Heshima Mkuu!
Nianze kwa kusema kuwa, si kupiga picha tu kwa Mapozi.Bali pia kupiga picha ya aina zote pasipo a, b, c, d's za upigaji picha na kuzi-enamse mitandaoni pasipo ridhaa yenye kuzingatia Mantiki na si ushabiki.
Pia ni kuingilia faragha ya Marehemu pasipo ridhaa stahiki.Si mmoja wa wana familia, si mwandishi wa habari, si mpiga picha mahususi nk, ya nini upige picha?.
Pia elimu sahihi juu ya Matumizi sahihi ya Simu janja (Smart-phones) inabidi itolewe kwa wingi miongoni mwa wana jamii ili kuepuka u-holoi poloi wa namna hii usiozingatia Logic ya jambo husika.
Madhara ya utumwa mamboleo ya kuiga kila kitu kutoka Magharibi na Mashariki ya mbali na kuileta katika jamii yetu then utegemee matokeo yaleyale ni kujipumbaza kihalaiki.Ni un-ethical kwa Maadili ya kitanzania.
Si sahihi Mkuu.