Nisaidieni Jinsi ya kupata marafiki

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
Wakuu salama,
Natumai MUNGU amewaamsha salama na tuko katika mapambano ya maisha! Kwa wale wagonjwa MUNGU awape wepesi mpone haraka.

Wakuu nimekuja kwenu nina shida moja naamini vichwa humu mtanisaidia, mimi ni mtu ambaye sina marafiki wale wa kusema tunapigiana simu weekend hii wapi etc! Sina hata yule rafiki wa karibu wa kubadilishana mawazo etc.

Hata nikitoka weekend nitaenda bar/beach nakaa tu alone nakunywa beer, naangalia labda mpira narudi home kuungana na wife na familia.

Nahitaji kuanzisha marafiki, nisaidieni mbinu za kupata marafiki wapya etc.
 
1: lengo la urafiki ni nini?
Kula bata, story tu, kupigana tafu kushibana katika shida na raha??

2: Baada ya hapo juu, aina zake sasa kama ni wa bata utawapata batani bar, huko beach etc kama ni wa kuchat tu hapa jf tupo.

3: Mkeo ndio rafiki ako

4: toa wasifu wako marafiki zako tuje na tukugande....
 
Hili wazo liondoe kichwani...dunia ya sasa kupata rafiki wa kueleweka ni kujidanganya... Kama una mtoto/watoto wako hao ndiyo rafiki wako wa uhakika hapa duniani...
Wengine wafanye washkaji zako tu wa kupiga nao stories 2,3 ila usiwategemee kwenye kila jambo au eti watakuja kukusaidia au kua na wewe kwenye shida na raha ni uongo, ni Mungu pekee ndo rafiki wa kuaminika wakati wote kwenye nyakati ambazo hata hutegemei anakushika mkono na kukufariji..
Urafiki wa sasa hivi wapo ki maslahi zaidi, friendship with benefits..
 
Mke? Nae sio rafiki wa kuaminika ni swala la muda tu nalo 😂😂
 
ndo nahitaji hao wa kupiga story mbili tatu mkuu
 
kupiga story kdg, bata kdg, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…