Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

Kwanza nakupongeza mleta hoja. Ni mada nzuri na umeieleza kwa wepesi hata mwananchi wa kawaida anaielewa.

Pili, nakuunga mkono kuwa kati ya nishati zote zinazotajwa katika mazingira ya kitanzania ni umeme ndio nishati safi na nafuu na inayopatikana maeneo mengi ya nchi yetu.

Binafsi, hizo nishati ulizozielezea zote nimeishazitumia na nimeamua kubaki na nishati moja ya umeme wa Tanesco
ambayo kwangu (nina familia ya watu 7) naona ni nafuu sana nikilinganisha na nishati nyingine maana kwa mwezi natumia wastani wa Tshs 25,000/ kununua umeme na unanitosheleza kwa matumizi yote ya umeme ikiwemo mwanga, jokofu, kunyoosha nguo, TV, radio, kusaga matunda na kupikia. Jiko la umeme ninalotumia ni la teknolojia ya Kijerumani linatumia umeme kidogo ukilinganisha na majiko ya umeme ya kizamani au ya kichina.

Mtungi wa gas upo kwa ajili ya dharura umeme unapokatika. Kwa hiyo nami nashauri serikali yetu ielekeze nguvu kuhakikisha inasambaza miundo mbinu ya umeme maeneo yote ya nchi yetu hasa vijijini na iweke ruzuku kwenye majiko haya ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu gharama yake kwani mimi nilinunua jiko hilo mwaka 2022 kwa bei ya Tshs 290,000/ badala ya kupigia chapuo biashara ya gas (LPG) ambayo ni miradi inayonufaisha nchi za kigeni inakozalishwa gas kuliko nchi yetu.
 
Tatizo kubwa la serikali ya ccm wanachoangalia kwenye kila mradi wao watapata nini sio nchi wala wananchi watapata nini
Tayari kwenye hili wafanyabiashara wa gesi ambao wengine ni makada wa ccm wameshachora mchoro wa kupiga pesa ndefu wakishirikiana na wanasiasa waliopo madarakani.
 
Siku wakigoma ghafla kutusuply gas tunakula vibichi.
Hawawezi kugoma sababu tunawapa dollar (kwahio pesa za kununua vitu vingine tunatumia kununua kitu ambacho tunacho) na kila siku tunalalamika dollar ikipanda maisha yanapanda kumbe ni sisi wenyewe tunapenda utegemezi (au kwa uhalisia wachache wanatuumiza wengi ili wao wafaidike)
 
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati ambazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeiweka mwisho sababu ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri, na hili linaweza kufanikiwa ikiwa tutafanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.


Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.

NB: Ushauri wa kuachana na LPG (Mitungi ya Gesi ya Sasa Majumbani) itaacha wengi ambao ndio Biashara yao kwenye hasara ila kwa kurekebisha hilo Serikali inaweza kushauriana nao au kuwawezesha kwa mikopo wawekeze kwenye matengenezo na marekebisho ya vifaa vya Umeme; kwahio badala ya kuagiza majiko kutoka nje assembly plants zinaweza zikawa nchini jambo ambalo litakuza ajira na kuwapa wigo waliopo kwenye biashara ya LPG kunufaika na Umeme - Badala ya Mihan, Oryx, Taifa gesi tutakuwa na Mihan, Oryx, Taifa Cookers
Akili kubwa hii.

Mkuu naomba dondoo kidogo kuhusu gas asilia kwenye vinyesi.

Kuna utaalamu gani masinki ya vyoo kuweza kutoa nishati ya kupikia?
 
Akili kubwa hii.

Mkuu naomba dondoo kidogo kuhusu gas asilia kwenye vinyesi.

Kuna utaalamu gani masinki ya vyoo kuweza kutoa nishati ya kupikia?
Ni kwamba Kinyesi kinavyooza kinatoa ile gesi methane sasa ujazo wa Methane hio hadi uwe wa kutosha kukufanya wewe uweze kupika labda utumie mifugo au sehemu ambapo wanashusha mzigo mwingi
feedstock.jpg
Ukiona hapo juu Ng'ombe mmoja anaweza kushusha mzigo mwingi zaidi na anatoa Gesi nyingi zaidi kuliko Binadamu yaani Ng'ombe mmoja ni kama binadamu 16... lakini kama una magereza unaweza kutumia mzigo wa wafungwa na hii ishafanyika hata Malawi...

malawi biogas.jpg
 
Ni kwamba Kinyesi kinavyooza kinatoa ile gesi methane sasa ujazo wa Methane hio hadi uwe wa kutosha kukufanya wewe uweze kupika labda utumie mifugo au sehemu ambapo wanashusha mzigo mwingi
Ukiona hapo juu Ng'ombe mmoja anaweza kushusha mzigo mwingi zaidi na anatoa Gesi nyingi zaidi kuliko Binadamu yaani Ng'ombe mmoja ni kama binadamu 16... lakini kama una magereza unaweza kutumia mzigo wa wafungwa na hii ishafanyika hata Malawi...

Mkuu ahsante kwa kunitoa tongo tongo.

Swali nililouliza, pamojana takwimu uloambatisha, limekuja kujibiwa vizuri zaidi na maelezo ya mfungwa wa gereza la Malawi.

Kumbe kuna vifaa maalumu vya kukorogea hiyo 'poo' vinaitwa digester pia na kiwango mahsusi cha kutosha kinachotakiwa kukorogwa ili kuzalisha gas ya kukidhi.

Katika simulizi hiyo wanaeleza kiwango cha nishati hiyo muda flani kilipungua baada ya idadi kubwa ya wafungwa kuachiwa kutokana na gonjwa la covi!

Maana yake ni kuwa walipoachiwa 'mali ghafi' ya kuzalishia ilipungua.

Ahsante mkuu, nimeelewa bila shaka.
 
Back
Top Bottom