Pia kijana nakushauri tazama namna ya kuwa unakaa "upstate New York " na ku commute daily kwenda New York. "Upstate" ni vimiji vinavyoiźunguka New York lakini kwa usafiri wa kule ni kama upo New York tu.
Zamani sana nakumbuka watu wakienda USA, Canada au Europe, kulikuwa kuna mpango unaitwa "world packers", huu unawasiliana kabla na unapokwenda, "unabeba boksi" kwa siku unazokuwa hapo, unapata kula na kulala.
Sifahamu kama bado upo.
Utafute kwa mtandao.
Njia zipo nyingi sana lakini muda naona hautakotosha kuzifanyia kazi, ungeanza kuuliza mapema tugekupa njia ambazo nnauhakika mojawapo ungeweza kujipatia hata kuishi bure kabisa ukajipatia pocket lmoney kila siku.
Hivi unapafahamu pale Dar YMCA? kama ni wa kike YWCA?
Kama unapafahamu ukifika hapo umeshatatuwa tatizo lako. Nenda kawaone.