufunga duka ukamsaidie kufanya kazi za nyumbani? Utakubali?.

Mambo mengine yanatokea sababu ya kutokukamilika kwa mwanadamu pamoja hasira na jazba. Manara anaipenda Simba lakini kuipenda huko hakuwezi kumfanya afanye mambo yasiyo na maslahi maishani mwake.

Watanzania acheni kuchukulia mambo powa. Kama Mo alitaka atangaze bidhaa zake angepanda dau zaidi ya azam na kama alitaka avunje mkataba angeweza kulipa gharama za kuvunjwa mkataba huo?

GENTAMYCINE Mshana Jr

HONGERA MANARA KWA KUANGALIA MASLAHI YAKO BADALA YA KUANGALIA YA WATU.
 
Sitaki kuongelea mambo yooote sababu hayataisha ila nalenga chanzo tu. Kumekuwa na hoja nyingi sana kuhusu Manara kuwa anafanyaje kazi simba huku akitangaza bidhaa za Azam, hilo lipo sahihi kabisa, ndio yupo sahihi, kwani kwani nani kamwajili Manara? Ni Simba au Mohamed enterprises? Msije kuchanganya hapo Manara anafanya kazi Simba utamlazimishaje atangaze bidhaa za bosi wake wakati ni vitengo viwili tofauti?
Na mimi nauliza maswali machache tu. Hivi kuajiriwa mahali fulani, tena sekta binafsi, ni lazima? Kwani Manara kuondolewa Simba, hana mahali pengine akaenda kuajiriwa au kujiajiri? Kama ipo, kuna ulazima gani kulalamika kuachishwa kazi ambayo ulikuwa hata hauna mkataba? Mbona makocha wengi tu wanaachishwa kibarua baada ya muda mfupi tu, na hawaitishi press?

Mtu umeambiwa kwamba jina lako halimo kwenye msafara wa timu, kwa mapenzi yako unaamua kukata tiketi kuifuata timu. Hotel imelipiwa waliopo kwenye msafara tu, wewe unaamua kulala receiption. Hapo kosa la nani? Ukilipa nauli unadhani na chumba utapata?
 
Kwanini alikaa kimya muda wote huo,mpaka alipoondolewa ndo anapuyuka,wanaomtuma aivuruge Simba hawatoweza,Simba ipo makini sana,walipita wengi wakaiacha Simba ipo na itaendelea kuwepo.
Fikiria tu kidogo hata kama ni wewe, ukiwa na mgogoro na bosi wako utaweza kumchafua wakati ukiwa kazini?
 
Mbona makocha wengi tu wanaachishwa kibarua baada ya muda mfupi tu, na hawaitishi press?
Hawana content za kusema, kumbuka Manara alifanya kazi Simba kwa mapenzi na kwa kazi,kwa hiyo mambo mengine aliyafanya kimapenzi bila kujali anapoteza au anapata nini.
 
kwa kweli huyu mtu ameonewa sana, sijui kama serikali kupitia wizara ya inayoshugulika na ajira & kazi ipoo
Kaonewa sana... hebu jiweke kwenye nafasi ya Manara uone jinsi utakavyopata maumivu makali ya kihisia na kiakili. Uongozi mzima hakuna pa kukimbilia, hakuna anakusikiliza hata kama ni wewe ungeenda kutafuta faraja nje tu.
 
Hawana content za kusema, kumbuka Manara alifanya kazi Simba kwa mapenzi na kwa kazi,kwa hiyo mambo mengine aliyafanya kimapenzi bila kujali anapoteza au anapata nini.
Kama huna sifa, hata uwe na mapenzi gani, mfumo utakuondoa tu. Utakuwa na mapenzi ya kuwa Jaji, lakini kama hauna digrii ya sheria, inabidi uwe mshabiki tu wa majaji
 
Manara alikuwa kila siku anawasifia akina chama na miquisone
alifikiri wameokotwa sijui

Manara ndio alikuwa anaitumia simba kwa maslahi yake binafsi

yupo simba tangu 2015

hebu tuambieni 2015 alikuwa na mkataba na kampuni gani

Mo ameweka pesa
hela inaongea
 
Kama huna sifa, hata uwe na mapenzi gani, mfumo utakuondoa tu. Utakuwa na mapenzi ya kuwa Jaji, lakini kama hauna digrii ya sheria, inabidi uwe mshabiki tu wa majaji
Sawa lakini mfumo umemtoa kwa sababu ya uhalisia wake. Mo anaonea wivu mkataba wa azam na Manara ndio maana akamtoa, kama yeye anapenda kutonga Manara amsaidie nini sasa?
 
Nawasalimuni nyote wanamichezo. Kwanza kabisa mimi ni shabiki wa Simba kabisa ila kuna kitu hakiko sawa.

Sitaki kuongelea mambo yooote sababu hayataisha ila nalenga chanzo tu. Kumekuwa na hoja nyingi sana kuhusu Manara kuwa anafanyaje kazi simba huku akitangaza bidhaa za Azam, hilo lipo sahihi kabisa, ndio yupo sahihi, kwani kwani nani kamwajili Manara? Ni Simba au Mohamed enterprises? Msije kuchanganya hapo Manara anafanya kazi Simba utamlazimishaje atangaze bidhaa za bosi wake wakati ni vitengo viwili tofauti?

Kwa mfano Umeajiriwa kazi ya kuuza dukani na mmekubaliana mshahara ni 60,000, utajisikiaje boss aliekuajiri akikulazimisha jioni baada ya kufunga duka ukamsaidie kufanya kazi za nyumbani? Utakubali?.

Mambo mengine yanatokea sababu ya kutokukamilika kwa mwanadamu pamoja hasira na jazba. Manara anaipenda Simba lakini kuipenda huko hakuwezi kumfanya afanye mambo yasiyo na maslahi maishani mwake.

Watanzania acheni kuchukulia mambo powa. Kama Mo alitaka atangaze bidhaa zake angepanda dau zaidi ya azam na kama alitaka avunje mkataba angeweza kulipa gharama za kuvunjwa mkataba huo?

GENTAMYCINE Mshana Jr

HONGERA MANARA KWA KUANGALIA MASLAHI YAKO BADALA YA KUANGALIA YA WATU.
Naomba kujua sababu ya Wewe Kunitaja hapa kwani naona kama vile una hamu ya Kulipukiwa na Bomu Kubwa kutoka nchini Israel ukilinganisha sasa nina Hasira Kali, mbaya na za hatari alizonipandisha huyo 'aliyebwabwaja' Jana.
 
Manara mpuuzi tu, soka Ni pesa, uswahili pelekeni huko.

Eti alisema aliitwa na Mo akaambiwa kuwa amekuwa maarufu kuliko Mo!! Kwa hiyo afukuzwe!

Yaani bilionnaire amuite Manara kumwambia kuwa amezidiwa umaarufu?

Mnaokaa upande wa manara mkapimwe akili.
 
Naomba kujua sababu ya Wewe Kunitaja hapa kwani naona kama vile una hamu ya Kulipukiwa na Bomu Kubwa kutoka nchini Israel ukilinganisha sasa nina Hasira Kali, mbaya na za hatari alizonipandisha huyo Mzungu Pori na 'Bwabwa' wenu 'aliyebwabwaja' Jana.
Acha chuki kijana,unaringia uzima wa afya au uzima wa mwili? Inaonekana unamchukia Manara toka akiwa msemaji wa simba
 
Wivu huo, sa kama huna vigezo yeye akusaidie nini? Lakini ndio jadi ya wavivu hasa watz hamtaki kuona mwenzenu akiwa na kitu
Kwanza Manala anawanyima vijana wengine ajira haiwezekani uwe Simba uwe Azam uwe ASAS uwe GSM wewe tu
 
Back
Top Bottom