Nisaidieni, umasikini wa familia unanitatiza

Its almost there
 
Asante kwa ushauri
 
Noted with thanks
 
Mkuu, Kwanza pole kwa whatever unachokipitiia, ila firkiri kwa undani zaidi, kukopa milioni 32, kugharamia 'aibu' na 'hadhi' kama kuna thamani sawa na mateso utakayoyapitia kipindi chote cha mrejesho wa huo mkopo!

Ni bora ujinyime kwa kusave kiasi fulani cha fedha , yuje kukimiza malego maana mpaka unayafikia, walau utakuwa kuna mafunzo na discipline umejijengea kuliko hicho unachokiwaza!
 
I tried this nilipokuwa kijana na nikafeli miserably,

Kama nakuona unavofeli, hasa kuanzisha biashara halafu ndugu aiendeshe (baba, mama, kaka, dada), itafeli tu hamna namna.

Achana na mawazo hayo, ww jichukulie mkopo wa 4yrs (maximum) which is around 18M,anzisha biashara yako ( small but utakayoweza imudu) then each month wape wazee, familia yako maximum of 20% ya mabaki ya mshahara wako, then wewe sustain for remaining salary na business yako.

Msisitizo, anzisha biashara utakayoisimamia mwenyewe, ya kusimamia mtu itafeli hata kama huyo mtu ni babaako
 
Mkuu ukiishi kwa kufurahisha watu hautakaa uje uwe na furaha ya kweli. Utaishia tu kuwa mtumwa. Cha msingi ninachoweza kukushauri, jaribu kuwa na shukrani kwa kidogo ulicho nacho Mungu naye atakuongezea. Vitu vizuri vinatake time, na lengo kubwa la kupambana ni kuwa na uwezo wa kifedha siyo kuonekana una uwezo wa kifedha.
 
Its almost there
Hawa wazazi wetu muda mwingine huwa wanatuangusha sana, unakuta anakopa kimyakimya bila kukutaarifu, siku marejesho yakikwama ndio unaona simu ukiwabana kuwauliza pesa mliyokopa mmefanyia nini wanabaki wanakuangalia tu..

Ila mkuu kama umri wa wazazi umeenda na unaona kabisa wanaweza kwenda kupumzika kijijini nakushauri itisha kikao cha familia nyumba wanayokaa sasa hivi hapo mjini ipigwe bei, lipa madeni hao wazazi wako wakiwa kijijini huko utakuwa unawatumia fedha za matumizi kila mwisho wa mwezi ila hili la kukopa naona ukiangua kilio hata kabla ya miaka saba (7) kuisha.
 
Banks Siyo Rafiki Wa Masikini, Usipojipanga Utapangwa
Kuongea Ni Rahisi Kazi Kutenda
Unataka Kwakuwa Una Kazi Family Yako Na Kwenu Kuwa Kama Ulaya. Ukikopa Ujue Dhamana Yako Ikifail Majembe Auction Mart Hao Mlangoni Utadhalilishwa Utajua


Tulia Ulivyo Tumia Kidogo Taratibu
 
Ndugu.....

Huo umasikini kama babu wa babu yako hakuumaliza....

Babu yako hakuumaliza....

Baba yako hakuumaliza......


Badala ya kuhangaika kujitia umasikini hebu ulichonacho save, invest.....pambana utoke huko.

Mzazi atakuelewa tu.

Huwezi beba dunia....

Usijibebeshe mzigo usiouweza.......

Pampja na haja ya kuitoa familia hapo ilipo...kuwa na kiasi
 
Good Summary
 
Homeboy kwanza pole sana kwa changamoto iliyokukuta kwanza haupo peke yako .tatizo vijana wengi wa kiafrika hasa sisi watanzania sio wabunifu yaani hatujui kujiongeza ndio maaana tunaanguka nisikuchoshe homeboy . Homeboy maisha yako tena rahisi sana ukiwambunifu ushauri wangu kwanini usiwe mkulima wa bustani ukadili na Kilimo cha mbogamboga Nyanya ,pili hoho kichaaa, Bamia nk au ukadili na kilimo cha msimu mahindi ,ufuta ,choroko ,maharage nk . Kuliko homeboy kwenda benki kuchakua pesa nyingi kiasi kama hiko ni nyingi sana hiyo .homeboy kilimo kinalipa usiende benki hiyo pesa itakugharimu hapo baadae
 
Nakuhakikishia una jipu lililoiva huna budi kulitumbua,,,Usipolitumbua litakutesa milele achana na mabahili wa kigoma nenda benki kachukue pesa kama ni kumjengea mzazi fanya hivyo huo mzigo uondoe, usije dondoka ghafla ukaenda na mawazo yako kaburini binadamu tunakatika ghafla xana,,,chukua mkopo tekeleza lengo nakuhakikishia hutajuta maana utakuwa na amani ya ndani pale unapoona wazazi wako sehemu nzuri ambayo umeiweka wewe.Binafsi nlkw kama wewe nikachukua maamuzi na sijawahi kujuta,,,kuna watu wana laana wako mjini wanatumbua maisha wakati wazazi wananyeshewa huko kijijini,,

Kumbuka mshahara haujengi hasa kwa watu waliotoka katk familia zenye changamoto
 
Naimba nihitimishe(maana utapata ushauri mwingi mwisho iwe miruzi mingi.....)
WALE WOTE MLIOSEMA AKOPE KWA AJILI YA KUZALISHA MPO SAHIHI SANA!
Tuanze kuangalia msingi wa hoja yake,
ni jwamba akope ili kuondoa fedheha! hili ni wazo zuri,ni vizuri kuondoa unyonge na uduni.
TUPANUE MAWAZO SASA:
Je,yeye anao uwezo wa kuondoa hali hiyo inayomkera,NDIYO!
1.Inaonesha anaomshahara mkubwa.
Basi akope,lakini kwa ajili ya kukuza kipate na katika faida basi aitumie kutatua changamoto nyinginezo.
CHANGAMOTO:
1.Inaonesha hana uzoefu na kazi za ziada,lakini anapenda maisha mazuri(au ya kati)
UTATUZI:
Tafuta watu wakufanyie kazi,lakini wewe uwe ubavuni mwao katika kazi(ya ziada) utakayochagua.
Nihitimishe na mfano mmoja:
Mshahara usio na support ya kipato cha ziada ni sawa na pipa lenye mrija mmoja wa kuingiza maji lakini upande mwingine lina mipira mitano ya kutoa maji,je pipa hilo litajaa kweli??
 
You're godamn Smart Ghost.
 
Comments yenye maneno machache sana ila imejitosheleza,good advice
 
Kopa hela peleka kansani to a sadaka ya kujikomboa tafuta Madhabau yenye nguvu mtakua mmekombolewa Pesa hazita kuendesha we utaziendasha Pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…