Dunia ndivyo ilivyo watu wenye pesa zao ndio wanaowaweka watoa maamuzi na wanaoamua kwenye madaraka au waamuzi pia wana hisa kwenye mambo mengi yanayofanyika..., hivyo mimi sikatai wanufaike ila wanufaike pale ambapo na wananchi na Taifa litanufaika....
Kuhusu gesi asilia ya Mtwara ni kama nilivyosema..., hii ili iwe practically njia moja ya kufanya huwa ni kuweka mabomba kutoka inapotoka mpaka inafika / tumika (ni kama Russia ana bomba kutoka huko kwao mpaka sehemu nyingi za Europe...
Sasa kutandaza hizo pipe sio mzaha na kwanini tutandaze pipe mpaka mlimani kwa bibi na babu fulani wakati hao wote wana umeme unawafikia ? Utaona kwamba njia rahisi ni kupeleka pipe mpaka sehemu chache ili nishati hio ya gesi asilia iweze kuchemsha maji ya kuendeshea turbines na kutengeneza umeme ili umeme huo upitie kwenye nyanya na kumfikia babu na bibi mlimani ili waweze kupika kitoweo chao....
Mbaya zaidi hata raia hatuna information yaani tumewaachia watu ndio watuamulie na wafikiri kwa niaba yetu bila kuhoji kwahio hata tukiambiwa kibaya ndio kizuri au hiki ndio kizuri zaidi hatuwezi kubisha zaidi ya kukubali..., kwahio cha maana ni kupata taarifa sahihi ili tukifanya maamuzi yawe ni ya manufaa..., pia hata hao big boys wanaweza kuwekeza kwenye vifaa vya umeme, (kutengeneza, ku-assemble na kuagiza) itakuwa ni raia wenzetu wananufaika na sio hii LPG ambayo tunanufaisha mataifa mengine pia...., na kupanda kwake kwa bei hatuna say yoyote...
Kuzalisha Biogas hata sasa hivi wewe haukatazwi unaweza ukaishi off-grid na kupikia kutumia samadi ya mifugo yako, tena hapo utakuwa unaishi sustainably.., lakini kwa nchi yetu nina uhakika umeme ukishuka sana (jambo ambalo linawezekana kabisa) kwanini mtu aangaike na kushughulika na vinyesi wakati akibonyeza tu switch baada ya muda ubwabwa umeiva...