SoC04 Nishati ya ‘hydrogeni’ mbadala wa utunzaji wa umeme itasaidia kupunguza changamoto kutokana na upungufu wa umeme na hitilafu kwenye gridi ya taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

voiceupp

Member
Joined
Aug 17, 2022
Posts
16
Reaction score
27
Uzalishaji wa umeme unapokidhi mahitaji nchini unachangia kwenye ukuaji wa uchumi kutokana na shughuli nyingi za viwanda vikubwa na vidogo kuendeshwa kwa utegemezi wa umeme Umeme unapokua wa uhakika uzalishaji wa bidhaa huongezeka na gharama za uendeshaji hupungua.

Wananchi waliojiajiri kupitia shughuli zinazotegemea umeme huepuka hasara ya kuharibikiwa na bidhaa, na kwa kushindwa kuendesha shughuli zao kwa ufanisi. Jambo ambalo huwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Changamoto kubwa kwenye uzalishaji wa umeme ni kwamba umeme unahitajika kuwepo kwa kiwango sahihi kwenye gridi. Kiwango kilichopo kwenye gridi kisizidi au kupungua kiwango cha matumizi.

Hivi sasa Tanzania baada ya kuwasha baadhi ya mashine za kuzalisha umeme kwenye bwawa la Nyerere tumeshuhudia umeme ukizalishwa kupita kiasi hali inayopelekea kuzima baadhi ya mashine kuepuka changamoto ya umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa.

Bwawa la nyerere linaweza kuzalisha megawati 2115, kwa mwaka 2023 uhitaji wa umeme nchini ilikua ni megawati 1363.94. Ingawa uhitaji wa umeme huongezeka kadiri siku zinavyokwenda kutokana na matumizi kuongezeka.

Uzalishaji wa umeme wa maji huathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Uzalishaji kupungua yanapotimu majira ya kiangazi na kipindi cha ukame kutokana na mabwawa kupungua kina hivyo nguvu ya maji inayozungusha mashine za kuzalisha umeme kupungua.

Changamoto kubwa nyingine ni hitilafu za mara kwa mara zitokeazo kwenye gridi ya taifa jambo ambalo hupelekea ukosefu wa umeme kwa saa kadhaa kwenye maeneo mengi nchini.

Nishati ya hydrogeni suluhisho la upungufu/kuzidi umeme na hitilafu kwenye gridi ya taifa;
Ingawa changamoto ya umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa inaweza kutatuliwa kwa kuuza umeme nchi jirani, lakini swali la kujiuliza ni Je, umeme huo utakua wa uhakika kwa kipindi chote? Hii ni ili kuepuka kushindwa kusambaza umeme wa uhakika pindi itakapotokea upungufu wa uzalishaji au hitilafu kwenye gridi ya taifa au kuongeka kwa matumizi ya umeme nchini.

Kuepuka changamoto hii ni vizuri kuchagua njia nzuri na sahihi ya kukabiliana na changamoto za umeme nchini. Njia ambayo itaweza kutumika kwenye matumizi mengine endapo hakutotokea upungufu wa umeme.

Njia nzuri ni kuhifadhi umeme unaozalishwa na kuweza kuutumia pindi uzalishaji utakapokua mdogo. Itafanyika endapo uzalishaji wa umeme utazidi kiwango cha matumizi na kupelekea umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa. Njia nzuri na nafuu ni kuhifadhi umeme kupitia nishati ya hydrojeni. Ili kuzuia umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa, umeme utakaozidi utatumika kuzalisha gesi ya hydrojeni na kuhifadhiwa. Umeme utakapopungua kwenye gridi gesi hiyo itatumika kuzalisha umeme na kurudishwa kwenye gridi kwa ajili ya kuepusha kukatika/mgao wa umeme.

Uzalishaji wa nishati ya hydrojeni kwa kutumia umeme unavyofanyika;
Zipo njia kuu mbili za kuzalisha nishati ya hydrojeni kwa kutumia umeme ambazo ni rafiki wa mazingira.
  • Kuvunjavunja maji (hydrolysis of water) na kupata hewa ya oksijeni na hydrojeni (H2O = H2 + O2)
Njia hii hutumia umeme kuvunja maji ya kawaida na kupata gesi ya hydrojeni na gesi ya oksijeni ambapo zote zinaweza kuvunwa na kuhifadhiwa.
Ili kupata kilo moja (1kg) ya hydrojeni kupitia njia hii inahitajika kilowati 50 hadi 55 za umeme (50-55kWh).
  • Kuvunjavunja amonia (NH3) (ammonia electrolysis) inayopatikana kwenye majitaka, mabaki na vinyesi vya viumbe hai na kupata hewa ya naitojeni (N2) na Hydrojeni (H2).
Njia hii inahitaji kilowati 1.55 (1.55kWh) ili kupata kilo moja ya gesi ya hydrojeni (1kg). Njia hii inatumia umeme mdogo zaidi ukilinganisha na ya kutumia maji ya kawaida.

1715351373929.png

Uzalishaji wa nishati ya hydrogeni kwa kutumia ammonia (Picha kutoka mtandaoni)

Kiasi cha umeme kinachotokana na nishati ya hydrojeni
Kwa makadirio kilo moja (1kg) ya hydrojeni inauwezo wa kuchakatwa na kuzalisha umeme kilowati 23 (23kWh). Ili kupata megawati 100 (100mWh) itahitajika walau tani 4.3 za nishati ya hydrojeni.

Faida za kutumia nishati ya hydrojeni kuhifadhi umeme;
Urahisi na unafuu kuzalisha
Ni rahisi kuzalisha nishati ya hydrojeni kutokana na mahitaji yake (maji, majitaka, mabaki ya viumbe hai na vinyesi vya wanyama) kupatikana kwa urahisi. Pia ni nafuu kutokana umeme utakaotumika kuzalisha nishati ya hydrojeni utakua ni ule uliozidi kutoka kwenye vyanzo vingine vya umeme (maji, jua, upepo na jotoardhi ‘geothermal’)
Rafiki wa mazingira.
Mabaki yanayotakana na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya hydrojeni ni maji na joto, vyote hivi huweza kutumika kwa matumizi mengine. Njia hii haizalishi uchafu au hewa chafu kwenye mazingira.
Matumizi mbadala
Nishati ya hydrojeni ina matumizi mengine kama kuendeshea vyombo vya usafiri (magari n.k) na mitambo ya viwandani. Hii ni faida kwani endapo uzalishaji wa umeme usiposhuka chini ya kiwango nishati hii itaweza kuuzwa na kutumika kwenye matumizi mengine.
Usafishaji wa maji na hewa
Uzalishaji wa nishati ya hydojeni kwa kuchakata amonia inayopatikana kwenye majitaka itasaidia kusafisha maji na kuzalisha maji safi yatakayofaa kwa matumizi ya binadamu. Pia kituo cha uzalishaji wa nishati ya hydrojeni kinaweza kutumika kusafisha hewa kwa kuchuja na kuondoa vumbi linalopatikana kwenye hewa.

Ili jambo hili kufanya kazi kwa ufanisi ni vyema kufanya mambo haya;
  • Kuhakikisha kila kanda inakua na kituo walau kimoja kwa ajili ya mchakato huu,
Itasaidia uzalishaji na uhifadhi mkubwa wa nishati ya hydrojeni. Pia itasaidia kua kama mbadala (backup) pindi itakapotokea hitilafu kubwa kwenye gridi ya taifa jambo ambalo litaepusha nchi nzima kukosa umeme.
Tanzania bara na visiwani kuna jumla ya kanda 10, kila kanda ikiwekewa kituo kimoja chenye uwezo wastani wa kuzalisha umeme megawati 150 kutokana na nishati ya hydrojeni itakayokua imehifadhiwa kwenye vituo hivyo, jumla itawezekana kuzalisha megawati 1500 ambazo zitamaliza kabisa changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
  • Kufanya marekebisho kwenye gridi za umeme,
Hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kila gridi ya umeme inabeba kiwango cha umeme inachostahili na kuepusha kubeba kiwango kikubwa cha umeme kuzidi uwezo wake jambo ambalo hupelekea kutokea kwa hitilafu za mara kwa mara kwenye gridi za umeme.

Hivyo; uhakika na utoshelezi wa umeme utafanikiwa endapo umeme unaozalishwa utatumika ipasavyo kwa kuhakikisha uwepo wake hata endapo uzalishaji utakaposhuka. Ili kufanikisha hili itahitajika kuhifadhiwa kwa umeme unaozalishwa hasa kwa kutumia njia nafuu na yenye ufanisi mkubwa. Uhakika na utoshelezi wa umeme ni chachu ya maendeleo ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmojammoja.
 
Upvote 740
Moderators safari hii muwe na qualified judges (waliompa ushindi wa mwaka jana, technically ni upuuzi) ile sio namna ya fikra za kodi.

Binafsi najipa wajibu wa kiherehere wa kukosoa, kila nitakapo pata wasaa.

Sasa mtu anaandika vipi mada ya uzalishaji wa umeme wakati hakuna mahala kazungumzia issues za energy security na reliability ya sources za uzalishaji kwa uwezo wa nchi.

Mtu kama huyu hajui hata gharama za kuzalisha hydrogen energy, kwa technology ndio ni environmental friendly but very expensive kuupata huo umeme kwa technology iliyopo.

Mtu hana jibu la gharama za technology na wala mbinu za kuonyesha nchi itafaidika kwa namna gani.

Hata kwa essay/report ya mwaka wa kwanza chuo it’s a failure F.

Hakuna cha maana unachoelewa katika uliyoandika.

Don’t worry you are not alone nawaendea na wengine.
 
Moderators safari hii muwe na qualified judges (waliompa ushindi wa mwaka jana, technically ni upuuzi) ile sio namna ya fikra za kodi MZ

Binafsi najipa wajibu wa kiherehere wa kukosoa, kila nitakapo pata wasaa.

Sasa mtu anaandika vipi mada ya uzalishaji wa umeme wakati hakuna mahala kazungumzia issues za energy security na reliability ya sources za uzalishaji kwa uwezo wa nchi.

Mtu kama huyu hajui hata gharama za kuzalisha hydrogen energy, kwa technology ndio ni environmental friendly but very expensive kuupata huo umeme kwa technology iliyopo.

Sasa wewe una jibu la technology na wala mbinu za kuonyesha nchi itafaidika vipi na kwa namna gani.

Hata kwa essay/report ya mwaka wa kwanza chuo it’s a.failure F.

Don’t worry you are not alone nawaendea na wengine.​
Pia ingependeza ulivyokosoa uje na fact uonyeshe ni gharama kubwa kiasi gani itakayotumika kuzalisha hiyo hydrogen ambayo nchi itahindwa kumudu.

Kumbuka gharama kubwa ni kutokana na umeme unaotumika kuzalisha hydrogen, na mimi nimeandika kutokana na yaliyotokea ya umeme kuzalishwa kuzidi kiwango mpaka kupelekea baadhi ya mitambo kuzimwa.

Kwa maana hiyo kama ni umeme kuna kipindi unakwepo mpaka unazidi, kwaiyo kuliko kuzima hizo mitambo ni bora kuutumia kuzalisha hiyo hydrogen.

Pia hapa tunazungumzia mambo yanayoweza kutekelezwa ndani na miaka 5 mpaka 25 na siyo yale tu yanayoweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja. Hivyo inawezekana kuanza kidogokidogo uzalishaji huo kama tatizo itakua gharama kwenye miundombinu yake.

Nchi nyingi zilizoendelea zinakimbilia kwenye nishati ya hydrogen hujiulizi ni kwanini? Na yapo malengo yaliyowekwa ya kuhakikisha gharama za uzalishaji wa hydrogen safi zinapungua. Kwa maana hiyo wapo watu wanapambana kuhakikisha hilo linatimia mpaka kufikia 2030 na hii ni pamoja na kuboresha na kuzalisha kwa wingi mashine za electrolyzer.

2030 kutoka sasa ni miaka 6 tu, hapo ukizungumzia miaka 20 mpaka 25 kutoka sasa kuna mwanga kwamba gharama za uzalishaji zitakua zimepungua kwa kiasi chake.

Pia usione nimeandika machache ukaona kwamba sina ufahamu na nilichoandika, maneno 1000 ni machache sana huwezi ukaandika kila kitu. Na hapo nimejaribu kufupisha lipo andiko nililonalo ambalo limebeba mambo mengi kuhusiana na nishati ya hydrogen ukitaka niambie nikutumie, pia hata majaribio ya uzalishaji wa hydrogen kwa kutumia hydrolysis na uzalishaji wa umeme kwa kutumia hydrogen nimeshafanya na sio kwamba naandika kitu ambacho sina uelewa nacho.​
 
Bandiko zuri hongera sana kwa kuleta mada fikirishi. Mimi nina swali moja tu Je, matumizi ya nishati ya hidrojeni yataleta athari gani kwa ajira zinazohusiana na sekta ya nishati nchini Tanzania?
 
Kwenye upande wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo vingine hawataathirika kutokana na uzalishaji wa hydrogen utategemea umeme utokanao na vyanzo vingine.
 
Pia ingependeza ulivyokosoa uje na fact uonyeshe ni gharama kubwa kiasi gani itakayotumika kuzalisha hiyo hydrogen ambayo nchi itahindwa kumudu.

Kumbuka gharama kubwa ni kutokana na umeme unaotumika kuzalisha hydrogen, na mimi nimeandika kutokana na yaliyotokea ya umeme kuzalishwa kuzidi kiwango mpaka kupelekea baadhi ya mitambo kuzimwa.

Kwa maana hiyo kama ni umeme kuna kipindi unakwepo mpaka unazidi, kwaiyo kuliko kuzima hizo mitambo ni bora kuutumia kuzalisha hiyo hydrogen.

Pia hapa tunazungumzia mambo yanayoweza kutekelezwa ndani na miaka 5 mpaka 25 na siyo yale tu yanayoweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja. Hivyo inawezekana kuanza kidogokidogo uzalishaji huo kama tatizo itakua gharama kwenye miundombinu yake.

Nchi nyingi zilizoendelea zinakimbilia kwenye nishati ya hydrogen hujiulizi ni kwanini? Na yapo malengo yaliyowekwa ya kuhakikisha gharama za uzalishaji wa hydrogen safi zinapungua. Kwa maana hiyo wapo watu wanapambana kuhakikisha hilo linatimia mpaka kufikia 2030 na hii ni pamoja na kuboresha na kuzalisha kwa wingi mashine za electrolyzer.

2030 kutoka sasa ni miaka 6 tu, hapo ukizungumzia miaka 20 mpaka 25 kutoka sasa kuna mwanga kwamba gharama za uzalishaji zitakua zimepungua kwa kiasi chake.

Pia usione nimeandika machache ukaona kwamba sina ufahamu na nilichoandika, maneno 1000 ni machache sana huwezi ukaandika kila kitu. Na hapo nimejaribu kufupisha lipo andiko nililonalo ambalo limebeba mambo mengi kuhusiana na nishati ya hydrogen ukitaka niambie nikutumie, pia hata majaribio ya uzalishaji wa hydrogen kwa kutumia hydrolysis na uzalishaji wa umeme kwa kutumia hydrogen nimeshafanya na sio kwamba naandika kitu ambacho sina uelewa nacho.​
IMG_7412.jpeg

Soma hiyo report kutoka wizara ya nishati U.K. uone Hydrogen ina gharama kubwa kiasi kuzalisha MWh kulinganisha na renewable nyingine.

Mind you carbon energy sources ni very cheap (minus environment costs) ndio maana kuachana nazo kabisa wameshindwa kama unatazama mambo kwa msingi wa energy security na kulinda uchumi.

Ni vipi umeme wa gharama kama hydrogen, utasababisha gharama za uzalishaji kupungua. Si ndio kwanza huu mgogoro wa Ukrainę na Russia kupanda kwa nishati ya kuzalishia umeme imeleta inflation duniani.

Unatuambia umeme umezalishwa mwingi inabidi wazime, ina maana TANESCO hawana substations za ku-regulate umeme, huo umeme wa Hydrogen auhitaji substation.

Unajua kwamba matumizi ya umeme ya peak na time na low time. Kwenye low demand time uzalishaji wa umeme unapunguzwa na kwenye peak time umeme unaongezeka. Kuna system za kuangalia national grid na kuwaambia wazalishaji waongeze na kuna muda wa kuwaambia wapunguze hipo ivyo duniani.

I don’t think umefanya research ya kutosha kwenye hoja yako zaidi ya kutueleza namna ya kuzalisha hydrogen tu, the rest of content are not related nor useful to society.

Mwisho kabisa kama wanauwezo wa kuzalisha umeme kwa hydro power wakapunguza kwenye low demand, si wanaweza ongeza tena unapohitajika; sasa where is the logic ya kwenda kuzalisha wa hydrogen wakati ni swala la kuwasha turbinę tu na kuongeza uzalishaji.
 
Moderators safari hii muwe na qualified judges (waliompa ushindi wa mwaka jana, technically ni upuuzi) ile sio namna ya fikra za kodi MZ

Binafsi najipa wajibu wa kiherehere wa kukosoa, kila nitakapo pata wasaa.

Sasa mtu anaandika vipi mada ya uzalishaji wa umeme wakati hakuna mahala kazungumzia issues za energy security na reliability ya sources za uzalishaji kwa uwezo wa nchi.

Mtu kama huyu hajui hata gharama za kuzalisha hydrogen energy, kwa technology ndio ni environmental friendly but very expensive kuupata huo umeme kwa technology iliyopo.

Sasa wewe una jibu la technology na wala mbinu za kuonyesha nchi itafaidika vipi na kwa namna gani.

Hata kwa essay/report ya mwaka wa kwanza chuo it’s a.failure F.

Hakuna cha maana unachoelewa katika uliyoandika.

Don’t worry you are not alone nawaendea na wengine.

View attachment 3008822

Soma hiyo report kutoka wizara ya nishati U.K. uone Hydrogen ina gharama kubwa kiasi kuzalisha MWh kulinganisha na renewable nyingine. Mind you carbon sources ni very cheaper (minus environment costs).

Ni vipi umeme wa gharama utasababisha gharama za uzalishaji kupungua. Si ndio kwanza huu mgogoro wa Ukrainę na Russia kupanda kwa nishati ya kuzalishia umeme imeleta inflation duniani.

Unatuambia umeme umezalishwa mwingi inabidi wazime, ina maana TANESCO hawana substations za ku-regulate umeme, huo umeme Hydrogen auhitaji substation.

Unajua kwamba matumizi ya umeme ya peak na time na low time. Kwenye low demand time uzalishaji wa umeme unapunguzwa na kwenye peak time umeme unaongezeka. Kuna system za kuangalia national grid na kuwaambia wazalishaji waongeze na kuna muda wa kuwaambia wapunguze.

I don’t think umefanya research ya kutosha kwenye hoja yako zaidi ya kutueleza namna ya kuzalisha hydrogen tu, the rest of content are not related nor useful to society.
Ongeza bia nyingine, bado mapema
Hivi vitu ndio tunavyotaka, combative arguments with research back up
 
View attachment 3008822

Soma hiyo report kutoka wizara ya nishati U.K. uone Hydrogen ina gharama kubwa kiasi kuzalisha MWh kulinganisha na renewable nyingine.

Mind you carbon energy sources ni very cheap (minus environment costs) ndio maana kuachana nazo kabisa wameshindwa kama unatazama mambo kwa msingi wa energy security na kulinda uchumi.

Ni vipi umeme wa gharama kama hydrogen, utasababisha gharama za uzalishaji kupungua. Si ndio kwanza huu mgogoro wa Ukrainę na Russia kupanda kwa nishati ya kuzalishia umeme imeleta inflation duniani.

Unatuambia umeme umezalishwa mwingi inabidi wazime, ina maana TANESCO hawana substations za ku-regulate umeme, huo umeme wa Hydrogen auhitaji substation.

Unajua kwamba matumizi ya umeme ya peak na time na low time. Kwenye low demand time uzalishaji wa umeme unapunguzwa na kwenye peak time umeme unaongezeka. Kuna system za kuangalia national grid na kuwaambia wazalishaji waongeze na kuna muda wa kuwaambia wapunguze hipo ivyo duniani.

I don’t think umefanya research ya kutosha kwenye hoja yako zaidi ya kutueleza namna ya kuzalisha hydrogen tu, the rest of content are not related nor useful to society.

Mwisho kabisa kama wanauwezo wa kuzalisha umeme kwa hydro power wakapunguza kwenye low demand, si wanaweza ongeza tena unapohitajika; sasa where is the logic ya kwenda kuzalisha wa hydrogen wakati ni swala la kuwasha turbinę tu na kuongeza uzalishaji.
Kwamba unahisi ninavyoandika navibuni, unachokisema nakijua.
Nilichoandika sio kwamba nishati ya hydrogen itumike kuongeza uzalishaji wa umeme, bali itumike kama kihifadhi umeme ili ikifika wakati wa kiangazi na ukame (maji yanapopungua) iwapo uzalishaji wa umeme kwa njia nyingine utapungua basi nayo itumike kuzalisha umeme .
Au itakapotokea itilafu kwenye gridi ya taifa itumike kama backup mpaka pale tatizo litakapotatuliwa.

Lakini pia kilichoonyeshwa hapo kwenye table CCGT (combined cycle gas turbine) ni tofauti na nilichozungumzia mimi cha kutumia Hydrogen kwa 100%.
1717594085558.png

View attachment 3009463View attachment 3009463
Ndugu umeme wa Hydrogen sio cheap kama unavyoongea.

Hayo makampuni makubwa huko yenye faida za net profit $500m+ yanayofikiria kwenda kwenye huo uzalishaji kwa sasa wote ni kwa sababu ya subsidises tu, lakini sio kwa kutumia retained earnings zao.

Na hakuna large scale electricity plant kwa sasa, kuna small scale pilot schemes.

US wametenga $369 billion kwa miaka 20 ijayo on research and development.

EU kwa sasa kila mwaka wanatenga zaidi €1 on subsidy ya pilot schemes.

China na kwenyewe utaratibu ni huo huo.

Hiyo hela si bora tujenge gas plants ambayo kwa sasa atutumii ata 6% ya capacity ya bomba. €1 billion nchi inapata plant size ya Kinyerezi mbili much more sensible kwenye energy security.

China inaongoza dunia kwenye uzalishaji wind farm; na kwenye nishati ya solar uzalishaji wa China in MW, US na EU wakichanganya awawafikii. Lakini China huyo ndio anaongoza kwa kuzalisha umeme wa mąkaa ya mawe.

Mipango ya energy security inaangalia reliable sources and cheap sources kwanza; haya mambo ya green Africa kiherehere tu.
 
Uzalishaji wa umeme unapokidhi mahitaji nchini unachangia kwenye ukuaji wa uchumi kutokana na shughuli nyingi za viwanda vikubwa na vidogo kuendeshwa kwa utegemezi wa umeme Umeme unapokua wa uhakika uzalishaji wa bidhaa huongezeka na gharama za uendeshaji hupungua.

Wananchi waliojiajiri kupitia shughuli zinazotegemea umeme huepuka hasara ya kuharibikiwa na bidhaa, na kwa kushindwa kuendesha shughuli zao kwa ufanisi. Jambo ambalo huwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Changamoto kubwa kwenye uzalishaji wa umeme ni kwamba umeme unahitajika kuwepo kwa kiwango sahihi kwenye gridi. Kiwango kilichopo kwenye gridi kisizidi au kupungua kiwango cha matumizi.

Hivi sasa Tanzania baada ya kuwasha baadhi ya mashine za kuzalisha umeme kwenye bwawa la Nyerere tumeshuhudia umeme ukizalishwa kupita kiasi hali inayopelekea kuzima baadhi ya mashine kuepuka changamoto ya umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa.

Bwawa la nyerere linaweza kuzalisha megawati 2115, kwa mwaka 2023 uhitaji wa umeme nchini ilikua ni megawati 1363.94. Ingawa uhitaji wa umeme huongezeka kadiri siku zinavyokwenda kutokana na matumizi kuongezeka.

Uzalishaji wa umeme wa maji huathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Uzalishaji kupungua yanapotimu majira ya kiangazi na kipindi cha ukame kutokana na mabwawa kupungua kina hivyo nguvu ya maji inayozungusha mashine za kuzalisha umeme kupungua.

Changamoto kubwa nyingine ni hitilafu za mara kwa mara zitokeazo kwenye gridi ya taifa jambo ambalo hupelekea ukosefu wa umeme kwa saa kadhaa kwenye maeneo mengi nchini.

Nishati ya hydrogeni suluhisho la upungufu/kuzidi umeme na hitilafu kwenye gridi ya taifa;
Ingawa changamoto ya umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa inaweza kutatuliwa kwa kuuza umeme nchi jirani, lakini swali la kujiuliza ni Je, umeme huo utakua wa uhakika kwa kipindi chote? Hii ni ili kuepuka kushindwa kusambaza umeme wa uhakika pindi itakapotokea upungufu wa uzalishaji au hitilafu kwenye gridi ya taifa au kuongeka kwa matumizi ya umeme nchini.

Kuepuka changamoto hii ni vizuri kuchagua njia nzuri na sahihi ya kukabiliana na changamoto za umeme nchini. Njia ambayo itaweza kutumika kwenye matumizi mengine endapo hakutotokea upungufu wa umeme.

Njia nzuri ni kuhifadhi umeme unaozalishwa na kuweza kuutumia pindi uzalishaji utakapokua mdogo. Itafanyika endapo uzalishaji wa umeme utazidi kiwango cha matumizi na kupelekea umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa. Njia nzuri na nafuu ni kuhifadhi umeme kupitia nishati ya hydrojeni. Ili kuzuia umeme kuzidi kwenye gridi ya taifa, umeme utakaozidi utatumika kuzalisha gesi ya hydrojeni na kuhifadhiwa. Umeme utakapopungua kwenye gridi gesi hiyo itatumika kuzalisha umeme na kurudishwa kwenye gridi kwa ajili ya kuepusha kukatika/mgao wa umeme.

Uzalishaji wa nishati ya hydrojeni kwa kutumia umeme unavyofanyika;
Zipo njia kuu mbili za kuzalisha nishati ya hydrojeni kwa kutumia umeme ambazo ni rafiki wa mazingira.
  • Kuvunjavunja maji (hydrolysis of water) na kupata hewa ya oksijeni na hydrojeni (H2O = H2 + O2)
Njia hii hutumia umeme kuvunja maji ya kawaida na kupata gesi ya hydrojeni na gesi ya oksijeni ambapo zote zinaweza kuvunwa na kuhifadhiwa.
Ili kupata kilo moja (1kg) ya hydrojeni kupitia njia hii inahitajika kilowati 50 hadi 55 za umeme (50-55kWh).
  • Kuvunjavunja amonia (NH3) (ammonia electrolysis) inayopatikana kwenye majitaka, mabaki na vinyesi vya viumbe hai na kupata hewa ya naitojeni (N2) na Hydrojeni (H2).
Njia hii inahitaji kilowati 1.55 (1.55kWh) ili kupata kilo moja ya gesi ya hydrojeni (1kg). Njia hii inatumia umeme mdogo zaidi ukilinganisha na ya kutumia maji ya kawaida.

View attachment 2986898
Uzalishaji wa nishati ya hydrogeni kwa kutumia ammonia (Picha kutoka mtandaoni)

Kiasi cha umeme kinachotokana na nishati ya hydrojeni
Kwa makadirio kilo moja (1kg) ya hydrojeni inauwezo wa kuchakatwa na kuzalisha umeme kilowati 23 (23kWh). Ili kupata megawati 100 (100mWh) itahitajika walau tani 4.3 za nishati ya hydrojeni.

Faida za kutumia nishati ya hydrojeni kuhifadhi umeme;
Urahisi na unafuu kuzalisha
Ni rahisi kuzalisha nishati ya hydrojeni kutokana na mahitaji yake (maji, majitaka, mabaki ya viumbe hai na vinyesi vya wanyama) kupatikana kwa urahisi. Pia ni nafuu kutokana umeme utakaotumika kuzalisha nishati ya hydrojeni utakua ni ule uliozidi kutoka kwenye vyanzo vingine vya umeme (maji, jua, upepo na jotoardhi ‘geothermal’)
Rafiki wa mazingira.
Mabaki yanayotakana na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya hydrojeni ni maji na joto, vyote hivi huweza kutumika kwa matumizi mengine. Njia hii haizalishi uchafu au hewa chafu kwenye mazingira.
Matumizi mbadala
Nishati ya hydrojeni ina matumizi mengine kama kuendeshea vyombo vya usafiri (magari n.k) na mitambo ya viwandani. Hii ni faida kwani endapo uzalishaji wa umeme usiposhuka chini ya kiwango nishati hii itaweza kuuzwa na kutumika kwenye matumizi mengine.
Usafishaji wa maji na hewa
Uzalishaji wa nishati ya hydojeni kwa kuchakata amonia inayopatikana kwenye majitaka itasaidia kusafisha maji na kuzalisha maji safi yatakayofaa kwa matumizi ya binadamu. Pia kituo cha uzalishaji wa nishati ya hydrojeni kinaweza kutumika kusafisha hewa kwa kuchuja na kuondoa vumbi linalopatikana kwenye hewa.

Ili jambo hili kufanya kazi kwa ufanisi ni vyema kufanya mambo haya;
  • Kuhakikisha kila kanda inakua na kituo walau kimoja kwa ajili ya mchakato huu,
Itasaidia uzalishaji na uhifadhi mkubwa wa nishati ya hydrojeni. Pia itasaidia kua kama mbadala (backup) pindi itakapotokea hitilafu kubwa kwenye gridi ya taifa jambo ambalo litaepusha nchi nzima kukosa umeme.
Tanzania bara na visiwani kuna jumla ya kanda 10, kila kanda ikiwekewa kituo kimoja chenye uwezo wastani wa kuzalisha umeme megawati 150 kutokana na nishati ya hydrojeni itakayokua imehifadhiwa kwenye vituo hivyo, jumla itawezekana kuzalisha megawati 1500 ambazo zitamaliza kabisa changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
  • Kufanya marekebisho kwenye gridi za umeme,
Hii ni kwa ajili ya kuhakikisha kila gridi ya umeme inabeba kiwango cha umeme inachostahili na kuepusha kubeba kiwango kikubwa cha umeme kuzidi uwezo wake jambo ambalo hupelekea kutokea kwa hitilafu za mara kwa mara kwenye gridi za umeme.

Hivyo; uhakika na utoshelezi wa umeme utafanikiwa endapo umeme unaozalishwa utatumika ipasavyo kwa kuhakikisha uwepo wake hata endapo uzalishaji utakaposhuka. Ili kufanikisha hili itahitajika kuhifadhiwa kwa umeme unaozalishwa hasa kwa kutumia njia nafuu na yenye ufanisi mkubwa. Uhakika na utoshelezi wa umeme ni chachu ya maendeleo ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmojammoja.
Mambo ya maana haya
 
Suala la umeme ni janga linalotatulika ila nawaza kwanini halitatuliwi.
 
Back
Top Bottom