Nisaidieni nifanye biashara gani? Nina mtaji wa 3,000,000/=, nipo Himo-Moshi

Nisaidieni nifanye biashara gani? Nina mtaji wa 3,000,000/=, nipo Himo-Moshi

tcha hapo himo panalipa.nunua ndizi kwa reja reja vijijini,nenda kauze kwa jumla pale MWIKA kila jumanne na ijumaa.inalipa sana.au fungua mgahawa hapo njia panda.uwe unauza soup asubuhi mchana msosi jioni makongoro kwa kuwa upo moshi weka ndani angalau kret1 ya soda za cocacola na nyingine ya bia serengeti.ukishindwa kabisa fungua genge hapo mbele ya kituo cha police holili.mia

Kaka ni bora ukafanya Biashara ya usafirishaji wa vitu ambavyo unaweza ukapata kwa bei nafuu na kuuza kwa bei nzuri mikoa yenye shida na huduma kama izo na bidhaa hizo ziwe ni zile zisioharibika upesi kama nyanya,maembe n.k!.na hii inahitaji business research!,no blah blah kwa hili...na kama utakuwa na tatzo la kusafiri kutokana na kazi yako ya ualimu unaweza ukafungua sehem za kuuza vifaa vya simu kama makava,chajiz,vochaz,usb kablez,betries,ukanunua na kompyuta ya kuingizia nyimbo n.j..ni biashara ambayo haiozi ila chagua sehem nzur yenye wakaz weng kidogo au fungua gamez play station kama sehem inawatoto wengi...haina haja ya kumpa m2 kukutengenezea buznes plan u can do it on your own...JIPANGE!

ticha, nenda kilacha hapo chuo cha mifugo kafungue cafe upige biashara ya misosi kwa wanachuo. Au kama vp nenda marangu pale t.t.c kuna wanachuo zaid ya 1000 na hawana huduma ya stationary mpaka marangu mtoni, ww nenda katege pale pale chuo.
Ila be care na mabinti wacje wakakufilisi.

Mkuu usisahau ku factor in issue zingine kwa mfano...upatikanaji wa mvua, u need to value na hilo shamba (kwa case yako umeassume jamaa tayari ana shamba lililo idle), gharama za usimamizi mpaka utakapovuna, usafiri na storage n.k n.k.

So kwa ushauri wangu, unahitaji kufanya upembuzi wa kutosha kabla hujaamua biashara gani ufanye. kwa maana hiyo Business Plan (Andiko la Mradi) kwa biashara yoyote ile ni muhimu sana.

Kuanzisha biashara si sawa na radio unayonunua dukani na ku plug and play.

Kama utahitaji kutayarishiwa Business Plan kwa gharama nafuu usisite kuwasiliana na mimi (just PM me).

Biashara matangazo..

ticha, nenda kilacha hapo chuo cha mifugo kafungue cafe upige biashara ya misosi kwa wanachuo. Au kama vp nenda marangu pale t.t.c kuna wanachuo zaid ya 1000 na hawana huduma ya stationary mpaka marangu mtoni, ww nenda katege pale pale chuo.
Ila be care na mabinti wacje wakakufilisi.

Ukipata mtu mzuri kwenye msosi inalipa sana.

nenda same ulime tangawizi acha na na ujinga wa kuuza maji ,pipi,unga its a risk hata wapuuz can take ,hii ndani ya mwaka umetusua

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO

GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 240,000/-
Vibarua 250,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 150,000/-
Jumla 640,000/-
MAPATO:
Kilo 20,000 X300 =6,000,000/-
Unatumia mbinu gani kuhakikisha unapata kilo 300 kwa heka? na hizo tangawizi zinatumia muda gani kati ya kupanda na kuvuna?

Tunatoka dar na milion 2.5 kupeleka mahindi kenya weewe una 3 unashindwa nini ongea na wazee wa kati ama wakuu wa polisi saizi ya kati wakupe mbinu

wewe umesema ni mwalimu sasa utafundisha watotoz wetu saa ngapi nasema acha tabia ya kudharau ualimu kwa maana ualimu ni wito au wenyewe wanasema public service yaani ni kazi yenye thawabu mbele ya Sir God kwa hiyo mimi nakushauri hizo senti ulizonazo andaa tuition center utatoka kuliko kuwaza biashara mbali na kazi yako utakutana na wapigaji utalizwa

kaka naona wewe ni mtu ambaye ni vissionary, kwa hiyo akili ulotumia kupata pesa hiyo , akili hiyo hiyo ikuongoze kuanzisha biashara.

Kwanza tujuze jinsi ulivyoweza kupata 3m. Isije kuwa ndiyo michango ya madawati tunayotoa!

egbert na mtanzania nyie watu mna laana mjue,so mwalimu yeye haruhusiwi kufanya biashara nyingine (kwa maisha haya yasiyo mthamini hata chembe) ye aendelee tu kupiga chafya na chaki...au akiwa na fedha zake basi kaiba michango ya wazazi au lazima azitolee maelezo ya kina...mtazamo huu ndo unafanya watu waikimbie hiyo fani

bora umwambie maana huyo naona hapendi maendeleo ya tcha kabisa

Mwalimu nakushauri ufuge kuku wa mayai, kwa kuwa utakuwa na muda wa kutosha kuwacheki asubuhi mchana na jioni.

kama ujawahi fuga kabisa nenda kwa bwn mifugo anza na kuku 200 au chini ya hapo, utahitaji.

banda, 200@3,000 600,000

vifaranga 200@2500 = 500,000

vifaa vinginenyo 120,000

jumla 1,220,000

baada ya miezi 4-5 wataanza kutaga mayai 180 kwa siku.

Mauzo ya mayai tray 180 kwa mwezi @5000 900,000

Chakula cha kuku bags13 ya kg50@33,000 525,000

Madawa na mengineyo 50,000

Faida kwa mwezi 325,000.

then faida mpaka wamalize kutaga mayai 2,600,000 miezi 8 had 12 ivi.

jaribu apo ticha, my queen does that. for any question you are welcome

Hiyo nimeipenda imetulia sana

wewe umesema ni mwalimu sasa utafundisha watotoz wetu saa ngapi nasema acha tabia ya kudharau ualimu kwa maana ualimu ni wito au wenyewe wanasema public service yaani ni kazi yenye thawabu mbele ya Sir God kwa hiyo mimi nakushauri hizo senti ulizonazo andaa tuition center utatoka kuliko kuwaza biashara mbali na kazi yako utakutana na wapigaji utalizwa

Hoja nzuri sana. Maoni hayo hapingani na nia ya Mwalimu kuanzisha biashara. Mwalimu ni vema akaangalia biashara ambayo inaendana na kazi yake na hapo kutakuwa na ufanisi mzuri wa utendaji wake vinginevyo atashtukia ameegemea upande mmoja kama hajafanya upembuzi wa kutosha.

Naungana na egbert44 bora mwalimu angefungua kituo cha Tuition cha kisasa ambacho kinaweza kuwa na mvuto kwake, au kuanzisha shule ya chekechea ni miradi inayoendana na taaluma yake.

kuna Gomboro usisahau inaua kuku bila huruma.

maisha ni mapambano hata iyo gomoro inaua kuku ili iishi, kwa iyo ww ili uishi lazima uimalize iyo gomoro kwanza kabla haija kudo!

ingia hapo kikavu piga vitunguu maji vya umwagiliaji utanipa majibu after3 month

Back
Top Bottom