Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

nishati nafuu kwa mtanzania wa hali ya chini ni ipi?
Umeme ndio nishati rahisi zaidi. Ukiweka umeme wa 10500/= unatumika mwezi na zaidi kwa Mtanzania wa kawaida.
Hapo utapika na taa utawasha bila shida
 
Bei itashuka pale Tanesco atakapomaliza lipa Madeni yake yote.
Hapana bei haitashuka kamwe kama hakuna willingness ya kushusha bei....

Ngoja nikupe mfano kidogo tuseme una pipa moja la maji ambalo umelishalikopea pesa za vikoba na lazima ulipe, wewe matumizi yako tuseme ilikuwa ndoo moja, na sasa sababu umepata pipa na maji ya mvua unapata kumi kwahio una ndoo tisa za ziada..., Sasa swali linakuja kipi ni bora uendelee kutumia ndoo yako moja na nyingine tisa kuuza kwa Tshs 1000 /= na watu hawanunui au uuze kwa tshs mia zile tisa angalau upate 900 upunguze deni la vikoba ?

Na kumbuka kwa watu kutumia umeme tutasave pesa ambayo tungenunulia gesi na kuongeza ufanisi wa watu kuanza kutumia oven zao na kuoka chakula
 
Umeme ndio nishati rahisi zaidi. Ukiweka umeme wa 10500/= unatumika mwezi na zaidi kwa Mtanzania wa kawaida.
Hapo utapika na taa utawasha bila shida
10,500/= kwa bei ya sasa unapewa units ngapi ? nataka tupige hesabu ya units na kuzibadilisha kwenye kg moja ya LPG ambayo ni equivalent na kama 13.6 units... Na tuseme ule mtungi una kg 15 (ambazo ni pungufu) na kama inauzwa 60,000/=; kila kg ya gesi ni kama 4000/= (Ingawa nadhani ukichukua jumla yale mamitungi makubwa kabisa ya mahotelini huenda ikawa 3,000/=

Sababu matumizi yanategemea efficiency ya kifaa, tuanzie kwenye gharama ya kg kwa kulinganisha na unit

Tuki-assume ukitoa 10,000/= unapata units 28 kwahio hizo ni sawa na kama kg 2 za Gesi (28/13.6)
Kilo moja kwa bei ya 4,000/= hapo utakuwa umetumia equivalent ya 8,000/= kwa hizo kilo 2

Hivyo kwa bei ya sasa ili Umeme uwe na nafuu itabidi uwe na kifaa chenye ufanisi mfano induction cooker (kama hii ina ufanisi wa zaidi ya mara tatu ya gesi) kwa bei hio hio utakuwa umepata equivalent ya units 84 na sio 28 tena...

Hapo utaona kwamba tunahitaji kufanya mawili.... Moja kushusha bei ya Umeme per Unit na Mbili kutoa Ruzuku watu wanunue vifaa vya kisasa na bora vya Umeme
 
Nimekwisha wahi kufanya huu utafiti Kupikia jiko la Umeme ni nafuu kuliko gesi.

Sababu hatufanyi hizi ni kwa sababu Umeme wetu sio wa uhakika.

Pia na vifaa tunavotumia.

Kama tutakuwa na Umeme wa Uhakika basi Kupikia Umeme ni nafuu sana.

Kingine kuhusu gas, ni marketing campaign inayotumika ni kubwa sana, hii inafanya hata Watu kuwa na bias decision
 
Nimekwisha wahi kufanya huu utafiti Kupikia jiko la Umeme ni nafuu kuliko gesi.
Inategemea unapika nini na unatumia kifaa gani.., kama unachemsha maji kwa jug kettle ya umeme ni rahisi kuliko gesi, kama unachemsha maji ya chai kwa kutumia plate ya umeme ya zamani inachukua muda kufika nyuzi 100 wakati gesi ukiwasha tu unapata hio nyuzi 100, lakini kama unatumia induction cooker hapo unagusa tu ufanisi ni zaidi ya asilimia tisini kwahio hapo gesi inaachwa mbali sana
Sababu hatufanyi hizi ni kwa sababu Umeme wetu sio wa uhakika.
Mkuu uhakika wa umeme upo, sababu hata kama kungekuwa kuna mgao wa umeme wa siku tatu kwa wiki watu wangeweka ratiba ya kupika maharage katika hizo siku tatu au wangefanya gesi kama back-up umeme ukikatika
Pia na vifaa tunavotumia.
Naam katika vifaa hapo kuna ukweli lakini katika vifaa hivyo hivyo sasa hivi vimekuwa na ufanisi kuliko zamani na zamani walitumia umeme sasa hivi mfano taa yenye uwezo kuliko zamani ilikuwa inatumia watts 100 sasa hivi yenye mwanga huo huo inaweza kutumia 15watts...., Nini kimebadilika utaona kwamba ni gharama za units..., kwahio units zikishuka hata vyombo visivyo na ufanisi watu watatumia tu lakini ili wasitumie itabidi TBS ichunge watu kutokuleta vifaa visivyo na ufanisi
Kama tutakuwa na Umeme wa Uhakika basi Kupikia Umeme ni nafuu sana.
Umeme ni wa uhakika..., kitu kinachofanya watu wasipikie umeme ni gharama sio rafiki hata wasiokatiwa ma-oven ambayo walinunue enzi za miaka ile sasa hivi wameyageuza kuwa makabati
Kingine kuhusu gas, ni marketing campaign inayotumika ni kubwa sana, hii inafanya hata Watu kuwa na bias decision
Naam kuna suala la uelewa huenda sio kila kitu kupikia gesi ni rahisi na sio kweli kwamba gesi ni nafuu kuliko mkaa ndio maana pamoja na campaign zao watu bado wanapendelea kutumia mkaa...

Amini nakwambia kama unit moja ikiwa Tshs 25 hata wapika vitumbua kitaa watakuwa wanatumia portable electrical stoves
 
Nimeona article katika gazeti la Mwananchi
What it means as LPG use soars 13-fold in ten years

Ambapo Ewura wanashangilia kwamba ni habari nzuri inayoonyesha watu kuhamia kwenye nishati safi, na nguvu zitaendelea kutumika ili watu wengi zaidi wahamie huku....
Yaani mwaka juzi tumiagiza tani 250,200 kutoka tani 18,170 miaka kumi iliyopita na watumiaji asilimia 50 ya gesi hiii ni sehemu za Pwani..., utaona kwamba tukiendelea kwa mwendo huu tutatakiwa kuagiza mamilioni ya tani za hii gesi na kuendelea na matumizi ya fedha za kigeni....., na kuweka rehani mapishi yetu kutegeme bei ya dunia inasemaje....

Je hii ni Habari Nzuri na Je hii ni njia Sahihi
Kumbuka si kweli kwamba mpaka dakika hii nishati hii ni nafuu kuliko mbangaizaji kujiokotea vijikuni na kuunga unga mlo wake kwahio zaidi ya kutumia dollar kuagiza hii nishati bado tutatumia Kodi zetu kama ruzuku ili kufidia kama tutataka bei ya gesi hii ishuke bei... Cha kujiuliza kwanini hizo nguvu tusiwekeze kwenye umeme ambao tunao na hatuagizi na ni rahisi kwa sisi kutumia gesi iliyopo Mtwara kuzalisha huo umeme mpaka umfikie mpikaji nyumbani kwake bila kuhitaji kuagiza mamilioni ya Nishati kutoka nje ya nchi ?
 
Kupikia Nishati ya umeme ni rahisi kwa ghrama kuliko gas. Mfano hai u annual umeme wa Tsh 10500/= unapata unit 73 matumizi yoote ya mapishi kwa mwezi haizi unit 20 ukijumlisha na matumizi ya pasi friji taa za ndani na nje unit 20 unakuwa umetumia Unit 40 hadi 45. Hayo nimatumizi ya just lakini kwa matumizi chini haizidi hizo units 40
 
nishati nafuu kwa mtanzania wa hali ya chini ni ipi?
Nishati nafuu na rahisi ni kuni na mkaa. Kumbuka kuna mtu hawezi kuwa na kipato cha kununua gesi kutokana na mazingira,kipato na umri wake
Kuni ndio inakua rahisi kwake kwani anaokota tu shambani
 
Kupikia Nishati ya umeme ni rahisi kwa ghrama kuliko gas. Mfano hai u annual umeme wa Tsh 10500/= unapata unit 73 matumizi
Sasa wewe ndio unaanza kuja kwenye hoja yangu na baada ya hii post nadhani utanielewa..., unapata units hizo sababu wewe upo zero tariff na ninakushauri usingojee huo umeme uishe kila mwezi jaza 9100 plus kodi ya jengo 1500 ndio hio kama 10,600 ama sivyo siku ukivuka matumizi ya 75 units watakupandishia wakuchaji zaidi ya 300 per unit...

wengine wote wakitoa elfu kumi wanapata units kama 28 tu.... kwahio ndio maana ninasema kama wote bei ikishuka na tukapata kwa elfu kumi units kama zako hata units 400 kwa elfu kumi nakwambia mitungi ya gesi itabakia kuwa mapambo
yoote ya mapishi kwa mwezi haizi unit 20 ukijumlisha na matumizi ya pasi friji taa za ndani na nje unit 20 unakuwa umetumia Unit 40 hadi 45. Hayo nimatumizi ya just lakini kwa matumizi chini haizidi hizo units 40
hizo units inategemea pia na matumizi kwa mtu ili kupata bei halisi lazima uangalie ufanisi wa chombo na ubadilishe umeme na gesi katika units sawa yaani kwh (units) na 1kg ya gesi ni equivalent na approx 13 units
 
Nishati nafuu na rahisi ni kuni na mkaa. Kumbuka kuna mtu hawezi kuwa na kipato cha kununua gesi kutokana na mazingira,kipato na umri wake
Kuni ndio inakua rahisi kwake kwani anaokota tu shambani
Naam huwezi kupambana na bure..., sababu yeye kwa sasa anaokota tu shambani wala hakati miti kwahio kwake yeye ndio cheapest ingawa huenda isiwe na ufanisi ule muda n.k. lakini mtu huyu akipata ruzuku ya kununu vyombo vya umeme na kuwa na rice cooker, jug kettle, fryer, oven n.k. mwenyewe tu atapenda ufanisi huu..., lakini kuhusu gesi ni kampeni tu za wauzaji..., sababu kwanza gharama ipo juu, pili gharama haiwezi kushuka zaidi ya bei ya dunia tunayonunulia..., tatu kumtuma boda tu au yoyote afanye delivery mpaka kwa huyu mzee pia ni cost ambayo inabidi kulipiwa na mtu fulani..., na kama itafanywa na serikali kama ruzuku fahamu hizo ni kodi zetu..
 
Hii iingizwe kwenye SoC 04
 
Hii hoja inahusu watu wa mijini na sio huko vijijini kabisa. Kuna sehem hata ukiwaambia wapikie mkaa watakuona unawabadilishia mfumo wa maisha
Naam kama mtu anatumia Kuni ambazo ni bure alafu anunue mkaa huoni hii itakuwa gharama kwake ? Hata wapikaji wale wa tender wanatumia kuni ni cheaper kwao..., Magereza wanatumia Kuni (ingawa hawa wangeweza kutumia Biogas ya Kinyesi chao)

Kwahio hawa watu badala ya kuja na ndoto za kuwatoa kwenye bure (kuni) na kuwapeleka kwenye gesi (wakati hawana kipato) ni vema tukawapeleka kwenye umeme ambao una ufanisi mkubwa sana na tunazalisha wenyewe
 
Ninapenda kuwasikiliza na kusoma makala za watu wanaojenga hoja na kuwa watatuzi wa matatizo... Na siyo wenye maswali tu bila majibu.

Andiko murua kabisa hili.

Big Up!
 
Uzi bora kabisa umejaa madini.

Nchi hii tunahitaji watu waina yenu.

Wenye akili mpo wengi nje huko ila wasio na akili ndio wanapewa nchi waivuruge wanufaishe matumbo yao na familia zao.
 
Watu wenye akili mpo nje huko ila wasio na akili ndo wanapewa nchi waiongoze wakinufaisha matumbo yao na familia zao.

NChi tunahitaji watu wanaofikiria kama ww.
 
Kuwaamini wanasiasa inakupasa uwe zuzu kidogo.
Yaani serikali hii hii iliyopandisha bei ya kuunganisha umeme kutoka 27000 hadi sh 318000 pia ikapandisha na bei za unite za umeme leo wanakuja na swaga za nishati rahisi mnataka kuamini?
Ukiona serikali inataka kufanya mradi na unapambwa jua wazi kuna mtu anatengeneza dili hapo.
Ruzuku itatolewa na gesi haishuki ng'o!
 
Kuwaamini wanasiasa inakupasa uwe zuzu kidogo.
Hakuna anayewaamini ila ndio hivyo mfuko umeanzishwa kwahio ni vema tukatumia hizo pesa kwa manufaa na sio kuzifuja
Yaani serikali hii hii iliyopandisha bei ya kuunganisha umeme kutoka 27000 hadi sh 318000 pia ikapandisha na bei za unite za umeme leo wanakuja na swaga za nishati rahisi mnataka kuamini?
Haipaswi kuunganishwa kuwe gharama tena ingekuwa bure sababu vifaa vyote mita nguzo ni mali yao ni sio mali yako wewe ulipie matumizi pekee
Ukiona serikali inataka kufanya mradi na unapambwa jua wazi kuna mtu anatengeneza dili hapo.
Ruzuku itatolewa na gesi haishuki ng'o!
Naam kuna watu watanufaika na hata gesi ikishuka kwako wewe unayenunua haitashuka kule wanaponunua..., kwahio ndio maana nina-suggest tuache kuagiza hii gesi lpg na gesi asilia ya mtwara badala ya kuletwa majumbani kwenye mabomba ipelekwe kwenye kuzalisha umeme na umeme ndio usambazwe ili watu wapikie..., tena kwa bei ya 25/ au au chini ya hapo kwa unit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…