Nisaidie ushauri...ndoa imenishinda

Nisaidie ushauri...ndoa imenishinda

bnyanya

Senior Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
178
Reaction score
63
Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 30. Nina mtoto mmoja. Wakati wa usichana wangu...nilikua kicheche sana na niliishi maisha ya gharama sana na nilibahatika kupendwa na watu wengi sana wenye pesa na wasio na pesa....na ilifikia hatua nikaamua kuacha hayo mambo na kustick na mtu mmoja ambae alikua mwanafunzi wa chuo ambae nilikua nampenda na kuhisi atakua mume wa maisha yangu na ndie niliyezaa nae.

Niliamua kuokoka na kua na hofu ya Mungu. Sikutaka tena mahusiano ya nje. Kwasababu hakukua na kipya kwangu. Kama starehe nilishafanya sana.

Maisha yakaanza...mume wangu alikua ananipenda. Lakin kwasababu ya uzuri wangu wanamme hawajaacha kunisumbua kila leo natongozwa. Mume wangu anajua background yangu...na kwakweli amekua msaada mkubwa katika maisha yangu.

Ni mwanamme anayependa na mwenye matamanio mazuri katika maisha yetu. Kuna ugonjwa mkubwa umenipata na yeye hapo alikubali kua bega kwa bega na mimi mpaka mwisho.

Nikweli alikubaliana na hali yangu lakini kadri siku zinaenda anakua na lugha chafu...kejeli. .dharau..matusi..na kunipiga na kuanzisha mahusiano nje. Mbaya zaidi hua anakuja kuniambia uchafu wote anaoufanya nje.

Alikua na kazi nzuri...lakin ikaisha kwasasabu ya kunidharau na kuchezea pesa na mwanawake wa nje ambae ilifikia mahala anampa simu yake anapokea.

Wakati anafanya yote hayo sikua na faraja na ndipo nilipoamua kutafuta mwanamme wa kuniliwaza nikiwa nimeshakata nae tamaa.

Soon mume alikuja na kunikuta na meseji ya huyo bwana na nikakili kua nina uhusiano nae. Mume wangu akanisamehe na nikamhaidi sitarudia tena lakin cha kushangaza anaenda kwa boss wangu kueleza yanayotokea nyumbani na kunitangaza kwa watu juu ya ugonjwa nilionao na mbaya zaidi bado anawasiliana na mwanamke wake mpaka muda huu. Na huyo mwanamke anapata kiburi cha kunikutaka na kunidharau na kunieleza madhaifu yangu ya magonjwa ambao ambayo mume wangu alimusimulia.

Nazidi kuumia zaidi nnapojua familia ya mme wangu inamfahamu huyo mwanamke wa nje na wanawasiliana na wifi zangu.

Wakati niko peke yangu nikifanya miradi ya maendeleo ambayo hata mume wangu alikua haijui....na iliniwezesha kujikimu kimaisha na mtoto wangu.

Sasa akarudi amerudi kwangu akiwa hana kazi...na akitaka kuanza maisha na mimi huku akisaidiwa mtaji wa biashara na ndugu zake ili tuweze kuishi kama familia.

Lakin mbaya zaidi..simu yangu yake..ya kwake yakwake...na anahisi bado nipo na mahusiano na yule mwanamme. Na hata ninapokwenda kwenye biashara zangu ananichunga na kuniwekewa mipaka ya kufanya kazi.

Akiwa kwangu...hatoi mahitaji wala kujishughulisha na chochote. Na anakua anaishi kwa kunitafutia sababu mpaka anataka kuniua. Hapa nilipo kanipiga sana mpaka nikapelekwa hospital.

Naombeni ushauri wenu ushauri. ..nataka nirudi kwetu na mtoto wangu nina kazi nina uwezo wa kufanya biashara..hapa nilipo nafatilia uhamisho.
 
^^
Ndoa maji ya shingo.. Hata ukiondoka mtoto wenu ni daraja litakalowaunganisha.
Mnamsaidia mtoto kukosa mapenzi ya wazazi wawili.
^^
 
Ugonjwa mkubwa ni upi kuwa wazi usaidiwe mm naona tuanze kwanza na ugonjwa hayo mengine blaa blaa tu.
 
Shosti pole sana,Siwezi kukwambia ondoka muache mumeo lakini kama ningekua mimi naona hata kunisahau ameshanisahau
yani kwenye raha akale na mpenzi wa nje shida ndio ule nae wewe kwani wewe hujui raha au hujui kutumia? kwakwelu shosti huyo sio mume anajishikiza tuu akifanikisha ataondoka tena lakini angalia moyo wako vile unavyokutuma usije hama mji halafu ukampigia cm mtoto anataka kukusalimia,fanya ukiondoka ndio umeondoka,Jengine mawifi shosti katika hao mawifi atakae kuona wifi sawa asiekuona wifi basi shida yako mume sio wifi wala shemeji mwenye gubu hao watu mie hata hawanilazi macho,muhimu mama mkwe na baba mkwe ..............
 
Pole sana na huo mkasa lakini huyo mmeo ni wa ndoa au kwa vile mnaishi pamoja? Anaishi kwako au kwa mwanaume? Mna vitu vya pamoja?
 
pole sana.........

na wewe utakuwa hujielewi,,,,,,,,,,,

unadai uliacha ukicheche kwasababu ya hofu ya mungu na huoni jipya lakini ukamegwa tena kisa mumeo anamega............. hii inaonesha hata wewe hujipendi.........

hapo hamna ndoa , ni mnaishi tu pamoja,,,,,,,,,,,,,, ukichukua background chafu + on and off history of cheating kwa pande zote........... halafu mmeanza kupeana madhara ya kimwili(kupigana) , bila kusahau mabadiliko ya tabia kumpelekea mmoja wenu mpaka kufukuzwa kazi, hapo kuna mushilization inakuja.

, mrudieni mungu mfanye toba na sala ya kunusuru ndoa yenu ikishindikana muachane, hamna namna.
 
Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 30. Nina mtoto mmoja. Wakati wa usichana wangu...nilikua kicheche sana na niliishi maisha ya gharama sana na nilibahatika kupendwa na watu wengi sana wenye pesa na wasio na pesa....na ilifikia hatua nikaamua kuacha hayo mambo na kustick na mtu mmoja ambae alikua mwanafunzi wa chuo ambae nilikua nampenda na kuhisi atakua mume wa maisha yangu na ndie niliyezaa nae.

Niliamua kuokoka na kua na hofu ya Mungu. Sikutaka tena mahusiano ya nje. Kwasababu hakukua na kipya kwangu. Kama starehe nilishafanya sana.

Maisha yakaanza...mume wangu alikua ananipenda. Lakin kwasababu ya uzuri wangu wanamme hawajaacha kunisumbua kila leo natongozwa. Mume wangu anajua background yangu...na kwakweli amekua msaada mkubwa katika maisha yangu.

Ni mwanamme anayependa na mwenye matamanio mazuri katika maisha yetu. Kuna ugonjwa mkubwa umenipata na yeye hapo alikubali kua bega kwa bega na mimi mpaka mwisho.

Nikweli alikubaliana na hali yangu lakini kadri siku zinaenda anakua na lugha chafu...kejeli. .dharau..matusi..na kunipiga na kuanzisha mahusiano nje. Mbaya zaidi hua anakuja kuniambia uchafu wote anaoufanya nje.

Alikua na kazi nzuri...lakin ikaisha kwasasabu ya kunidharau na kuchezea pesa na mwanawake wa nje ambae ilifikia mahala anampa simu yake anapokea.

Wakati anafanya yote hayo sikua na faraja na ndipo nilipoamua kutafuta mwanamme wa kuniliwaza nikiwa nimeshakata nae tamaa.

Soon mume alikuja na kunikuta na meseji ya huyo bwana na nikakili kua nina uhusiano nae. Mume wangu akanisamehe na nikamhaidi sitarudia tena lakin cha kushangaza anaenda kwa boss wangu kueleza yanayotokea nyumbani na kunitangaza kwa watu juu ya ugonjwa nilionao na mbaya zaidi bado anawasiliana na mwanamke wake mpaka muda huu. Na huyo mwanamke anapata kiburi cha kunikutaka na kunidharau na kunieleza madhaifu yangu ya magonjwa ambao ambayo mume wangu alimusimulia.

Nazidi kuumia zaidi nnapojua familia ya mme wangu inamfahamu huyo mwanamke wa nje na wanawasiliana na wifi zangu.

Wakati niko peke yangu nikifanya miradi ya maendeleo ambayo hata mume wangu alikua haijui....na iliniwezesha kujikimu kimaisha na mtoto wangu.

Sasa akarudi amerudi kwangu akiwa hana kazi...na akitaka kuanza maisha na mimi huku akisaidiwa mtaji wa biashara na ndugu zake ili tuweze kuishi kama familia.

Lakin mbaya zaidi..simu yangu yake..ya kwake yakwake...na anahisi bado nipo na mahusiano na yule mwanamme. Na hata ninapokwenda kwenye biashara zangu ananichunga na kuniwekewa mipaka ya kufanya kazi.

Akiwa kwangu...hatoi mahitaji wala kujishughulisha na chochote. Na anakua anaishi kwa kunitafutia sababu mpaka anataka kuniua. Hapa nilipo kanipiga sana mpaka nikapelekwa hospital.

Naombeni ushauri wenu ushauri. ..nataka nirudi kwetu na mtoto wangu nina kazi nina uwezo wa kufanya biashara..hapa nilipo nafatilia uhamisho.

ipo haja ya kuachana kwa sababu kwa maelezo yako haya inaonyesha wazi kabisa kwamba ndani ya ndoa yenu hakuna tunu ya kuheshimiana tokea mwanzo wa maisha yenu na hata kabla ya mahusiano yenu kiufupi utulivu zero
 
Haya bhana hata ukitubu maovu yako, there is still a price to pay. Remember David and Jonathan in the bible, Moses and God regarding striking the rock twice with pride, Moses confessed but he didn't enter the promised land. Stay with God and you will be blessed.:thumbup:
 
Tatizo lenu ni hayo mahusiano yenu ya nje. Kwa jinsi unavyoeleza inaonesha nyie hamuaminiani na hamko commited to ur relationship. Mara nyingi watu wanaotokatoka nje sana wanakuwa hawajiamini ndani so kutoka ni kama kunawapa emotional stability ambayo waliikosa kwa uvivu wao wakutokutafuta kuwaamini wenzi wao.

Hata kupigwa, kukosa kazi, starehe vyote vinaanzia huko. Wewe utaenda kwenu utaolewa na mwingine na yeye ataoa mwingine lakini ndoa zenu zitakuwa hivyohivyo.
What to do;

  • Ongea na mumeo nendeni kwa wataalamu wa mahusiano, hasahasa viongozi wa kiroho(kidini). Mkaungame dhambi zenu hasa ile kubwa ya kuvunja viapo vya ndoa yenu takatifu. Both of u have been hypocrites and untrustworthy for u breached u r marital contract

  • Mkaapiane upya, mjifunze kupendana upya, mjifunze kuwa waaminifu na pia mjifunze kuaminiana. Kisha muanze ndoa upya (Na msiache kwenda honeymoon).

  • Usitegemee kumbadili huyo mwanaume ndo utapata furaha. Shetani wako ni past yako and its always there to haunt u!
  • Kila la heri
 
kuwa kwenye ndoa yahitaji hekima na busara ya hali ya juu, hebu cheki mnavyo dhalilishana.

Mrudieni Mungu muanze upya maisha yenu ya ndoa Maana wote mu wachafu
 
swali imefunga ndoa rasmi au ndo kuzalishana na kujimilikisha undoa...? ushauri wewe ndiyo unayejua uchungu unaopata sasa maamuzi yapo kwako,... ila kama ni mimi kwa sabuabu kiuchumi hayupo vizuri nishampiga kapuni mda mrefu tu bila kujali chochote.................. mapenzi ya siwe kigezo cha kunipa karaha maisha yangu yote nisione raha ya maisha.....dharau lete mfukoni upo vizuri haina shida, unadharau alafu unapumulia mashine kwa kweli me siweziiii na Mungu Anisaidie nisipate mume wa ivyo amen
 
Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 30. Nina mtoto mmoja. Wakati wa usichana wangu...nilikua kicheche sana na niliishi maisha ya gharama sana na nilibahatika kupendwa na watu wengi sana wenye pesa na wasio na pesa....na ilifikia hatua nikaamua kuacha hayo mambo na kustick na mtu mmoja ambae alikua mwanafunzi wa chuo ambae nilikua nampenda na kuhisi atakua mume wa maisha yangu na ndie niliyezaa nae.

Niliamua kuokoka na kua na hofu ya Mungu. Sikutaka tena mahusiano ya nje. Kwasababu hakukua na kipya kwangu. Kama starehe nilishafanya sana.

Maisha yakaanza...mume wangu alikua ananipenda. Lakin kwasababu ya uzuri wangu wanamme hawajaacha kunisumbua kila leo natongozwa. Mume wangu anajua background yangu...na kwakweli amekua msaada mkubwa katika maisha yangu.

Ni mwanamme anayependa na mwenye matamanio mazuri katika maisha yetu. Kuna ugonjwa mkubwa umenipata na yeye hapo alikubali kua bega kwa bega na mimi mpaka mwisho.

Nikweli alikubaliana na hali yangu lakini kadri siku zinaenda anakua na lugha chafu...kejeli. .dharau..matusi..na kunipiga na kuanzisha mahusiano nje. Mbaya zaidi hua anakuja kuniambia uchafu wote anaoufanya nje.

Alikua na kazi nzuri...lakin ikaisha kwasasabu ya kunidharau na kuchezea pesa na mwanawake wa nje ambae ilifikia mahala anampa simu yake anapokea.

Wakati anafanya yote hayo sikua na faraja na ndipo nilipoamua kutafuta mwanamme wa kuniliwaza nikiwa nimeshakata nae tamaa.

Soon mume alikuja na kunikuta na meseji ya huyo bwana na nikakili kua nina uhusiano nae. Mume wangu akanisamehe na nikamhaidi sitarudia tena lakin cha kushangaza anaenda kwa boss wangu kueleza yanayotokea nyumbani na kunitangaza kwa watu juu ya ugonjwa nilionao na mbaya zaidi bado anawasiliana na mwanamke wake mpaka muda huu. Na huyo mwanamke anapata kiburi cha kunikutaka na kunidharau na kunieleza madhaifu yangu ya magonjwa ambao ambayo mume wangu alimusimulia.

Nazidi kuumia zaidi nnapojua familia ya mme wangu inamfahamu huyo mwanamke wa nje na wanawasiliana na wifi zangu.

Wakati niko peke yangu nikifanya miradi ya maendeleo ambayo hata mume wangu alikua haijui....na iliniwezesha kujikimu kimaisha na mtoto wangu.

Sasa akarudi amerudi kwangu akiwa hana kazi...na akitaka kuanza maisha na mimi huku akisaidiwa mtaji wa biashara na ndugu zake ili tuweze kuishi kama familia.

Lakin mbaya zaidi..simu yangu yake..ya kwake yakwake...na anahisi bado nipo na mahusiano na yule mwanamme. Na hata ninapokwenda kwenye biashara zangu ananichunga na kuniwekewa mipaka ya kufanya kazi.

Akiwa kwangu...hatoi mahitaji wala kujishughulisha na chochote. Na anakua anaishi kwa kunitafutia sababu mpaka anataka kuniua. Hapa nilipo kanipiga sana mpaka nikapelekwa hospital.

Naombeni ushauri wenu ushauri. ..nataka nirudi kwetu na mtoto wangu nina kazi nina uwezo wa kufanya biashara..hapa nilipo nafatilia uhamisho.
Dada umesema kwamba wewe ni mlokole, me ningekushauri kaombe ushauri kwa wachungaji wako, na wewe pia ukifanya maombi. hiyo ni kazi ya shetani na shetani atafurahi kuona umeshindwa na mimi naamini huwezi shindwa vita hii
 
Endelea kufuatilia uhamisho, wazo zuri. Kuwa mbali japo kwa muda mfupi kunaongeza heshima.
 
pole sana.........

na wewe utakuwa hujielewi,,,,,,,,,,,

unadai uliacha ukicheche kwasababu ya hofu ya mungu na huoni jipya lakini ukamegwa tena kisa mumeo anamega............. hii inaonesha hata wewe hujipendi.........

hapo hamna ndoa , ni mnaishi tu pamoja,,,,,,,,,,,,,, ukichukua background chafu + on and off history of cheating kwa pande zote........... halafu mmeanza kupeana madhara ya kimwili(kupigana) , bila kusahau mabadiliko ya tabia kumpelekea mmoja wenu mpaka kufukuzwa kazi, hapo kuna mushilization inakuja.

, mrudieni mungu mfanye toba na sala ya kunusuru ndoa yenu ikishindikana muachane, hamna namna.

umeshaniwahi nilichokua nataka kusema!!BIG LIKE
 
fafanua kuhusu afya yako, umetudokeza kuwa una ugonjwa, kuwa muungwana tuambie waumwa nini.
 
Ogopa sana malipizi, your past life haunts you! Ukiokoka lkn hukuwa delivered. Suluhisho la ugomvi wa ndoa si kuwa na kimada au buzi nje ya ndoa, ni sawa na kuwasha kiberiti kwenye petroli. Inawezekana huo ugonjwa ulionao unampa jamaa frustration. Uzuri unaoutaja hapo ni umbo lako na si tabia, ingekuwa tabia ndoa yenu ingekuwa yenye Furaha tele. Kuwa mwminifu kwanza wewe halafu utakuwa na kila sababu ya kumvutia mwenzio ktk kujirudi.
 
...kiukweli background itakuwa inakuhaunt tu, sasa kwa kuwa wewe dada uliona umechoka ukicheche ukaamua kutulia na kuolewa, inawezekana huyo mumeo naye alikuwa na bakgraund km ya kwako na kwamba bado muda wa kuacha ukicheche kwake haujafika, so mlipokutana wewe ushamaliza, mwenzako yeye bado, basi ni msala hadi hapo! nyie wote hamjatulia so mrudieni Mwenyezi Mungu na kuamze upya ila ikishindikana, basi u kol it kwit!
 
Back
Top Bottom