Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

Wansisitiza gas kwa sababu kuna mhuni mmoja kawatia mifukoni ana maslahi na LPG
 

Makaa ya Mawe coal Tanzania kwa matumizi ya nyumbani, tujifunze kwa wenzetu.

Makaa ya mawe hutumiwa kama chanzo cha ndani cha nishati na kaya za kipato cha chini nchini Afrika Kusini.

Makaa ya mawe ni chanzo cha nishati cha bei nafuu na hutoa matumizi mawili - hupasha joto nyumba na kuruhusu kupikia kufanyika katika kifaa kimoja kwa kutumia mafuta moja tu.

Licha ya bei nafuu na upatikanaji wa nishati , matumizi ya makaa ya mawe husababisha viwango vya juu sana vya uchafuzi wa hewa na magonjwa ya kupumua yanayoambatana - wastani wa dola milioni 160 kwa mwaka nchini Afrika Kusini.

Upatikanaji wa umeme hausababishi kaya kuhama kutoka kwa makaa ya mawe kwa kuwa umeme na vifaa vya umeme vinachukuliwa kuwa haviwezi kumudu.

Mada hii inawasilisha taarifa zilizokusanywa wakati wa utafiti wa msingi wa nishati katika kitongoji cha mijini kilicho na umeme nchini Afrika Kusini, na inaelezea jinsi makaa ya mawe yanatumiwa na kununuliwa na kaya maskini. Njia mbadala ya kuwasha moto, iliyothibitishwa kupunguza moshi na uchafuzi wa hewa fomu moto wa makaa ya mawe imeonyeshwa kwa kaya na matokeo ya kutia moyo chanya.

Mbinu iliyojumuishwa, kushughulikia muundo wa makazi yenye ufanisi wa nishati, usambazaji wa vifaa vya nishati safi na bora pamoja na utumiaji wa njia mbadala ya kuwasha moto, inashauriwa kushughulikia uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya makaa ya mawe ya kaya.

Mtaa Afrika ya Kusini

Kwa nchini Tanzania juhudi zifanyike nishati hii itumike kwa kuwahusisha wabunifu wa majiko na sufuria za kuhimili nishati ya makaa ya mawe. Mafundi mchundo technicians na viwanda vidogo watiwe moyo kuzalisha majiko ya kuweza kutumia makaa ya mawe ambayo yanapatikana kwa wingi nchini Tanzania na kusafirishwa nchi za nje ili pia yaweze kutumika ndani ya nchi ngazi ya kaya / familia

UNAYAFAHAMU MAKAA YA MAWE?, JIONEE KWENYE BANDARI YA MTWARA TANZANIA YANAVYOSAFIRISHWA KWENDA NJE YA NCHI ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=GqXx-H6ZS8Q
2021 17 Julai
Rafael Mbise ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha, Tanzania hapa chini katika video amesema amebuni jiko hilo kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. UNAWEZA KUWASILIANA NAYE KWA NAMBA HIZI..... 0767390430.


View: https://m.youtube.com/watch?v=GbOvgIebhak
 
Dili la mhuni mwenye maslahi na LPG hakuna la maana hapo
 
Haya Sasa ndo madini yanayohotajika hapa JF. Sio notes za mapambio na mashudu mengi yasiyo eleweka..
 
Mafundi mchundo technicians na viwanda vidogo watiwe moyo kuzalisha majiko ya kuweza kutumia makaa ya mawe ambayo yanapatikana kwa wingi nchini Tanzania

Kamati yafika wilaya ya Mbinga kuangalia mojawapo ya mgodi wa makaa ya mawe mkoani Ruvuma nchini Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=mrIYzP9g8zw
Juhudi ya kupata nishati ya makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani hii itaokoa miti yetu ktk mapori na misitu isitumike kama kuni na mkaa wa kupikia majumbani
 
Kuna watu India wanapikia hadi mavi ya ng'ombe issue ni upatikanaji na bei nafuu kwahio hata haya tukiyapata / kuyatumia hapa yatakuwa nafu, pia sawa yana unafuu wa gharama je kwa afya, sababu wadau wa mazingira ulimwenguni wanaweza kuanza kukupiga majungu.... Mwisho kabisa ushauri wangu kama haya yanapatikana na kwa bei nafuu kuliko vyanzo vingine na bila athari kubwa za kimazingira badala ya kuyasambaza kwenye kila kaya kwanini tusiyapeleke sehemu moja tu ili yakafue umeme na hizi kaya zilitewe umeme (ambao ni rahisi kuutumia)?
Licha ya bei nafuu na upatikanaji wa nishati , matumizi ya makaa ya mawe husababisha viwango vya juu sana vya uchafuzi wa hewa na magonjwa ya kupumua yanayoambatana - wastani wa dola milioni 160 kwa mwaka nchini Afrika Kusini.
Unaona hata kwenye hii article yako wanayapiga vita
Upatikanaji wa umeme hausababishi kaya kuhama kutoka kwa makaa ya mawe kwa kuwa umeme na vifaa vya umeme vinachukuliwa kuwa haviwezi kumudu.
Naam bei ni kubwa ya umeme (ambayo mimi nasema kwa vyanzo vyetu ishuke hata kufikia 25/= kwa unit) bila hivyo watu wataendelea kufanya magendo hata mkipiga vita mkaa au wengine watalala njaa sababu gharama ya chakula itakuwa imeongezeka...
Okay hii ni mbinu ambayo huenda itapunguza makali ya ki-afya je hayo makaa yatakuwa bei gani mtaani ?, Mbili kuna athari za makaa ya mawe katika uchimbaji au utunzaji yanaweza kuathiri ground water na uwakaji wake una emissions zaidi ya LPG...,

Lakini mimi am all for that kama hii nishati inafaa ni bora iende kufua umeme na watumiaji waletewe nishati majumbani inayofanya shughuli zao zote hapo majumbani kuanzia kuchemsha maji mpaka kukaanga chips na kuoka mikate.
 
Naam kama hayo makaa ya mawe yapo na ni rahisi kuliko vyanzo vingine huoni kwamba itakuwa na ufanisi zaidi kama tukiyatumia kuzalisha umeme alafu tukatumia umeme huo kupikia ? Ukizingatia kama tutakuwa na umeme mwingi kuliko mahitaji basi kuna uwezekano wa umeme kushuka bei kama tutaacha ubinafsi na tamaa za watu wachache za kutumia shida za wengine kama fursa.... (Umeme ni Huduma)
 
Unaona hata kwenye hii article yako wanayapiga vita

Mabeberu tusiwasikilize, tutumie makaa ya mawe kwa matumizi ya kupikia na hii itapelekea misitu yetu kuongezeka hivyo hewa safi zaidi pia mazingira ya kijani kutunzwa
 
Mabeberu tusiwasikilize, tutumie makaa ya mawe kwa matumizi ya kupikia na hii itapelekea misitu yetu kuongezeka hivyo hewa safi zaidi pia mazingira ya kijani kutunzwa
Swali linakuja kipi ni rahisi kuchukua haya makaa ya mawe na kuyauza kama mkaa au kuchukua haya makaa ya Mawe kuyapeleka sehemu ya kufua umeme na huo umeme kuusambaza katika kila Kaya.., Badala ya kusafirisha mizigo ya makaa ya mawe tusafirishe umeme mpaka majumbani
 
Rosti Tamu ambaye ni mpambe wa Mama na mfanyabiashara maarufu wa gesi tayari ashampanga mama ili apige pesa
Kama ulivyosema nishati rahisi kwa sasa ni umeme ambao upo wa kutosha na ukishushwa bei watu wengi watahama kwenye kupika kwa kuni,mkaa,na gesi na kuamia kwenye umeme na hilo wafanyabishara wa gesi hawawezi kubali kirahisi.
 
Nimesikia Serikali na Wizara ya Nishati inajiweka sawa ili kuongeza miundombinu ya kuweza kupokea gesi nyingi zaidi (yaani kuagiza) kweli nimesikitika sana..., Hii ni kuonyesha kwamba tumeamua kwenda njia ya Propane gesi (gesi ya kuagiza)
 
Nauza gesi huu ushauri siutaki
Faidaya yako kwa gesi kwa mwezi ni kiasi gani kama ni retailer nadhani itakuwa kwenye buku tano.., lakini huoni kwamba badala ya hizo bilioni tulizopewa nje kuwanufaisha makampuni ya ulaya kina Oryx hizo pesa msipewe nyie badala ya kuuza mitungi muuze majiko ya umeme na viwanda vya ku-assemble na ku-repair majiko ?

Na sisi tusiouza gesi badala ya kutumia elfu 50 na kitu kununua mtungi ili tupike labda kwa mwezi gharama ikishuka tukatumia hata elfu 20 au kumi kwa bei hio chenji inayobaki tukafanya mengine huoni kila mtu atanufaika ?
 
Nikishakuhudumia utarudi tena lini?
Gesi kila mwezi lazima ujaze gesi
 
Nikishakuhudumia utarudi tena lini?
Gesi kila mwezi lazima ujaze gesi
Utahamia kwenye kuuza maji ya kunywa (Kila siku lazima wanywe) au vijisenti watu watakavyosave badala ya kununua gesi wataweza kununua nyama (Hivyo pesa yao utaipata pengine) na nzuri zaidi hii pesa itazunguka ndani sio kupelekea watu ughaibuni ili kununua gesi jumla tuje kuuza rejareja...
 
Logikos, huu ni ushahidi mzuri wa binadamu sisi,

Binadamu ni kiumbe mbinafsi sana, anapoona unataka kuingikia maslahi yake, yupo tayali hata kukupoteza,

Nimekuwa nikisoma maandiko yako, yanaonyesha kabisa upo kwa ajili ya kuona maisha ya Mama zetu , ndugu yanapata unafuu,

Lakini unabypass baadhi ya vitu ambavyo ni logic kabisa.,

Sasa sijui hujui au umeamua kuweka mtego tu,

Ni vitu gani hivyo, nitaeleza.

Hivi kwa ufahamu wako wewe , unadhani haya uliyoelezea hayafahamiki huko kwa watoa maamuzi,

Yanafahamika sana, shida ni UROHO WA PESA, UBINAFSI, ROHO MBAYAUBINADAMU ZIRO,

Haya yote wanajua , lakini wanachoangalia ni kuneemesha matumbo yao.

Mtu anaona aneemeka yeye kwa kuagiza gas, ili mfuko wako utune , lakini sio kumsaidia Mwananchi.

Hivi unajua kwa nini walipiga vita bwawa la Mwalimu,

Ni kwamba walijua ndio mwisho wa kuneemeka.

Na nakwambia hata likiisha vile vinu tisa vyote vya kufua umeme haviwezi kuwashwa.

Magufuli alipunguza mpaka bei ya kuunganisha umeme, na mambo yakaenda, kwa nini hawa leo wamepandisha tena mpaka laki tatu,

Hivi kwa nini hata walishindwa kupandisha mpaka 100000/-, iende mpaka 300000 ? , hii ni kwa manufaa ya nani,

Kingine unachosahau , hawa watu wameshindwa kubunu au kukusanya kodi, sasa wameina njia nafuu ya kukusanya kodi ni kuwaminya wananchi, maana hiyo ni njia njia nyepesi sana ya kukusanyia kodi, sio kukupa unafuu wa maisha wewe mwananchi,

Hawa watu ni wabaya sana, hawana huruma na wananchi, wana mapesa mengi sana lakini hawalidhiki,

Mtu anaona bora kutetea wajengewe majumba wakustaafu , au walipwe posho za waume zao, wakistaafu, pamoja na mapesa yote wakiyonato, lakini sio kumtetea mwananchi hata kumpa unafuu wa kupika chakula tu.

Kwa hiyo kaa ukijua haya unayoyaandika sio kwamba ni mawazo mapya , hapana wanajua sana,

Ika ni roho mbaya tu.

Labda ungeanduka namna ya kuwafanya hawa watu waache riho mbaya.

Nimemnnukia MAMAyangu jiko la gesi na taa ya solar, lakini vyote vimebaki mapambo tu, amerudi kwenda kuokota kuni. Sababu gharama zake sio rahisi jihivyo, leo hawa wanasuport mambo ya gesi, hicho kipato cha wananchi kutumia gas wamekiongeza lini.

Acha ndugu, hata mambo ni magumu.

Magufuli tu ndiye aliyeweza kusema neno moja tu na mambo yakawa. Sio hawa ambao tunao.
 
Naam wao wanajua lakini wananchi hawajui ndio maana wanalishwa propaganda kwahio mimi hapa najaribu kuweka upande wa pili ili wananchi wajue ukweli wa mambo..., nimegundua wananchi wanadhani haya ni ya kweli:-
  1. Kwamba hii gesi ya kwenye mitungi majumbani inaweza ikawa ndio gesi yetu asilia ya Mtwara hivyo hatuagizi
  2. Kwamba umeme hautoshi wala hauwezi kutosha kwa watu kupikia
  3. Kwamba umeme hata ukiwa mwingi tukimaliza Bwawa tutauza nje au tumekopa sana hivyo tutakuwa tunalipa wanaotudai hivyo hauwezi kushuka bei
  4. Kwamba umeme sio wa uhakika hivyo utakuwa unakatika katika wakati gesi ipo
  5. Kwamba wanaweza wakapewa ruzuku gesi ishuke (hawajui kwamba pesa ya ruzuku ni pesa yao inachukuliwa kwa mgongo wa nyuma)
  6. Kwamba nishati nafuu ni gesi na umeme hauwezi kuufikia nishati hii
  7. Kwamba hizi units za umeme tunazolipia ni fair kabisa wala hazina tatizo na haziwezi kupungua (wakati ukweli ni kwamba zamani walikuwa na vifaa vya umeme visivyo na ufanisi na bado walivitumia na walimudu gharama)
Sasa motive yangu ni hopefully wakiwa wanapita kumpa mama yako mtungi wa gesi na jiko la gesi bure (ili wamteke kila baada ya ukiisha anunue tena na hatakuwa hana choice sababu mkaa utapigwa marufuku) AWEZE Kuwauliza haya ambayo by the atakuwa anayajua na sasa hayajui....
 
Yaeh , bahati nzuri hawa watu ni wajuzi wa plopaganda,
Na sisi wananchi wananchi wameshatufanya majuha,

Ndio maana kitu chochote cha kutufanya tuwe na ufahamu wametuzibia,

Utaona mwaka kesho uchaguzi ukifika namna wananchi watakavyowashobokea,

Tunasahau kila kitu,

Wana roho mbaya sana hawa viumbe
 
Na sisi tunawaachia ndio maana humu nilitegemea niweke uzi huu kama mtego ili watu waje wanibishie au wanieleweshe au wanifahamishe wapi nimekosea..., sasa navyoona kimya nashangaa, na sidhani kama wote wanafaidika na huu ulambaji asali ni kwamba wengi ni kina sisi ambao tunalipia gharama katika matumizi na wajukuu watalipa Madeni ya Mikopo tutakayokopa ili tufanikishe huu mradi wa kuwanufaisha wachache na mataifa ya mbali...
 
Inasikitisha sana,
Lakini ipo siku isiyokuwa na jina inakuja,

Na mwenyezi Mungu asivyokuwa na haiana , amewapiga upofu mkubwa sana , kiasi kwamba hawasikii wala hawaoni.

Mungu ibariki Nchi yangu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…