Nisaidieni kuwaelewa Wakenya!

Hahahahaha. Which wealth are you talking about. Tell me which properties do you own in your own country?
At 28yrs I have 17acres and By age 40 I should be Having 300 acres. What do you have and what are your future plans?
 
Halafu haya makelele ya lugha mbona Watanzania huwa hawawapigii majirani zao wengine, huwa wako obsessed na Kenya tu.
Afrika Kusini ambayo Watanzania hupenda kuwashobokea wale wanaongea lugha 12 kama lugha zao rasmi, na ni vigumu kumpata Msouth anaongea zote kwa ufasaha. Hata mataifa mengne yaliowazunguka hakuna waliofungiwa kwenye lugha moja kama wao, wote wanaongea lugha tofauti.

Tatizo la Watanzania ni kwamba tumewashinda kwenye Kingereza, hili huwa linawauma sana na kuna wachache wameanza kupokea Kingereza. Ukiwa Bongo unakuta familia za walionacho wanaongelesha watoto wao Kingereza, lakini saint Kayumba walalahoi wanadanganywa wabaki kwenye Kiswahili eti ndio uzalendo. Likija suala la interview na nafasi za ajira, matangazo yanasema lazima mhusika awe na uwezo wa kuongea Kingereza, sasa saint kayumba wengi hawawezi, wanaishia na ze ze ze huku udenda ukiwatoka kama mazezeta.

Ni muhimu sana kuwa na uwezo wa kuongea lugha kadhaa, watoto wangu wanaongea lugha zao za asili yaani Kikikuyu, Kiluhya na pia wanajifunza Kijaluo na Kikamba. Zaidi ya hapo wanaongea hizi za kuja kama Kiswahili, Kingereza na shuleni wanafundisha Kifaransa. Mtoto anakua mjanja wa lugha na inawaboresha sana na kupanua uwezo wao wa kutumia akili sio kufungiwa kwenye lugha moja kama mbuzi.
 
Acha kujiliwaza wewe, ukiondoa South Afrika ambayo kutokana na watawala wao waliwachanganyia lugha, na katika jambo kubwa lilowafanya wapingane na makaburu ni kuwalazimisha watu weusi watumie lugha ya africana katika shule zao, hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya migomo mashuleni yaliyopelekea mauaji ya Soweto, kukataa lugha ya wakoloni wao, nchi zingine zote zina lugha moja ambayo ndiyo lugha yao ya taifa, kwa mfano Zambia ni English, Burundi ni kirundi na lugha ya pili ni kifaransa, lakini shughuli zote za serikali ni kwa kirundi, Rwanda ni Kinyarwanda, ya pili siku hizi ni English, shughuli zote za Serikali ni kinyarwanda

Tatizo lenu ni kwamba Kenya kama ilivyo Tanzania, tumebahatika kuwa na lugha yetu indeginous ambayo sio ya kabila moja kama ilivyo Ethiopia, tena inazungumzwa na watu wengi barani Afrika ya watu weusi kuliko lugha yoyote nyingine, tena Kenya imeichagua kuwa lugha ya taifa lake, iweje mshindwe kuitumia katika shughuli za serikali sehemu kubwa mnatumia lugha ya mabwana zenu, kwanini msitumie na pesa za mabwana zenu kama kigezo ni kuweza kuwa global?, huo ni utumwa wa hali ya juu sana, hata hao mabwana zenu wengine ambao kiingereza sio lugha yao ya taifa kama Norway, German na Holland, wanatumia lugha zao na kiingereza ni lugha ya pili kama ilivyo kwa Tanzania

Sent from my MediaPad T1 8.0 using JamiiForums mobile app
 
https://www.facebook.com/
Msikilize huyu Professor toka Nigeria, hawa ndiyo watu walioelimika
 

Hamna kitu, nyie tatizo lenu kubwa mpo wazembe sana, mumeshindwa kujifunza kuongea Kingereza.
Kenya hakuna mtu asiye elewa Kiswahili, labda kama anaishi kwenye shimo, pili Kingereza kinafundishwa kuanzia chekechea, hivyo hata watu wa kijijini kabisa kule mashinani hata kama hawakiongei, lakini wanakielewa na ukikuta mtu hakielewi Kenya, basi hakuenda shule kabisa na huyo kwa hotuba ya rais hata ikihutubiwa kwa Kiswahili haitamfaidi.

Bahati nzuri ni kwamba, Kenya tunaenzi sana lugha zetu za asili hivyo baadaye hotuba hudadavuliwa kwenye taarifa za habari vijijini kwa lugha za asili.

Tofauti kabisa na kwenu, unakuta mtu amefika kidato cha nne lakini Kingereza hakielewi kabisa, halafu kuna wengi mumefika vyuo vikuu lakini mkiambiwa mjieleze kwa Kingereza mnaishia kuuma uma midomo na kupata jazba. Mnajifanya kutunisha misuli wakati mumeshindwa kukwepa Kingereza maana hampo industrialized, hivyo kila kitu mnaishia kuagiza na vinakuja na maelezo ya Kingereza.

Mataifa yote yaliyowazunguka wanatumia lugha zaidi ya moja, nyie mumefungiwa na kujidanganya. Na mara nyingi hata hiyo moja huwashinda, maana wengi wenu hata humu mna uandishi wa kiajabu. Sasa Kingereza hamkijui, lugha zenu za asili mlishazitelekeza, Kiswahili chenyewe kipo bado sana kwenye matumizi ya kisasa, hakijaiva iapasavyo na pia nyie hampo sawa kwenye uandshi wake.
 
Lengo kuu la lugha yoyote ya taifa ni kuwaunganisha wanainchi wa Taifa husika kuwa kitu kimoja, ukiona nchi haina lugha moja inayoeleweka pakubwa na wananchi walio wengi, basi kuna uwezekano mkubwa nchi hiyo isiewe na umoja wa kitaifa ikaishie kwenye mgawanyiko mkubwa na hizo lugha zikawa zinatumika kama mipaka, mfano ni south Afrika, Nigeria, Cameroon, Belgium, Canada, Kenya, na nyinginezo.
Ni mtu mwendawazimu pekee anayeweza kusema eti kuna baadhi ya watu katika nchi yao ambao hotuba za rais hazimsaidii kwasababu haelewi lugha inayotumiwa na rais, ni kichaa peke yake anayeweza kusema eti hotuba baadae zinatafsiriwa katika lugha mbalimbali ili wale ambao hawakumuelewa rais waelewe, je kama rais alienda kuhutubia katika eneo hilo na huyo mwananchi alihudhurua huo mkutano wa hadhara ataelewaje?

Kama kawaida unakataa ukweli ili kuhalalisha tribalism yenu iliyokomaa na kutishia uhai wa nchi yenu, kuendekeza lugha za asili katika maeneo ya mijini na ofisini ni sababu muhimu sana ya watu kutambuana na kubaguana kwa misingi ya ukabila, kutotumia lugha moja ya taifa, tena kudharau lugha yenye asili ya nchi yenu ni dalili ya utumwa wa mawazo na fikra, huyo professor toka Nigeria amelizungumza vizuri sana, nani asiyejua kwamba Kenya ni vibaraka wa wazungu?, Africa yote inafahamu ni kwa jinsi gani Kenya ilivyosaliti nchi za Afrika wakati wa harakati za ukombozi

Kenya mtaendelea kubaguana kwa misingi ya ukabila, mtaendelea kuchinjana kwa misingi ya ukabila na mwisho nchi itasambaratika kama ambavyo tayari sehemu za Kenya zilivyoanza mchakato wa kujitenga, wakati mataifa duniani yanaipongeza Tanzania kwa kuitumia lugha ya Kiswahili katika kumaliza ukabila na kuleta umoja wa kitaifa, ninyi bado unaendekeza ukaidi na sifa za kijinga, sasa kama nchi zote unazosema zimetuzunguka zinazungumza lugha nyingi, ni ipi kati ya hizo ambayo imefanikiwa kumaliza ukabila kama Tanzania?
 

Nimejaribu kusoma ulichokiandika nikakosa mantiki, kama kawaida kutumia maneno mengi ili kusema nothing hadi unanipotezea muda nikisoma riwaya yote.
Lengo kuu la lugha ni kuelewana, useme ueleweke na kama kuna wasiokuelewa itafsiriwe kwa hao. Lakini tutaendelea kutumia Kingereza zaidi yenu maana uzembe wenu umewafanya mbaki kwenye kugha moja wakati majirani zenu wote wamejiboresha kwenye matumizi ya lugha zaidi ya moja.
 
Huwezi kupata mantiki katika maandishi yangu mengi yaliyotukuka, sababu kubwa ni your personal ego, unadhani itakuwa fedheha kwako kukubali kwamba Kenya ilifanya na inaendelea kufanya kosa la msingi kwa kutokipa umuhimu lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo lugha yake ya taifa na ni lugha ya kiafrika asilia badala yake kuthamini kiingereza lugha ya wakolon.

Ufahamu fika kwamba, hata kama mtu ni adui yako, lakini kama ndiye daktari mwenye uwezo wa kutibu ugonjwa wako huna budi kumwendea na kumsikiliza. Katika hili la lugha, Kenya lazima muige Tanzania vile ilivyotumia lugha ya kiswahili katika kupambana na ukabila na kujenga umoja wa kitaifa, kinyume na hapo Kenya inasambaratika
 
Kenya hata mtu wa darasa la kwanza anajua Kizungu
 
Asilimia kubwa ni kiarabu, kama Waarabu hawangekuja kubaka Waafrika hakingebuniwa.
Tatizo mliiga hadi uzembe wa Waarabu na Uswahili mwingi.

kwa hiyo Kenya inaizidi maendeleo Oman na Dubai au UAE kwa ujumla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…