Niseme nisiseme? Watoto kufundishwa ulawiti huko Kilimanjaro kosa ni la Serikali

Niseme nisiseme? Watoto kufundishwa ulawiti huko Kilimanjaro kosa ni la Serikali

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Shule zinazotumia mitaala ya nje lkn zinasajiliwa hapa nchini na serikali yetu zinaongezeka kila uchwao.

Lakini cha kushangaza ni kwamba waliopewa dhamana ya kutoa usajil kwa shule hizo (wizara ya elimu) hawajisumbui kukagua kwa undani kilichomo ndani ya mitaala hiyo.

Kilichotokea Kilimanjaro wala siyo kosa la walimu wa shule husika. Walimu wanafundisha kinachopaswa kufundishwa ambacho kimeelekezwa na mtaala. Na mtaala huo umeruhusiwa na serikali kupitia wizara ya elimu. Sasa kosa la walimu liko wapi?

Kama kuna kosa basi wa kwanza kuwajibishwa waitwe ni waziri wa elimu na timu yake, waziri wa jinsia na timu yake pamoja na waziri wa mambo ya ndani na timu yake.

Wasitufanyie maigizo ya kufanya vikao vya dharura kuonesha kwamba wanachapa kazi. No! No! No! Waondoke!
 
Kuna walakini, aliyelalamika hakuripoti popote zaidi ya JF, kamuona mwanae anamfundisha mtoto wa jirani, kakauka kama vile sikitu... nikomashaka .... mtoto wa miaka 9 kumfundisha mwenzie inamaanisha kashakuwa tarumbeta, halafu unapotea kimya kimya, maisha yanaendelea kama kawaida???!! huyu mzazi gani?tusaidiane wana JF.
 
Na mzazi Hana time ya kukaa na moto kumuuliza yanayojiri huko shuleni kila mhula ukiisha. Tupo bize na maisha.
 
hili lingetokea pwani hili dunia ingesimama wallah...
 
Na mzazi Hana time ya kukaa na moto kumuuliza yanayojiri huko shuleni kila mhula ukiisha. Tupo bize na maisha.
Wengi wanaosoma shule hizo ni watoto wa watu wazito siyo walala hoi. Shule zinazotumia mitaala ya nje ada yake kwa mwaka inanunua IST mbili.

Lkn pamoja na kulipa ada yote hiyo mtoto anaishia kufundishwa ulawiti.

Ama kweli, pesa huharibu kizazi (generation)
 
Kuna mmarangu mmoja amemuoa shoga kutoka zanzibar.
Eti na yeye anamfungia ndani kama mwanamke duh!..nihatari.
 
Wengi wanaosoma shule hizo ni watoto wa watu wazito siyo walala hoi. Shule zinazotumia mitaala ya nje ada yake kwa mwaka inanunua IST mbili.

Lkn pamoja na kulipa ada yote hiyo mtoto anaishia kufundishwa ulawiti.

Ama kweli, pesa huharibu kizazi (generation)
Mkuuu kwakweli nisiwe muongo hii habari sijaiona naomba unielekeze nikaione na mm ni video au walipost mahali?
 
Pwani wana uzoefu wa kutosha,hiyo elimu ndiyo kwanza inapelekwa huko moshi.
Fuatilia mashoga wakubwa wanatokea wapi mpaka kijana aliyeolewa then uje hapa ...Achana na porojo hakuna huo ujinga ni tetesi tu.
 
Mkuuu kwakweli nisiwe muongo hii habari sijaiona naomba unielekeze nikaione na mm ni video au walipost mahali?
Gazeti la Nipashe la j3 ama j4 lilikuwa na habari hii na ndiyo ilikuwa habari kubwa kuliko zote.

Na hata humu JF ilipostiwa
 
Back
Top Bottom