Nisaidieni tofauti ya Mwanasheria na Wakili

Nisaidieni tofauti ya Mwanasheria na Wakili

SODOKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,656
Reaction score
722
wa JF naombeni mwenye kujua iyo tofaut ya mwanasheria na wakili anijuze
 
Hata wewe waweza kuwa mwanasheria ukisoma sheria kwa ngazi ya shahada,lakini wakili mbali na kupata shahada sharti uende shule ya sheria usome mwaka mmoja ndio upate sifa ya kuwa wakili.
 
Hazina maana sawa na ndio sababu kuna majina tofauti
Tutofautishie mkuu, uko kwenye sheria mi sijui kwa sababu watu hawa huwa nashindwa kuwaelewa namna wanavyofanya kazi.
Kwanza kitendo cha kumtetea mharifu na kusimama mbele za watu akimuita mwarifu kwamba ni mteja wake ... hapo ndo huwa nashindwa kuwaelewa. Kitu kingine wana ubishi usiokuwa na maana hata mitaani.
 
Mwanasheria (Lawyer) ni mtu aliyesomea taaluma ya sheria na wakili (attorney) ni mwanasheria anayetumia taaluma hiyo kuwatetea watu kwenye mashauri mbalimbali katika mahakama ngazi yoyote ile!

So you have to be a lawyer for you to be an attorney right?

All attorneys are lawyers but vice versa is not true
 
Mawakili wote ni wanasheria ila si wanasheria wote ni mawakili,mwanasheria ni yeyote aliyesomea sheria katika ngazi yoyote iwe certificate, diploma,nk ingawa hawezi kuipractise popote lakini wakili ni mtu ambaye jina lake lipo katika registry ya mawakili,inayomwezesha kupata muhuli na hivyo kuweza kuipractise anywhere.ili kuwa wakili ni lazima uwe na bachelor au zaidi na pia lazima upitie law school
 
Back
Top Bottom