Nisahihishe kama si kweli, lakini Iran haina hofu sana na Marekani, Inayemwogopa hasa ni Benjamin Netanyahu

sijui hao vilaza wanafatilia hii vita wakiwa wapi maana wanongea vitu vya kitoto
 
Bila kumdhibiti Netanyahu itakuwa hatari sana.Haoni shida kubonyeza kitufe cha silaha hatari na kufanya maangamizi makubwa.
kwa wenye upeo na maswala ya vita ukiona mtu anafanya hivyo ujue kashindwa sasa inabidi atumie njia ya mkato zaidi...
 
Acha uongo, basi mwaka Jana ambapo Israel alikua almost mwenye si wangepiga hata ndege Moja🤣🤣

Wakaishia kuongopa wameangusha ndege ya Israel, watu wasubiri picha. Hadi Leo mwaka sasa hakuna picha hata ya bahati mbaya.
ayatollah kauliwa,moto ukawashwa mtu na shoga yake wakaomba mazungumzo ili yaishe
 
pole
 
Iran walisema kama Israel itaendelea kushambulia Lebanon na Gaza basi wao pia wataishambulia Israel. Israel bado inaendelea kushanmbulia Lebanon na Gaza, Mbona Iran hajarusha hata kokoto kwenda Israel?
Iran wanajua kwamba safari hii wakithubutu kuigusa Israel, huenda Tel Aviv isisikilize tena amri za Trump za kusimamisha mashambulizi. Na kama unavyoijua Israel, ndani ya siku moja tu taarifa zinaweza kuanza kumiminika: Breaking News, waziri wa ulinzi amelengwa, mkuu wa usalama wa taifa ameshambuliwa, makamanda wa IRGC, viongozi wa jeshi la anga, n.k. hakuna nafasi iliyo salama, Wanaweza kujificha kwenye mahandaki hata uvunguni mwa vitanda lakini wakishawekwa kwenye 18 hawachomoki.
 
Km sio Trump kumzuia netanyau

magaidi ya Iran yangeshasambaratika
Alimzuia lini na wapi? Mbona alimpa greenlight ashambulie bila msaada wa USA ila tokea hapo aliufyata.

Israel haiwezi lolote bila US, otherwise taja hata vita moja ambayo Israel wamepigana bila msaada wa US. Moja tu itaje
 
Alimzuia lini na wapi? Mbona alimpa greenlight ashambulie bila msaada wa USA ila tokea hapo aliufyata.

Israel haiwezi lolote bila US, otherwise taja hata vita moja ambayo Israel wamepigana bila msaada wa US. Moja tu itaje
12 Day war vita ya mwaka jana ambayo Israel ilituma marubani wa kike kwenda kufanya mazoezi kwa vitendo Iran walifyeka mawaziri wa ulinzi, usalama wataifa, mkuu wa jeshi irgc, n.k.

Ni mpaka siku ya 12 Trump aliposikia Israel wanaenda kumla kichwa Ayatollah akawaomba wasitishe na vita ikaishia hapo.

VIta ya mwaka huu ilipoanza ilikuwa ni Joint Op, Lakini kwa upande wao Israel wakaanzia pale pale walipoishia,
 
Mbona Trump aliwaambia wapigane wenyewe ila Israel ikapotezea. Si waje wenyewe Iran bila US wanasubiria nini?

Kma US alidunguliwa ndege 42 hao Israel watatoboa bila Air defense ya US?
 
Mbona Trump aliwaambia wapigane wenyewe ila Israel ikapotezea. Si waje wenyewe Iran bila US wanasubiria nini?

Kma US alidunguliwa ndege 42 hao Israel watatoboa bila Air defense ya US?
Trump amewahi kuwazuia tu Israel wasiende kumla kichwa Ayatollah na mwaka huu akawaamuru kuacha mashambulizi,

Iran imelenga hata ndege moja ya Israel hata kwenye vita ya mwaka jana ambayo wanafunzi wa kike walitumwa kufanya field ?
 
Acha upotoshaji, kwenye 12 day war hao US walishiriki umesahau operation midnight hammer ambapo walitumia B2 bombers kuangusha "bunker busters" kwenye Nuclear stations za Natanz na Fordo? Hao Israel hawana hizo silaha wala ndege so bila US hakuna nuclear facility waliokua na jeuri hata ya kuvunja kufuli.

Israel bila US haina lolote, otherwise taja hapa vita yoyote ambayo Israel imepambana na taifa jingine bila US?
 
Marekani ilishiriki kwenye kusambaratisha nuclear

Marubani tena wa kike wa Israel walitumwa kufanya mazoezi kwa vitendo na waliweza mission kwa kuwaua viongozi wakubwa wa jeshi la Iran,

Walipotaka kwenda kumla kichwa Ayatollah, Trump akainua simu akawaamboa inatosha, hata hivyo vita ya mwaka huu marubani wa Israel walianzia palepale walipoishia
 
wangetimiza ndoto Yao ya miaka yote ya kuiangamiza Israel.
Lini wamesema hili? Kwani wakitaka kuiangamiza Israel si wangetengenezea nuclear bomb huko Russia ambako scientists wa Iran wapo na wangerusha kwani kinawashinda nini?

Huo sio mpango wao na ndio maana huwa mkiulizwa muweke ushahidi wa hiko kitu hamnaga
 
Acha uongo, basi mwaka Jana ambapo Israel alikua almost mwenye si wangepiga hata ndege Moja🤣🤣
Hakuwa mwenyewe walisaidia na USA kupitia mission ya midnight hammer. Israel hana jeuri ya kupigana na taifa lolote bila USA.

Taja vita moja tu aliyopigana mwenyewe
 
Hivi Iran akaenda one vs one na Israel unaona nafasi ya Israel kushinda kirahisi?
Hivi Iran akaenda one vs one na Israel unaona nafasi ya Israel kushinda kirahisi?
Hiyo vita inapiganwa vipi? Ikiwa ni vita kamili yaani Israel na yeye arushe tu mabomu na kupiga Iran kama Iran anavyorusha mabomu kwenda Israel pasipo kupoint maeneo ya kijeshi, Iran ataangamia pakubwa sana sababu Israel huwa anapossess anga la Iran kadri atakavyo.

Israel hulenga shabaha, Iran yeye anarusha makombora tu basi popote pale lifike. Sasa jiulize leo hii Iran yarushwe makombora tu, patakalika pale? Iran hana ulinzi wa kuzuia anga lake, hii ni kete kubwa sana ameipoteza.
 
Kwamba Iran hana air defense system kiongozi? Hebu angalia madesa yako vizuri huenda habari za Foxnews,bbc na vituo vya wale wahuni vinapotosha.

Iran anayo mifumo kibao ya kujilinda ya anga ambayo anatengeza yeye na kununua nje pia.Sasa ukisema Israel anatawala anga la Iran unakuwa umeweka na ushabiki pia sio uhalisia.

Narudia Israel akienda one vs one na Iran chance ya kupasuka ni kubwa.Israel ya kwenye media na uhalisia ni vitu viwili tofauti.

Kwenye media Israel ni jitu kubwa kweli njoo sasa kwenye uhalisia hamna kitu.Hamas majanja tu wa Palestine walishikilia mateka Israel akaanza kurusha tu makombora kamaa kichaa anaua raia wasio sehemu ya vita leo hii unasema Israel anapiga kwa target?
 
Siyo kwamba Israel ameona moto wa Iran?
 
Hivi Iran akaenda one vs one na Israel unaona nafasi ya Israel kushinda kirahisi?
Wapiga debe tu hao,hawana ukweli wowote wanaouzungumzia. Kama Israel ina nguvu kubwa kwanini kajitenga na Vita walivyovianza pamoja na kuiacha Marekani peke yake!?
Kama Iran ni dhaifu au waoga wanaweza kuendeleza Vita kwenye maeneo mengine zaidi haliyakuwa Marekani na Israel wanapokezana!?
 
Kupenda kubaya kaka! na duniani hakuna asiependa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…