Nisaidieni, umasikini wa familia unanitatiza

Nisaidieni, umasikini wa familia unanitatiza

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,494
Reaction score
2,540
Wakuu habari zenu,

Naomba usiache kuchangia kwenye uzi huu ili niweze kupata msaada wa kukabili changamoto nazopitia.

Case yangu iko hivi: Nina uhitaji wa kiasi cha pesa kisichopungua milioni 30. Pesa hii sina uwezo wa kuipata kwa pamoja based on my job monthly income.

Lakini Kuna sense of urgency pesa hii inahitajika ili kutatua pressing needy inayoikabili familia yangu. (Mniwie radhi sitatoa details za issue yenyewe coz ninao ndugu na jamaa humu JF wasije ona nauvua nguo hadharani ukoo wangu)

Uharaka wa kuipata pesa hii umenifikisha bank kadhaa kuangalia kama naweza pata kiasi hiki cha pesa. Hata hivyo nimeishia kuchanganyikiwa tu coz inatakiwa niwe na pesa ya marejesho isiyopungua kiasi cha laki 6.7 kwa muda wa miaka Saba. Yaani unakopa milioni 32 unarudisha milioni 54.

Mbaya zaidi pesa hii tunayohiitaji ni totally for consumption and liability . Yaani sio ya kuzalisha (not for investimate) ila itatuondolea haibu na kumfanya mzazi wangu niliye naye ajisikie vizuri na ku appreciate uzao wa tumbo lake)

Situation inakua tough coz mimi binafsi nahitaji pesa kama nusu ya hiyo ili kuboresha maisha yangu hapa mjini. Kuna mambo niko nyuma sana ukijilinganisha na mate wenzangu wenye status sawa hali inayopelekea kuninyima confidence and ending up being confused and frustrated.

Wakuu katika situation kama hii

Unazani ni sahii kuchukua mkopo umiza utakaonitesa for seven years?

Je, ni wapi napoweza pata pesa bila riba kubwa? (Ninaweza jicommite kiasi cha laki 5 kila mwezi ili nirudishe principal loarn)

Je, katika situation hii kipi kiwe kipaumbele kurejesha tabasamu kwa mzazi na fame ya familia au nijiokoe mwenyewe kwanza?

Wenye uzoefu wa maisha tafadhari usiache kutoa msaada wako wa kimawazo.

Karibuni wakuu
 
Kwanza pole. Binafsi naamini maisha ni sasa ya kesho anajua muumba we jilipue tu chukua mzigo huo solve ishu zako.

Kudaiwa inadaiwa serikali ya Mama Samia na bado inaendelea kukopa.

Utanisamehe kama nimejibu kitu kilichokukwaza maana na mimi nina stress zangu za madeni na nipo kwenye harakati ya kumkopa mtu m1
 
USIKOPE!

- Hauhitaji pesa kwaajili ya kuwekeza, wewe unahitaji pesa kwaajili ya matumizi. Siku ukimaliza hayo matumizi, utaumia zaidi na marejesho badala ya kupata nafuu. Kopa kwaajili ya kuwekeza au kwa matumizi ya lazima, sio matumizi ya muhimu!

- Kama unaweza kutenga laki tano kwa mwezi kwaajili ya kulipa marejesho ya mkopo, kwanini usiitumie hiyo laki tano kutatua hiyo shida taratibu? With good management, unaweza kufanya kitu kikubwa kwa hatua ndogo ndogo kwa kutumia hiyo laki tano ya kila mwezi na ukabaki kua loan free!

- Acha kujilinganisha na watu wengine. Unajipatia stress zisizo za lazima kwa kujilinganisha na watu ambao hamlingani majukumu, kipato au hata background. Usione watu wanaishi vizuri mjini hapa kaka, kuna mengi nyuma ya pazia. Stay on your godamn lane. Cha msingi ni kupiga hatua hata kama ni taratibu. Being better than yesterday is more than enough!

- kujicommit kwenye mkopo ambao sio kwaajili ya kuwekeza, kwa miaka saba ni hatari. Vipi ukipata shida nyingine hapo katikati? Vipi kuhusu emergency za kila siku? Breaking out of the poverty circle is not a simple thing. Kuna wakati inakubidi upuuzie baadhi ya shida, ili uweze kujipanga na upambane nazo ukiwa tayari.

Peace be upon you!
 
Unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuacha kujilinganisha maisha yako na hao uliowaita 'Mate wenzako" ishi maisha yako kwa kipato chako huku ukiendelea kutafuta,usishindane na watu ambao huna hata idea ya njia wanazopitia wao mpaka kufika hapo walipo.
 
1. "mimi binafsi nahitaji pesa Kama nusu ya hiyo ili kuboresha maisha yangu hapa mjini. Kuna mambo niko nyuma sana ukijilinganisha na mate wenzangu wenye status sawa hali inayopelekea kuninyima confidence and ending up being confused and frustrated."

2. "kipi kiwe kipaumbele kurejesha tabasamu kwa mzazi na fame ya familia"

Kulingana na hizo kauli mbili hapo juu nachoweza kukushauri usichukue mkopo kabisa maana utajikuta unatengeneza matatizo zaidi ya hayo uliyokuwa nayo mwanzo. Kwenye haya maisha usipende kujilinganisha na wengine maana kila mtu anapitia changamoto zake hao workmate wenzako unaweza kuona wako mbali pengine hawana changamoto kama unazozipitia wewe ndo mana wako hapo walipo, Ukijaribu kuishi kwa kuangalia wengine utaishi na stress zako mpaka kufa kwako.

Kengine kwenye familia yenu naamini mpo wengi kama ni changamoto ya mzazi basi ni vyema hiyo inshu mkaibeba pamoja kama wanafamilia kuona mtaitatuaje ili ujipunguzie mzigo Usijaribu kufanya maamuzi ya peke yako ili uonekane shujaa.
 
Pole sana mkuu,ninapitia changamoto kama kama yako,nafikiri unahitaji kumjengea mzazi wako nyumba nzuri,na wewe mwenyewe uwe na nyumba nzuri lakini usitumie nguvu kubwa kuwafurahisha wazazi wako.

Tafuta pesa taratibu,lakini usijiingize kwenye MIKOPO,ukijiingiza kwenye mikopo utachangachanyikiwa zaidi,utakuwa na mikopo mikubwa stress unakuwa nazo za kulipa madeni ya mikopo.

Ukikopa utaishia maisha magumu sana kuliko sasa,achana na mikopo mikubwa ili kuwafurahisha wazazi wako,tafuta pesa taratibu usijiweka kwenye mtego zaidi wa ugumu wa maisha kwa kujiingiza kwenye madeni
 
Usikope pesa kwa ajili ya kuifurahisha familia yako. Tupo tuliofanya hivyo, not only that we were not appreciated but it never brought any change. Na hiyo itafanya waone kuwa una pesa nyingi na utatwisha mizigo mingi.

Rome was not built in a day or a year. It took time. Kaa na mzazi wako, zungumza naye mweleze uhalisia wa kipato chako.

Wajibu wako ni kwa wazazi, mkeo na watoto na wazazi wa mkeo ikiwa hawana wa kuwasaidia, but nawe ni kijna wao unapaswa kuwaangalia. Wengine wote ni mizigo, they will never appreciate you, ukiwaendekeza watakuona kama shamba la kuvuna, na mwisho watakucheka.

Find happiness in what you earn and let them know you are strugling. Usijibebeshe mizigo.

Kama ni kukopa, kopa. anzisha biashara, faida inayotokana na biashara hiyo ndiyo utamsupport mzazi na kubadilisha mazingira ya mzazi taratibu.
 
Kwanza pole. Binafsi naamini maisha ni sasa ya kesho anajua muumba we jilipue tu chukua mzigo huo solve ishu zako.

Kudaiwa inadaiwa serikali ya Mama Samia na bado inaendelea kukopa.

Utanisamehe kama nimejibu kitu kilichokukwaza maana na mimi nina stress zangu za madeni na nipo kwenye harakati ya kumkopa mtu m1
Asante kwa ushauri
 
USIKOPE!

- Hauhitaji pesa kwaajili ya kuwekeza, wewe unahitaji pesa kwaajili ya matumizi. Siku ukimaliza hayo matumizi, utaumia zaidi na marejesho badala ya kupata nafuu. Kopa kwaajili ya kuwekeza au kwa matumizi ya lazima, sio matumizi ya muhimu!
...
Asante mkuu. Nitajitahidi kuzingatia ushauri wako
 
Unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuacha kujilinganisha maisha yako na hao uliowaita 'Mate wenzako" ishi maisha yako kwa kipato chako huku ukiendelea kutafuta,usishindane na watu ambao huna hata idea ya njia wanazopitia wao mpaka kufika hapo walipo.
Noted brother
 
1. "mimi binafsi nahitaji pesa Kama nusu ya hiyo ili kuboresha maisha yangu hapa mjini. Kuna mambo niko nyuma sana ukijilinganisha na mate wenzangu wenye status sawa hali inayopelekea kuninyima confidence and ending up being confused and frustrated...
Asante kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom