Nisaidieni, najihisi kabisa nimepewa limbwata

Inafikirisha Sana jinsi unavyoharibu pesa na ndoa yako kisa ngono za single mother .

Huyo alichokifanya hajakuroga ila amekutenganisha hauna utulivu wa Mwili , roho na nafsi mtu makini hawezi kutoa pesa zake kwa singo maza na kuua ndoa yake.

Unaweza fanya meditation ili kuanza kutengeneza muunganiko wako wa kiakili roho Mwili na nafsi.
 
Anayelogwa huwa anajua?
Kuna length unajua.. Mimi Nilihisi kuwa siko normal dhidi ya yule Single Mother but nikawa nachukulia poa . siku zilivyoenda nikaambiwa na msaidizi wa mganga wake.
Huyu msaidizi ndiye anagawa Dawa kwa wagonjwa baada ya kupata maelekezo toka kwa mganga Mkuu.

It was like "kumbe wewe ndiye unadate na fulani?mwenzio anakuzidi ujanja!!".
 
Mkuu langu mim ni balaa, nimecha familia sasa nakaa na kimada. Sijui mwanangu anakula nini, ndugu pande zote wamenitenga na eti hata siwataki wala kuona umuhimu wao. Mpaka mama yangu mzazi namkwepa na simu sipokei. Limbwata lipo
 
Wangu kanifanya Pimbi, sifanikiwa mpaka wale wa shilling ngapi au vp unaelekea mbezi nikupe lift
 
Pole sana aisee. Ndio changamoto zakuchepuka hizo bora ungebaki njia kuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…