Nishati Safi ya Kupikia: Kupata Kipato kutoka kwenye Carbon Credit kwa kuhakikisha wananchi wanapikia nishati safi

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kutokana na Kampeni za Mazingira na kuhakikisha nchi haziendelei kuharibu Dunia yetu, Kuna kiwango fulani ambacho kimewekwa katika viwanda (hususan katika nchi zinazotoa / zalisha sana Carbon) kwamba wasizidi kiasi fulani.

Sasa kuna nchi kama Tanzania yenye misitu na haizalishi sana Carbon inaweza kuwauzia hivyo viwanda (wazalishaji wa carbon) ili kiwango chao cha kuchafua kiongezeke (kama uchafuzi wao umezidi, hivyo wanaweza kununua credit kutoka pengine na mwisho wa siku kuonekana kwamba wapo within kiwango)

Sasa kutokana na Ushauri wangu wa hapo nyuma ambapo nilionyesha kwamba kwa nchi yetu moja ya Nishati safi kabisa ni Umeme

Na nikaongezea kwamba Tanesco inaweza kuingia ubia na wazalishaji vifaa vya umeme (majiko) na kuwauzia watu kwa ruzuku ili waweze kutumia


MAPATO ZAIDI (TANESCO / UMMA / WATANZANIA) WANAVYOWEZA KUPATA KUTOKANA NA NISHATI SAFI

Sasa utaona kwamba kutokana na TANESCO / WATANZANIA kuweza kuwauzia watu hivi vifaa vya kupikia watakuwa wame offset kwa kiasi kikubwa sana Carbon Emmissions, hivyo kuwa certified kama mpunguzaji mkubwa wa CARBON, hivyo kwa kuuza hizo Credit itakuwa ni njia mojawapo ya kupata Kipato ambacho kinaweza kusaidia katika Ruzuku za kuwapa watu majiko.

Tuanzia Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza
 
Sijaelewa hapa.
 
Sijaelewa hapa.
Hata wewe kama una misitu ya kutosha unaweza kuisajili na kupata documentation kwamba una Hekari kadhaa za miti..., kwa kawaida miti inatumia carbon dioxide na maji kwenye mwanga wa jua kufanya photosynthesis na hivyo ndio mimea inajipatia chakula chake
6CO2 + 6H2O → C6H12O6 + 6O2
Na kwa kufanya hivyo tunajipatia sisi oxygen na maisha yanaendelea bila shida..., Tatizo uzalishaji wa carbon dioxide kutoka kwenye vyanzo vingi umekuwa mwingi kuliko hata mimea inavyoweza kutumia carbon dioxide. Carbon Dioxide kwenye atmosphere ina trap heat...

Carbon dioxide in the atmosphere warms the planet, causing climate change. Human activities have raised the atmosphere’s carbon dioxide content by 50% in less than 200 years.
Kwa mataifa na dunia kwa ujumla kuona hili wameanza kuhakikisha watu hawaharibu mazingira kwa kuongeza kutengeneza carbon dioxide, ndio maana kuna motisha ya kutumia magari ya umeme, kuacha kutumia vitu kama mkaa n.k.

Sasa wewe ambaye una miti yako na inanyonya carbon dioxide sio haki kwako kuendelea kuharibiwa dunia yako na watu wengine wanaochafua..., hivyo kupewa motisha kuendelea kutunza miti na kwa wale wanaochafua kuacha kuchafua wanaweza kununua kwako ile credit kutoka kwako (wewe ambaye hauchafui) na wakiweka kwenye vitabu vyao itaonekana uchafuzi wao ni minus usafishaji uliofanya wewe (miti yako) wewe utapata pesa na wao wataendelea kuchafua bila fine ya kuvuka kiwango walichowekewa...
 
wakiinunua kwangu si itakuwa haipo au nawauzia ile excess?
 
wakiinunua kwangu si itakuwa haipo au nawauzia ile excess?
Hii ni theoretical, kwahio hata wewe ukiuza au usipouza bado miti yako itakuwa inakula carbon dioxide na maji na kutengeneza starch (wanga) na oxygen...; 6CO2 + 6H2O → C6H12O6 + 6O2, Na wanaochafua huenda wakashindwa kuendelea kuchafua sababu wataonekana wamevuka kile kiwango walichowekewa

Hivyo wewe kama wewe una bidhaa ambayo wao wanahitaji, kwahio hapo kuna fursa ambayo unaweza kuiweka sokoni ili uweze kulipwa..., Na hio ndio hata sasa hivi Tanzania tunatumie misitu yetu na kuna pesa inaingia... (Kwahio wewe unachouza ni wingi / ukubwa wa misitu sababu unaweza kusema msitu huu unakula Tonne kadhaa za Carbon Dioxide)


 
naona kama ni njia ya nchi zilizoendelea kukwepa uwajibikaji
 
naona kama ni njia ya nji zilizoendelea kukwepa uwajibikaji
Naam ndio maana yake ila ndio hivyo bora hata vijisenti wawape wale ambao hawachafui kuliko wao kuendelea kuchafua na kutuharibia dunia wote (wao na sisi); Ingawa shida hata hizo pesa taifa linazopata sioni zinatusaidia nini zaidi ya kuishia kwenye matumbo ya watu...

Nadhani cha maana wangekatazwa kuchafua na sio vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…