bnyanya
Senior Member
- Sep 27, 2013
- 178
- 63
Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 30. Nina mtoto mmoja. Wakati wa usichana wangu...nilikua kicheche sana na niliishi maisha ya gharama sana na nilibahatika kupendwa na watu wengi sana wenye pesa na wasio na pesa....na ilifikia hatua nikaamua kuacha hayo mambo na kustick na mtu mmoja ambae alikua mwanafunzi wa chuo ambae nilikua nampenda na kuhisi atakua mume wa maisha yangu na ndie niliyezaa nae.
Niliamua kuokoka na kua na hofu ya Mungu. Sikutaka tena mahusiano ya nje. Kwasababu hakukua na kipya kwangu. Kama starehe nilishafanya sana.
Maisha yakaanza...mume wangu alikua ananipenda. Lakin kwasababu ya uzuri wangu wanamme hawajaacha kunisumbua kila leo natongozwa. Mume wangu anajua background yangu...na kwakweli amekua msaada mkubwa katika maisha yangu.
Ni mwanamme anayependa na mwenye matamanio mazuri katika maisha yetu. Kuna ugonjwa mkubwa umenipata na yeye hapo alikubali kua bega kwa bega na mimi mpaka mwisho.
Nikweli alikubaliana na hali yangu lakini kadri siku zinaenda anakua na lugha chafu...kejeli. .dharau..matusi..na kunipiga na kuanzisha mahusiano nje. Mbaya zaidi hua anakuja kuniambia uchafu wote anaoufanya nje.
Alikua na kazi nzuri...lakin ikaisha kwasasabu ya kunidharau na kuchezea pesa na mwanawake wa nje ambae ilifikia mahala anampa simu yake anapokea.
Wakati anafanya yote hayo sikua na faraja na ndipo nilipoamua kutafuta mwanamme wa kuniliwaza nikiwa nimeshakata nae tamaa.
Soon mume alikuja na kunikuta na meseji ya huyo bwana na nikakili kua nina uhusiano nae. Mume wangu akanisamehe na nikamhaidi sitarudia tena lakin cha kushangaza anaenda kwa boss wangu kueleza yanayotokea nyumbani na kunitangaza kwa watu juu ya ugonjwa nilionao na mbaya zaidi bado anawasiliana na mwanamke wake mpaka muda huu. Na huyo mwanamke anapata kiburi cha kunikutaka na kunidharau na kunieleza madhaifu yangu ya magonjwa ambao ambayo mume wangu alimusimulia.
Nazidi kuumia zaidi nnapojua familia ya mme wangu inamfahamu huyo mwanamke wa nje na wanawasiliana na wifi zangu.
Wakati niko peke yangu nikifanya miradi ya maendeleo ambayo hata mume wangu alikua haijui....na iliniwezesha kujikimu kimaisha na mtoto wangu.
Sasa akarudi amerudi kwangu akiwa hana kazi...na akitaka kuanza maisha na mimi huku akisaidiwa mtaji wa biashara na ndugu zake ili tuweze kuishi kama familia.
Lakin mbaya zaidi..simu yangu yake..ya kwake yakwake...na anahisi bado nipo na mahusiano na yule mwanamme. Na hata ninapokwenda kwenye biashara zangu ananichunga na kuniwekewa mipaka ya kufanya kazi.
Akiwa kwangu...hatoi mahitaji wala kujishughulisha na chochote. Na anakua anaishi kwa kunitafutia sababu mpaka anataka kuniua. Hapa nilipo kanipiga sana mpaka nikapelekwa hospital.
Naombeni ushauri wenu ushauri. ..nataka nirudi kwetu na mtoto wangu nina kazi nina uwezo wa kufanya biashara..hapa nilipo nafatilia uhamisho.