Nisaidieni Jinsi ya kupata marafiki

Nisaidieni Jinsi ya kupata marafiki

Wakuu salama,
Natumai MUNGU amewaamsha salama na tuko katika mapambano ya maisha! Kwa wale wagonjwa MUNGU awape wepesi mpone haraka.

Wakuu nimekuja kwenu nina shida moja naamini vichwa humu mtanisaidia, mimi ni mtu ambaye sina marafiki wale wa kusema tunapigiana simu weekend hii wapi etc! Sina hata yule rafiki wa karibu wa kubadilishana mawazo etc.

Hata nikitoka weekend nitaenda bar/beach nakaa tu alone nakunywa beer, naangalia labda mpira narudi home kuungana na wife na familia.

Nahitaji kuanzisha marafiki, nisaidieni mbinu za kupata marafiki wapya etc.
Mfanye mkeo awe rafiki yako
 
huyu tayari ni rfk
Basi ndo uwe una hang out nae ,kuhusu kusaidiana kwenye matatizo ni vizuri ukajiunga kwenye vikundi mbalimbali hapo mtaani kwenu au kanisani mana sehemu kama hzo huwa wanachangishana ela za kusaidiana na pia huwa wanashikana mikono kwenye shida
 
asante sana mkuu kwa ushauri
 
fafanua mkuu na yako hapa utapata msaada!kuna watu wa maana humu kukupa ushauri
Mkuu mimi nina shida hii ya kutokuwa/kutokupata marafiki kama wengne unakuta wadau wanapiga stor na kuchekelea mimi nashindwa na mbaya zaidi ni kwamba naona ni sawa kabisa muda mwing nakuwa home au ntaenda mahala najua hakuna watu ni chill binafsi naiona kuwa abnomality...
 
Hilo tatizo halijaanza ukubwani lazima ni tangu ukiwa mtoto kuna hatua ambayo mtoto anakuwa na uwezo wa kujichanya na wenzake na kutengeneza marafiki .Lakini marafiki hawatafutwi wanakuja wenyewe tu.
 
Fact mkuu, marafiki wanajileta.
 
Back
Top Bottom