Nisaidieni connection za kazi au kibarua ndugu zangu

JOESKY

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
823
Reaction score
2,045
Habari za majukumu ndugu zangu wa jf?

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 mzaliwa wa wilaya ya kyela. ninaishi (mbeya mjini)

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu ngazi ya shahada ya kwanza ya elimu (BAEd) kutoka chuo kikuu cha Tumaini Makumira Arusha mwaka 2016. Nimetafuta kazi kwa bidii sana na nimefanya interview nyingi sana bahati haijawa upande wangu kabisa kwani nashindwa kufanikiwa kwa kila interview sababu kubwa ikiwa ni kukosa connection.

Interview ya mwisho nimefanya na taasisi moja hivi inajihusisha na mambo ya elimu tulianza watu 750 tukachujwa mpaka 112 ambapo ikanibidi kusafiri kutoka mkoani mbeya mpaka hapa dodoma kwa ajili ya interview ya mwisho ya kupata watu 36 nilijitahidi kadri ya uwezo wangu unfortunately sijui ni kigezo gani kilitumika kuniengua.

Nimefikiri sana na kuona kwamba kutafuta kazi ya kwenye career yangu itanifanya nishindwe kabisa kufanikiwa kwani kuna ugumu bila connection.

Naomba kwa wale mlio na connection ya hapa dodoma mnisaidie niweze kupata hata vibarua vya kwenye sites mbalimbali angalau niweze kuyamudu maisha hapa mjini.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Usikate tamaa mapema wengine toka 2012 bado tupo kitaa, tumeamua kujiajiri
Sijakata tamaa ndugu yangu natamani tu nipate pa kuanzia maana kujiajiri nimeshindwa kabisa shauri ya kukosa mtaji familia zenyewe zilitusomesha kwa kuuza mashamba yote
 
Habari za majukumu ndugu zangu wa jf?

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 mzaliwa wa wilaya ya kyela. ninaishi (mbeya mjini)

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu ngazi ya shahada ya kwanza ya elimu (BAEd) kutoka chuo kikuu cha Tumaini Makumira Arusha mwaka 2016. Nimetafuta kazi kwa bidii sana na nimefanya interview nyingi sana bahati haijawa upande wangu kabisa kwani nashindwa kufanikiwa kwa kila interview sababu kubwa ikiwa ni kukosa connection.

Interview ya mwisho nimefanya na taasisi moja hivi inajihusisha na mambo ya elimu tulianza watu 750 tukachujwa mpaka 112 ambapo ikanibidi kusafiri kutoka mkoani mbeya mpaka hapa dodoma kwa ajili ya interview ya mwisho ya kupata watu 36 nilijitahidi kadri ya uwezo wangu unfortunately sijui ni kigezo gani kilitumika kuniengua.

Nimefikiri sana na kuona kwamba kutafuta kazi ya kwenye career yangu itanifanya nishindwe kabisa kufanikiwa kwani kuna ugumu bila connection.

Naomba kwa wale mlio na connection ya hapa dodoma mnisaidie niweze kupata hata vibarua vya kwenye sites mbalimbali angalau niweze kuyamudu maisha hapa mjini.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Unaweza kufanya kazi ya sales and marketing?
 
Back
Top Bottom