Nisaidieni! Je, hizi ni dalili za ugonjwa gani!?

Nisaidieni! Je, hizi ni dalili za ugonjwa gani!?

Babchabi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
1,745
Reaction score
777
Wakati nipo na miaka 13 nilishawahi kupata Kisonono (Kichocho), wakati huo ilikua tunaogelea sana katika mito michafu. Ila sasa tuko watu wazima.

Jana niliamka na homa baada ya kujisikia temperature inapanda nikavuta Paracetamol ya 1000 mg nikapiga homa ikashuka ila baada ya masaa 4 huanza kurejea.

Hii paracetamol nilitumia mara 3 kwa siku, cha ajabu kuamkia leo ikawa naenda haja ndogo mara kwa mara na tena huwa mkojo unanibana sana kiasi kwamba hata kujizuia nashindwa. Wakati nakojoa huwa najisikia kichomi kwa mbali, sio sana, ila baya zaidi mwishoni mwa mkojo hua natokwa na damu kama vile kisonono.

Mimi niko na wife na nashukuru kwamba sina mpango wa kutembea na hawara nje na pia mwenzangu namuamini, ushauri wenu tafadhali.
 
kisonono na kichocho ni vitu viwili tofauti pia kama nikichocho paracetamol sio dawa yake nenda hospital wafanye examination ndio tatizo lako litajulikana na dawa utapewa
 
aaah ok ahsante mkuu kwa fikra zangu nilifikiri kichocho ndio kisonono ok nimeshaenda hospital nimepeleka mkojo nimeambiwa nifate majibu after 2days
 
kisonono n ugonjwa wa znaa mkuu na je ultibiwa? na kama hukutibiwa vzur na kupona hayo ndo madhara yake!!fka kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
 
Majibu ya kweli yako kwa matabibu, tafadhali nenda hospitali upate uhakika.
 
aaah ok ahsante mkuu kwa fikra zangu nilifikiri kichocho ndio kisonono ok nimeshaenda hospital nimepeleka mkojo nimeambiwa nifate majibu after 2days

huo mkojo 2 days wanafanya culture?
 
Kisonono ni ugonjwa wa ugonjwa wa zinaa. Dalili za kisonono ni kukojoa usaha na mkojo kuuma. Usipotibiwa njia ya mkojo inaweza kuziba.

Kichocho kinapatikana kwa kuogelea kwenye maji yenye konokono. Dalili zake ni mkojo kuuma na kukojoa mjojo wenye damu mwisho. Usipotibiwa kichocho waweza kupata saratani ya kifuko cha mkojo.

Nahisi una kichocho sugu ulichokipata utotoni. Fanya hima utibiwe.
 
UTI ni ugonjwa nadra kwa mwanaume labda awe na matatizo ya kuziba njia ya mkojo au tezi dume.

Wanaume wanapata sana UTI, na kwa kudharau dalili za mwanzo huwainakomaa na kufikia kukojoa damu/mkojo wenye damu! main courses kwa wanaume ni vyoo vya kukaa vya ofisini.
 
Tayari naendelea na matibabu dokta ameniandikia dawa nimezipiga damu imekata huu ugonjwa unasababisha na figo dokta kanishauri niwe nakunywa maji kila wakati na niende kufanya cheking ya figo kama ziko poa magonjwa ni mengi wakuu mii nashukuru sijawahi kutumia kilevi chochote toka mdogo hadi saivi.
 
huo mkojo 2 days wanafanya culture?
Mkuu dokta wa kweli ni yule anaeangalia maradhi na kukupa majibu ya uhakika huo mkojo unachunguuzwa maradhi yote ulionayo sasa wee unaona 2days ni nyingi ulitaka dakika 30 upewe majibu tayari nimeshaenda kuchukua majibu ile siku ya mwanzo kabisa dokta aliniandikia dawa kuzipiga asubuhi jioni ilikata kaniandikia vipimo vyengine niende kufanya xray ya figo.
 
mkuu dokta wa kweli ni yule anaeangalia maradhi na kukupa majibu ya uhakika huo mkojo unachunguuzwa maradhi yote ulionayo sasa wee unaona 2days ni nyingi ulitaka dakika 30 upewe majibu tayari nimeshaenda kuchukua majibu ile siku ya mwanzo kabisa dokta aliniandikia dawa kuzipiga asubuhi jioni ilikata kaniandikia vipimo vyengine niende kufanya xray ya figo

xray ya figo?
 
Kukojoa damu ni dalili ya kichocho. Wakati mwinginge tunategemea mtu kukojoa damu kama amekuwa involved kwenye ajali na some of the internal organs like kidneys zimekuwa involved, kwa wewe fanya culture ya mkojo then utajua nini kinakusumbua.
 
Kimbia hospitali ukapimwe, hayo magonjwa ukichelewa athari zake ni kubwa sana
Tayari nishamuona dokta na tayari natumia dawa na kesho nina appointment ya cheking, Mungu anijaalie aniepushe na maradhi sugu.
 
Back
Top Bottom