Nisaidieni nakonda

Nisaidieni nakonda

mramba

Member
Joined
Jul 23, 2009
Posts
30
Reaction score
2
Mimi mwenzenu ni mwanachuo wa chuo fulani nachukua fani ya utabibu degree hapa Tanzania, nilitokea kumpenda dada mmoja zaidi ya miaka minne iliyopita na kwa kuwa sikuwahi kuwa na mpenzi hapo kwanza kwa sababu zangu binafsi sikuchelewa kumweleza lililonisibu moyoni.
Yule dada wakati huo wote tukiwa form five alinikatalia kwa madai kwamba yeye anasoma kwanza ndo mambo kama hayo yaje baadaye(tulikuwa shule tofauti wakati huo ila nyumbani wilaya moja). Nilikubaliana naye kwa kumsisitiza kwamba bado ataendelea kuwa moyoni mwangu na sitaweza kumpenda mwingine. Baada tu ya kumaliza form 6 niliendelea kumsumbua kuhusu hilo na akashikilia msimamo wake kwa mba haamini wanaume hivyo nimwache kwanza achukue bachelor yake hayo mambo kwake anaamini yana muda wake tu. Kwa kweli kwa nilivyompenda yule mrembo niliendelea kumsisitizia suala hilo na kujitahidi kuwasiliana naye mara kwa mara kwani tulikuwa mikoa tofauti. Yeye hakufanya vizurikwenye masomo yake hali iliyopelekea abadili mchepuo toka sayansi na kwenda arts kwa mwaka mmoja an alipofanya mtihani alifanya vizuri hivyo kujiunga na chuo kikuu fulani pale mji kasoro bahari.
Nimekuwa nikimsisitizia huyo dada kuhusu mapenzi yangu kwake pamoja na kumsaidia kwa mambo madogomadogo kwa matumaini ipo siku atabadili msimamo wake, ila cha ajabu wajameni ni mpaka leo hii msimamo wake upo vilevile kwa madai kwamba nyumbani ndiye pekee aliyesoma hivyo wanamtegemea sana hataki kuwaangusha kwa kuanza mapenzi kabla hajamaliza na vilevile alishawhi kuwa na jamaa huko akiwa o'level na jamaa akampa kibuti hivyo hawaamini tena wanaume eti anaogopa wanaweza kumfanya akafeli chuo bure halafu akawaangusha nyumbani kwake.
sasa wapenwa huyu dada nimemfia kinoma na sijawahi kuona kama yeye ktk maisha yangu yote, Nimejaribu ku-tune my mind set otherwise but i completely failed. NIFANYEJE??
 
Kama unampenda msubiri amalize chuo. Haraka ya nini? Mbona bado mko vijana sana? Subiri bana!
 
Vumilia tu ndugu yangu kama unampenda kweli na yeye ameshikilia msimamo wake huo. But ni vizuri ukajua msimamo wake juu yako kama kuna dalili zozote mapenzi juu yako ili usije ukapoteza muda wako mwingi na mali bure. Tafuta muda mzuri mfungie safari maalumu muombe mkutane sehemu nzuri tulivu then mkae muongee kwa mapana na marefu ili upate uhakika. Akikuhakikishia kuwa nafasi yako ipo ila wapaswa kusubiri basi fanya hivyo, ila usikubali kurudi bila kupata jibu la uhakika, kiukweli inauma sana kumpenda asiyekupenda.
 
Ha ha ha haaaa

puppy love............

Hebu jaribu kuwa na msichana mwingine
na hakikisha na yeye anajua......utaniambia.........
 
pole kakangu ila mimi naamini huyo mdada hakupendi!
kwani anaekupenda hata akiwa hajawa tayari kutoka na wewe kimapenzi anakuwa anakujali nakukupa moyo....unaona upendo wake waizwazi kwa matendo wala hakupi hofu hadi kufikia stage hiyo ya kuwa na wasiwasi!
jaribu kumpotezea kwa muda uone kama atastuka....akitulia jua hakupendi raha ya mapenzi mpendane sio upende wewe tu!
amini mwanamke sio yeye tu atatokea mwingine utampenda nae atakubabaikia kichizi hadi utaona utamu wa mapenzi!
ukiendelea kusubiri nahofia atakuumiza zaidi.....utasikia anaolewa au ana mimba!
 
........Mimi nina mashaka na upendo wa huyo msichana kwako, kipindi alivyokuwa secondary kweli mapenzi yangemchanganya na masomo.
Ila sasa hivi yupo chuo na haonyeshi dalili yoyote ya upendo kwako............mhhhhhhhhhhh!! Shtuka hapo mkaka isijekuwa ana mtu mwingine wewe anakuyeyusha tu maana ndio zetu baadhi ya wasichana.

Hivyo wewe unaweza kumjua vizuri kama kweli anakupenda ila masomo ya chuo ndio kikwazo au hata dalili ya kukupenda hana ila anakupiga tarehe tu.
 
Ha ha ha haaaa

puppy love............

Hebu jaribu kuwa na msichana mwingine
na hakikisha na yeye anajua......utaniambia.........

ushauri mzuri sana, huyu jamaa anafuga bonge la bomu, wakidada wa chuo, uliza kwanza uambiwe, we subiri mziki utauona
 
pole kakangu ila mimi naamini huyo mdada hakupendi!
kwani anaekupenda hata akiwa hajawa tayari kutoka na wewe kimapenzi anakuwa anakujali nakukupa moyo....unaona upendo wake waizwazi kwa matendo wala hakupi hofu hadi kufikia stage hiyo ya kuwa na wasiwasi!
jaribu kumpotezea kwa muda uone kama atastuka....akitulia jua hakupendi raha ya mapenzi mpendane sio upende wewe tu!
amini mwanamke sio yeye tu atatokea mwingine utampenda nae atakubabaikia kichizi hadi utaona utamu wa mapenzi!
ukiendelea kusubiri nahofia atakuumiza zaidi.....utasikia anaolewa au ana mimba!

........Mimi nina mashaka na upendo wa huyo msichana kwako, kipindi alivyokuwa secondary kweli mapenzi yangemchanganya na masomo.
Ila sasa hivi yupo chuo na haonyeshi dalili yoyote ya upendo kwako............mhhhhhhhhhhh!! Shtuka hapo mkaka isijekuwa ana mtu mwingine wewe anakuyeyusha tu maana ndio zetu baadhi ya wasichana.

Hivyo wewe unaweza kumjua vizuri kama kweli anakupenda ila masomo ya chuo ndio kikwazo au hata dalili ya kukupenda hana ila anakupiga tarehe tu.

Hapo ni wewe tu unapenda ye hakupendi utaumia tu cut your losses and MOVE ON!
tafadhali pokeeni makofi kutoka kwenye avatar yangu. hii ndio ushauri , hapo hakuna mapenzi wala babu yake mapenzi. kijana kuwa mwanaume ,songa mbele. acha kukonda wakati mwenzako anaondoka na ugali na samaki bila kujali feelings zako .
:closed_2:! tunaomba mada nyengine kama ipo.
 
Mvumilivu hula mbivu,keep on kuvumilia,utazivuna mbivu muda si mrefu :A S 8::A S 8::A S 8::A S 8:
 
kaka mbona unafunga mada wakati mie nilikuwa na mchango hebu ngoja niutoe hivyo hivyo

PIGA CHINI MARA MOJA ANAKUPOTEZEA MUDA TU TAFUTA DEMU MWINGINE UENDELEZE MALAVIDAVI NAE
 
Mvumilivu hula mbivu,keep on kuvumilia,utazivuna mbivu muda si mrefu :A S 8::A S 8::A S 8::A S 8:

:becky::becky::becky: Anaweza akavumilia mwishowe akavuna zilizooza hapa inaonyesha huyu msichana hayuko willing haiwezekani all that time tokea sekondari mpaka chuo sasa binti hataki kuelewa somo mimi namshauri huyo kijana atune mind yake somewhere else asije bure akapata vidonda vya tumbo huku mwenzako yeye anaendeleza libeneke lake wala she doesn't even care about your feelings
 
Inawezekana kabisa kua huyo dada hana mtu mwingine ila tu hajataka kuipa akili yake mda wa kufikiria kuhusu mapenzi.
Tena anatoa sababu kabisa kua anategemewa nyumbani na hataki kuwa-dissapoint ndugu na wazazi wake.

Historia ya maisha yangu ya mapenzi ina fanana sana ya ya huyo binti, sikutaka kabisa kujihusisha na mapenzi nikiwa shule, nilianza semister ya mwisho ya mwisho ya masomo yangu na sasa ni mama na nina familia yangu.

Huyo dada hataki kutoa commitment zozote sasa maana hataki kuishirikisha akili yake ktk mambo ya mapenzi. Cha msingi huyo kaka amuulize ni lini atakua tayari kujihusisha na mapenzi, halafu huyo kaka apime mwenyewe kutokea hapo.

Hii hali inatokea sana inategemea tu na malezi, mazingira aliyokulia na imani za kidini.
 
Ukicheza na nyani, utavuna mabua kaka. Umri wa chuo mtu anaweza kuchangua mbivu au mbichi. Anakuvunga huyo.
 
Pole sana inavyoonyesha binti hana mapenzi kwako ..Kama angekuwa anakupenda angekupa ushirikiana na kukuonyesha kuwa anakupenda sana ila hayuko tayari kujihusisha na mapenzi mpaka hapo malengo yake yatakapotimia
 
Ha ha ha haaaa

puppy love............

Hebu jaribu kuwa na msichana mwingine
na hakikisha na yeye anajua......utaniambia.........

Mawazo yako ni mazuri lakin mh!...... Yeye kampenda huyu akianza na mwingine tena wakati anampenda yule basi ni mwazo wa kujifunza
Kuzichanga karata mbovu na sijui kama ataishia hapo.
Ujue huo ni Uchuzi uanweza usizeeke!

Kuwa Mvumilivu na umwombe Mungu, anaweza kuwa chaguo lako au siye na mwisho wa siku ukapata Msichana mzuri wa kukufaa.

Ndoa siyo mambo ya kchagua kama purchases zingine. Be careful!
 
ebu kua na wewe HAKUPENDI WALA HAKUTAKI KABISA yan km vp mpotezee mapema usijitie huzuni kwa ONE DAY YES .....eeh eehhh ma braza m telling u the yrs ur watng for ha iz enaf nw .take ye way take ur way oooooooooooohh thr no lov o waitng tym apo
uyo ana kajamaa kengine ndo anakapenda na anafanya nae maisha we bakia kushika pembe tu kwa iman ipo siku ntanyonya!!
tumia akili yako ya kuzaliwa tenma utumie ile ya darasa la tatu ata usiisumbue ya darasa la 5 utajua..thk thk yhk kwa akili changafu..........HAUPENDWI sor tosay so!!!!!!!!!
jipindishe kunako kona nyngne utampata mwngne ambaye aujawai kui=mwona km yeye!!!!!!!11
ahh ahh kakangu umenchekesha eti....... sijawahi kuona kama yeye ktk maisha yangu yote,...hahaha ana nin uyo? pembe usoni? au ana gia visiginon?ebu achana na utoto bwana b realistc utampata mwngne

pole kaka yangu we r ol watoto watoto bt wewe umezid kidg kwaiyo puppy love yako mmh apana

achana na izo mashairi nyanyuka smama life z too shot uskubali kinyangaruka flani kibane mtiririko wa furaha yako wkt ye uko anakula tu gud tym...uskubali iyo verse iimbike kwako
tafuta mwngne replace oda then life goes on!~!!!!!!!!!!!
 
kalaghabaho na Ubozi wako!!Muda haukusubiri!!! lala mbele!! kama wako atajuja
 
Huu labda ni woga wa kutongoza?? Unamngoja mtu asiyekua na taim na wewe??
 
Back
Top Bottom